Maarifa Hatari: Embu tujifunze na kumjadili huyu Shetani vizuri

Habari yako imekaa kiimani zaidi.

Kwasababu habari ya Mungu na shetani ni hadithi tu

Hakuna Mungu, hakuna shetani katika ulimwengu halisi.

Yote haya ni mapokeo ya kidini yanayopandikizwa vichwani mwa waamini ili kuzifurahisha hisia zao.
Je, unaweza kuthibitisha hilo?
 
Shetani ni dubwasha likubwa sana hata Mungu 'ameshindwa' kupambana nalo eti anaturushia sisi wanadamu tuhangaike nalo! Tutaweza kweli? Sidhani mi sina time ya kupambana na shetani. Mungu kama anatupenda atusaidie kuliangamiza tuishi vizuri.
 
Bado kauli hii ina ukakasi, nadhani na wewe unajua ila hautaki tu kukiri
Unaelewaje ^usizitegemee akili zako mwenyewe^ na ^usizitumie akili zako^?

Biblia haisemi usizitumie akili zako, bali zisiwe mwongozo, na kumfanya mwanadamu aishi nje ya Mungu.

Ukakasi uko wapi?
Hili si kweli, hata maneno yako yanakiri kwamba binadamu hatakiwi kufuata utashi wake mwenyewe
Ukatoliki ndio umekuwa ukifundisha tangu karne na karne hadi sasa kwamba fikra ya mwanadamu haipaswi kuwa huru nje ya mafundisho ya Ukatoliki.

Kwa maneno mengine, muumini hapaswi kuwa na utashi huru. Kamwe hilo si fundisho la Biblia.

Kila mahali Biblia imeonesha kwamba mwanadamu amepewa uhuru wa kuchagua, ama kumtii Mungu au kufuata utashi wa nafsi yake, kama alivyofanya Shetani.

Uamuzi wa kumtii Mungu na kuishi, au kumwasi na kuangamia, uko kwa mtu mwenyewe.

^Waambie, Kama Mimi niishivyo, asema Bwana MUNGU, sikufurahii kufa kwake mtu mwovu; bali aghairi mtu mwovu, na kuiacha njia yake mbaya, akaishi. Ghairini, ghairini, mkaache njia zenu mbaya.^ Ezekieli 33:11

ambayo kwa tafsiri nyingine utashi huo unaweza kuhusishwa na kutafuta maarifa na maendeleo.
Kama nilivyojibu kwenye swali lililopita, si kweli hata kidogo kwamba mwanadamu akiwa chini ya mamlaka ya Mungu hawezi kupata maendeleo na wala kufanikiwa.

Kinyume chake, msingi wa maendeleo na mafanikio ya mwanadamu hutegemea kujiweka kikamilifu katika usimamizi wa Muumba wake.

Maisha ya Ibrahimu, Daudi, Sulemani, na wengine wengi wacha-Mungu katika historia huthibitisha hilo pasi na shaka.

Ni kweli Shetani anaweza kumpa mtu utajiri na mafanikio (ya muda), lakini haina maana kwamba kuwa chini ya utawala wa Mungu ni kuchagua umaskini.

^Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao siku zote, wa kunicha, na kushika amri Zangu zote siku zote, wapate kufanikiwa wao na watoto wao milele!^ Kumbukumbu la Torati 5:29
 
Elimu nzito katika mistari michache.

Ahsante mkuu
 
Kazi kweli kweli


Bado haujajibu swali langu. Sijaongea mpaka umsujudie shetani, nimeongea kwa utashi wake mwenyewe hawezi kuleta hivyo?
Shetani anaishi kwa malengo. Tangu aasi mbinguni na kutupwa chini, na kuiweka dunia chini ya mamlaka yake, hufanya kila jitihada za kuongeza raia wa ufalme wake.

Katika kutimiza azma hiyo, silaha yake kubwa ni ushawishi wa hila, uongo, udanganyifu. Hupandikiza chuki baina ya mtu na mtu, taifa na taifa. Huzalisha na kueneza magonjwa.

