Maarifa Hatari: Embu tujifunze na kumjadili huyu Shetani vizuri

Naona hata maana ya malaika hujui. Malaika ni mtumishi wa Mungu, mjumbe wa Mungu, wa kiroho.

Hao wote uliowataja - maserafi, makerubi, Shetani (Lusifa, wakati huo), ni malaika.

Kuna malaika wema na waovu. Waovu ndio hao mapepo au pepo wachafu, majini, nk
 
Mmelishwa Matango pori. Hakuna kitu kiitwacho shetani. Hizo ni nadharia za kuwapumbaza. Ebu fanya kama shetani hayupo, je Mungu atakuwepo?
Uwepo wa Mungu, Shetani, malaika watakatifu na waovu, mbingu, ufufuo, na umilele ni halisi kama uhalisia wa uwepo wa mwanadamu, mbingu na nchi.

Hapo ndipo tunapata maelezo pekee kamili kuhusu asili ya mwanadamu, uumbaji, kusudi na hatima yake.

Nangoja ulete hoja mbadala.
 
"Shetani" siyo kiumbe tofauti, ni binaadam mwenyewe, ushetani ni sifa tu.
Ukisema: ^Yule jambazi ni shetani hasa.^ Uhusika wa Shetani umebebwa na jambazi anayetajwa.

Ni wazi kwamba kinachoongelewa hapo ni hulka ya Shetani iliyoakisiwa kwenye matendo ya huyo jambazi, na wala si kwamba yeye ndiye nafsi halisi ya Shetani.

Hata hivyo, uwepo wa Shetani ni halisi. Kama ambavyo mtu mwema huiakisi tabia takatifu ya Mungu, mtu mbaya naye huiga na kuakisi matendo ya Ibilisi Shetani.

Ibilisi Shetani ni kiumbe halisi, Lusifa kwa wakati ule kabla hajamwasi Mungu, akatupwa duniani.
 
Huwez kumjua Mungu au shetan vizuri kama hukufunuliwa na Roho Mtakatifu. Hii Dunia tuko two way traffic. Kwanza ili hicho unachota kukijua unatakiwa uondoe kile unachokiamini kwanza ili uwe free kujifunza hiyo njia mpya. Pili system ya kiroho na kimwili ni tofauti sana. Huwez kujua namna roho zinavyofanya kazi ukiwa kwenye mwili. Lazima na wewe uwe wa rohon maana mstari mmoja wa Biblia unaweza ukawa na maana tatu tofauti. Na Mungu huwez kumjua kama hujanyenyekea na kutii
 
Mwili wa mwanadamu mfano wake rahisi tunaweza kusema taa ya umeme.

Umeme ukiunganishwa, taa inawaka. Umeme ukitenganishwa, taa inazima.

Nguvu ya umeme huo ndiyo Biblia inaita ^pumzi ya uhai,^ wakati mwili ni udongo ama mavumbi.

^Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.^ ~Mwanzo 2:7

Mavumbi ya ardhi + pumzi ya uhai = nafsi hai

Kama ambavyo umeme wenyewe hauwezi kuwaka bila taa, pia pumzi hiyo ya uhai aliyopuliziwa mwanadamu haiwezi kuwa hai kwa yenyewe bila mwili ama mavumbi.

Mwili na pumzi ya uhai kwa pamoja huunda nafsi hai.

Zikitenganishwa hizi mbili unapata vitu vilevile, ambavyo ni mavumbi na pumzi ya uhai.

Ndiyo maana kaburini kuna mifupa tu, na hatimaye mifupa nayo husagika na kurejea kuwa udongo.

Habari ya roho inayojitegemea, iliyo hai, siyo fundisho la Biblia. Huo ni upotoshaji dhahiri kutokana na falsafa za Kiyunani.
 
Habari ya roho inayojitegemea, iliyo hai, siyo fundisho la Biblia. Huo ni upotoshaji dhahiri kutokana na falsafa za Kiyunani.
Ingekuwa vizuri kila mtu akatoa maoni yake katika uzi huu kulingana na imani yake au kile anachokielewa bila kunyoosheana vidole na kuambiana fulani anapotosha au fulani ni agent wa shetani. Inawezekana kujadiliana na kuhoji hoja za mwingine bila kutumia lugha ya kukwazana. Tuishi humo.
 
Sijabobea sana mambo ya dini ila mwanadamu yupo kwenye unfair battle dhidi ya shetani na malaika zake.
Huko ni kushindwa kutambua vizuri asili ya mwanadamu na uwezo alio nao. Biblia inafundisha kwamba mwanadamu ameumbwa kwa ^sura na mfano^ wa Mungu.

Sura na mwili wa mwanadamu, Mungu aliviumba ili kumwakisi Yeye. Kristu alipoutwaa mwili huu wa mwanadamu, alimshinda Shetani. Na ndivyo hivyo pia nasi tunapaswa kumshinda Shetani.

Shetani ni adui aliyeshindwa tayari. Badala ya kuhofia uwezo wake, ni vyema tukatafakari na kujinufaisha kwa uweza mkuu wa Mungu, tunaopewa kupitia neema ya Mwanawe Yesu Kristu.

^Tazama, nimewapa amri ya kukanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hakuna kitu kitakachowadhuru.^ ~Luka 10:19
Ndiyo maana Biblia huviita kwamba ni vita katika ulimwengu wa roho. Ili ashinde vita, lazima mwanadamu avae ^silaha zote za Mungu,^ ambazo zimetajwa huku Efeso 6:11-18.

Kwenye maelezo yako umeandikwa kwamba angekuwa na ^uwezo wowote wa kutengeneza silaha^ ili amkabili Shetani, basi angemshinda.