Hutumia umaskini kuwateka na kuwatumikisha na kuwapotosha wanadamu. Husababisha ajali, majanga, na mateso kwa mwanadamu na viumbe duniani. Shetani hutenda kazi kupitia watu waovu walio mawakala wake.

Shetani huweza kukupa mafanikio kwa lengo la kukushawishi umwache Mungu na kujiweka chini ya mamlaka yake.

Ndiyo maana akamwambia Yesu angempa utajiri wote wa dunia iwapo Kristu angekubali kumsujudia.

Mwanadamu kuusalimisha utashi wake kwa Shetani, siyo lazima mpaka amsujudie kihalisia. Kile kitendo tu cha kukubali na kufanyia kazi pendekezo la Shetani, huko ni kumsujudia Shetani.

Kwa maneno mengine, mtu anapokubali kutekeleza nia na mawazo ya Shetani, hapo anakuwa mtumishi wa Shetani – anamsujudia Shetani.
 
Anayeweza kuwa kila pahali kwa wakati mmoja ni Mungu Mwenyezi pekee, wengine wote huwa pahali pamoja kwa wakati mmoja.

Shetani kamwe siku hizi hana access ya moja kwa moja na wanadamu, hutumia human agents kuwafikia wanadamu. Hata wazamia kuzimu hukutana na kiumbe mwenye kubadilika badikika aijitambuisha kama Shetani lakini sio, ila ni human agent wake, mostly a powerful marine spirit ajilikanaye pia kama Queen of the Coast.

Biblia imeandikwa kwa lugha ya picha na inahitaji tafsiri nzuri, maarifa ya kiroho, na taarifa kutoka kwenye shuhuda zilizothibitika.
 
Hizi ni nadharia ambazo ndiyo zinatufanya tushindwe kuyaelewa haya mambo. Naomba turudi kwenye uhalisia wa kweli wa maisha
Okay nafikiri kuna watu wana shuhuda za kweli za matukio ya kweli ya kujichanganya na kufanya kazi na shetani ni kweli shuhuda hizi zinasisimua na kufungua macho sana. Kama unapenda story hizo nitakuelekeza wapi utazipata.
 
Anayeweza kuwa kila pahali kwa wakati mmoja ni Mungu Mwenyezi pekee
Sahihi.
wengine wote huwa pahali pamoja kwa wakati mmoja.
Sahihi.
Shetani kamwe siku hizi hana access ya moja kwa moja na wanadamu,
Siyo kweli.

Umesema ^siku hizi.^ Je, alianza lini kukosa hiyo access?

^Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze.^ ~ 1 Petro 5:8
hutumia human agents kuwafikia wanadamu.
Sahihi
Hata wazamia kuzimu hukutana na kiumbe mwenye kubadilika badikika aijitambuisha kama Shetani lakini sio, ila ni human agent wake, mostly a powerful marine spirit ajilikanaye pia kama Queen of the Coast.
Kuzimu ni nini na wapi? Unapaelewaje?
Biblia imeandikwa kwa lugha ya picha na inahitaji tafsiri nzuri, maarifa ya kiroho, na taarifa kutoka kwenye shuhuda zilizothibitika.
Biblia ina mashairi, mithali na hekima, historia, unabii, vielelezo ama mifano, sheria, riwaya na visa, falsafa, sayansi, nk.

Humo zimetumika mbinu zote za ufundi ama sanaa ya lugha (isimu) -- tamathali za semi.

Sasa lugha ya picha ni kipande kimoja tu ambacho kimehusika, na wala siyo kote, Mwanzo hadi Ufunuo.

Kwa mfano, vielelezo vya Yesu ni sehemu mojawapo ambapo Biblia imetumia lugha ya picha.

Lakini sehemu za Biblia kama vile matukio ya uponyaji na huduma ya Kristu, kwa sehemu kubwa hivyo ni visa vya moja kwa moja, ambavyo humhitaji mtu ajue tu lugha rahisi husika ili avielewe.

Ni upotoshaji kulazimisha kila andiko la Biblia lisomeke kama lugha picha inayowakilisha kitu fulani kisichojulikana wazi moja kwa moja kutokana na maneno yaliyotumika kukielezea.
 
Alafu unawasikia wajinga siku za ibada wakiomba eti wanamkemea shetani na kumkanyaga[emoji1787][emoji1787].

Mpaka kizazi hiki hakuna mwenye uwezo wa kumpinga shetani, iwe mchungaji,nabii wala shekhe.

Hao mnaosema mnashindana nao na kuwakemea ni vibaraka wa shetani ambao ni jeshi la nafasi/level ya chini sana.

Shetan unatakiwa ujue kuwa huko ulimwengu alikotoka kabla hajafukuzwa alikuwa na Cheo cha KERUBi, yaani kiumbe wa kiroho ambaye ni zaidi ya malaika, mbingun kuna viumbe wengi wa kiroho wakitofautiana vyeo,nguvu na majina yao kulingana na nguvu zao.

Kerubi sio malaika,maserafi sio malaika, bali ni kiumbe cha kiroho chenye cheo juu ya hao malaika, wachungaji wamewadanganya sana kuhusu elimu ya viumbe wa kiroho.

Shetan huko huko mbinguni sio kwel kuwa alikuwa Mkuu sana, bali alikuwa na cheo ambacho kikubwa kwa baadhi ya viumbe(malaika) lkn wapo viumbe waliokuwa wakuu na wenye nguvu zaidi yake ambao baadhi walishiriki kumfukuza mbinguni.

Viumbe waliofukuzwa na shetan ni malaika yaan viumbe wa cheo kidogo ambao shetan aliweza kuwashawishi kulingana na uwezo wake na cheo chake.


Baada ya kuja dunian, shetan alishawishi baadhi ya wafuasi wake(malaika) kufanya unajisi wa Uzao wa viumbe vya dunian kwa kushiriki Uzazi baina ya viumbe wa kimbingu(malaika) na viumbe wa dunia wakiwepo binadamu,wanyama,wadudu ndipo likaibuka kundi la uzao chotara ambao bible zenu zinawaita Nephilims/giants, chotara hawa ndio chanzo cha uzao wa viumbe wapya wa kiroho waitwao Mapepo/majini maana hawa ndio kundi la mwisho la uzao wa viumbe wa kiroho.

Simple, baada ya Mafuriko ya Nuhu yaliyolenga kuangamiza uzazi haramu, basi miili ya hao Nephilims ilikufa lkn Roho zao ziko hai, maana Roho haifi bali mwili, na hizo Roho za wale Nephilims yaani chotara wa viumbe wa kimbingu(malaika) na uzao wa viumbe wa dunian kama vile wanadamu na wanyama,ndio uzao matokeo ya hao Chotara ambao baada ya miili yao kuangamizwa zikabaki roho zao ambazo ndizo tunaita Mapepo.

Mnatakiwa mjue kutofautisha kati ya mashetan,majini au mapepo, shetani sio pepo, wala mapepo sio mashetan, bali shetan ndie kiongozi ama kiongozi wa malaika wasariti ambao ndio Baba wa mapepo yoote hapa dunian.

Na kwa level zetu wanadamu viumbe tunaoshindana nao ni mapepo yaan jeshi la shetan la cheo kidogo, mambo ya kiroho yanakwenda kwa Utaratibu, huwezi kumpambanisha kiumbe mwenye nguvu kubwa zaidi kuliko mpinzani wake, ndiomaana mpaka sasa Shetan hawezi kuja duniani kushindana na viumbe dhaifu wanadamu wakati analo jeshi la viumbe wanaoweza kutushughulikia haswa na tusiwashinde.

Ogopa kiongozi wako wa kidini anayesema anashindana na shetan, kwa level zetu hakuna mwenye huo uwezo wa kushindana na shetani maana ana uwezo zaid ya viumbe wote hapa dunian.

Ili kushindana na shetan kwanza unatakiwa uwe na uwezo wa kuwashinda jeshi lake la cheo cha chini kama vile mapepo ambao wako na matabaka mbalimbali kama vile majini/mizimu,vibwengo, vikaragosi na mapepo yote ya kila aina, ndipo uje ushindane na kundi la malaika ambao shetani alishuka nao ambao ndio wenye cheo cha juu katika Rank ya uongozi wa shetani na ndipo sasa umfuate Yeye mwenyewe shetani ushindane nae baada ya kuwashina majeshi yake.

Kwa namna hiyo kuna binadamu hapa dunian mwenye uwezo wa kumfikia shetan??.

Kama vijipepo tu vinatuendesha na kutuenyesha sana je hao malaika wa shetan wa cheo cha kati mtawaweza? Na shetan mwenyewe mtamuweza?

Dini zinawapotosha sana na zimepotosha sana kuhusu hiyo Elimu ya viumbe wa kiroho na Ujuzi wao hiyo yote ni kwakuwa shetani ndie Mungu wa hii dunia na ndie Mungu wa dini zote na ndie aliyeamlisha ziundwe na zimuabudu yeye kwa majina ya vificho.

Hakuna binadamu kwa kizazi chetu mwenye uwezo wa kumface Shetani, Msidanganywe, shetan ni zaid ya mlivyoaminishwa, sio kumpa sifa bali ni ukweli ambao hautaambiwa na hao matapeli wenu wa ibada za makanisan na misikitin, hawa wote viongoz wenu wa kidini hakuna hata mmoja anaeweza kugusa Wala kumtetemesha shetan.

Shetan ndie anaitawala dunia indirect kupitia dini na viongozi wake wa kisiasa lakin kama akija yeye kama yeye hakuna dunian kiumbe wa kusalia bali ni Neema za Muumba kuweka balance ya Nguvu za kiroho ili kumzuia shetani asiuharibu mfumo wa dunia na viumbe wa kidunia or otherwise sote tungefutika.

Shetan ni more powerful zaidi ya mlivyodanganywa na dini zenu za uongo.
 
Makerubi sio malaika, ni sawa na kusema kingdom ya wanyama kuna akina simba,nyati,chui, ng'ombe mpaka binadamu.

Sasa unaposema shetan ni malaika ni sawa na kusema ktk kundi la wanyama chui ni simba, jambo ambalo si kweli.

Malaika ni aina ya viumbe wa kiroho,kerubi ni cheo cha juu cha viumbe wa kiroho ambao sio , malaika,maseraf vile vile.

Someni elimu hii ambayo haipo katika hizo ngonjera zenu za biblia na quran, elimu hii ni kubwa kuliko baadhi ya akili zenu ndiomaana mmepotoshwa sana kumuhusu shetani
 
Mmelishwa Matango pori. Hakuna kitu kiitwacho shetani. Hizo ni nadharia za kuwapumbaza. Ebu fanya kama shetani hayupo, je Mungu atakuwepo?
 
"Shetani" siyo kiumbe tofauti, ni binaadam mwenyewe, ushetani ni sifa tu.
 
"Shetani" siyo kiumbe tofauti, ni binaadam mwenyewe, ushetani ni sifa tu.
Wow! Haya sasa ndiyo maarifa hatari.

Wengi bado wanarudia maneno yale yale ambayo wote tunayajua na tumeyasoma, nawakumbusha wote tujiongeze kwa kuangalia uhalisia wa maisha, siri kubwa ya haya mambo tutaijua kama tutafumbua macho yetu na kuwa na utashi wa kutambua mambo kwa jinsi yalivyo. Tumepewa akili ili tuweze kung'amua mbivu na mbichi.

Embu funguka zaidi Bi Faiza.
 
Shetani mbona tunaishi naye mkuu, kama wewe ni Muislam unafikiri unamuabudu nani?
 
"Shetani" siyo kiumbe tofauti, ni binaadam mwenyewe, ushetani ni sifa tu.
Kwa maana hiyo Mohammed alishukiwa na mwanadamu mwenzake na kupewa haya za Qur'an? Kumbuka baada ya kushukiwa, Mohammed akawa kichaa na kupotea kusikojulikana kwa miaka kadhaa, kisha akarudi baada ya kupona ukichaa na kujifanya kashukiwa na Mungu na kupewa Qur'an. Usicheze na shetani wewe, uliza Mohammed akuambie ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…