Lakini tunajua silaha zote zipo tayari, hoja ni utumiaji wa silaha hizo.
 
Mkuu kama kama Mikaeli alimshinda shetani kwanini hakumuua kabisa ili sisi tusipate tabu?
Sasa kwa nini Mungu asimuue shetani tukawa watu wema wote. Je shetani ana faida gani kwa Mungu?
Bila shaka kuna manufaa makubwa sana kufuatia hekima ya Mungu kumwacha Lusifa aendelee kuwa hai, licha ya uasi wake na kuwalaghai malaika wengine wamfuate.

Sisi kama wanadamu, bado hatujajua kila kitu husika. Lakini kitendo cha Lusifa kutupwa hapa duniani, ni wazi kwamba kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya uasi wake mbinguni na upinzani wake dhidi ya mamlaka ya Mungu.

Mungu anaudhihirishia ulimwengu wote wema, huruma, uvumilivu na upendo Wake mkuu kwa viumbe Wake; na pia kuhusiana na ukuu, haki na utakatifu Wake, kwa jinsi anavyoshughulikia suala la Shetani (na waasi wenzie).

Vilevile, Mungu anatuonesha hatari kubwa iliyoambatana na uamuzi Wake wa kutuumba kwa ^sura na mfano^ Wake.

Ni dhahiri kwamba Lusifa na malaika waasi, na wanadamu wadhambi, wameshindwa kutambua thamani ya tunu kuu ya uhuru wa utashi (free will).

Tunaweza kusema kwa hakika kwamba miongoni mwa amana zote adhimu na maridhawa ambazo Mungu angeweza kumpa mwanadamu, uhuru wa utashi ni mojawapo.

Ndicho hutufanya tuwe wanadamu kamili hasa, tukifikiri na kutenda kwa utashi wa nafsi zetu.

Tunu hii bora ilipotumika vibaya, dhambi ikaingia – kwanza mbinguni, na kisha duniani kwa viumbe wa Mungu wapya. Huzuni ilioje!

Kitendo cha Mungu kumwacha Shetani aendelee kuwa hai ni namna fulani ya kumpa nafasi atekeleze hoja za madai yake dhidi ya Mungu.

Ukisoma kuhusu mahojiano ya Mungu na Ayubu katika kitabu cha Ayubu, ni kana kwamba Shetani alidiriki kumpa Muumbaji wake changamoto, na Mungu kwa hekima Yake kuu, akaikubali.

Changamoto hiyo ndiyo jaribio kuu ambalo Ibilisi amekuwa akiifanyia kazi duniani kwa miaka 6,000 sasa.

Ni bayana kwamba hoja mahususi za Lusifa dhidi ya mamlaka ya Mungu zingeweza kujibika kikamilifu na mazima milele (completely and finally forever), kwa mujibu wa hekima kuu ya Mungu na silika Yake takatifu na yenye upendo, kwa kuwaruhusu viumbe Wake wenye utashi huru japo ^wachungulie^ ng’ambo ya pili kwa kuhabiri (experience) maisha nje ya Mungu.

Ingekuwa wengi hawajarukwa akili leo, wangetambua manufaa tele katika uvumilivu huu mkuu wa muda mrefu wa Mungu kwa Ibilisi na jeshi lake, licha ya taabu, maumivu, na mauti ambayo wameyachochea na kuyasababisha tangu ulimwengu kuumbwa.

Hatimaye, baada ya yote, sote tutatambua kwamba kweli Mungu ndiye mwenye mamlaka, kweli, hekima, heshima, haki na ukuu.

^Nao wauimba wimbo wa Musa, mtumwa wa Mungu, na wimbo wa Mwanakondoo, wakisema, Ni makuu, na ya ajabu, matendo Yako, Ee Bwana Mungu Mwenyezi; Ni za haki, na za kweli, njia Zako, Ee Mfalme wa mataifa.^ ~Ufunuo wa Yohana 15:3
 
Asante mkuu kwa maelezo yako. Nashukuru sana kwa kutumia muda wako kunielewesha. Ubarikiwe sana mkuu.
 
Hutumia ushawishi kupitia watu na uwezo wake upo limited sana hajaachwa aranderande atakavyo.
Weka andiko.

Weka andiko la kuthibitisha hoja.

^Kuzimu^ ni shimoni au kaburini au makao ya wafu. Agano la Kale linatumia neno ^sheol^ na Agano Jipya ^hades.^ Zaburi 89:48; 30:3; 16:10; Hesabu 16:30; Matendo 2:27, 31.

^Wanawe wote, na binti zake wote, wakaondoka wamtulize, lakini akakataa kutulizwa, [Yakobo] akasema, La! Nitamshukia mwanangu, nikisikitika, hata kuzimu. Baba yake akamlilia.^ ~Mwanzo 37:35

^Bahari ikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake; na Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu waliokuwamo ndani yake. Wakahukumiwa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.^ ~Ufunuo 20:13
 
Kwanini unahadaa watu kwa kutumia kitabu duni chenye migongano kila kona!?

Unalazimishaje kuwa habari hizo kuwa ni za kweli ilihali zinamigongano diaba zima!?
 
Mada iko kiimani kwa kiasi fulani kwa kuanzia ila tunavyoendelea kuijadili najaribu kuwasisitizia wachangiaji wajikite katika uhalisia wa maisha na experience tunazoziona katika maisha yetu ili tumjue Shetani vizuri
Sawq ili tuondoke kwenye imani,

Nieleze shetani ni nani/nini!?

Na unathibitishaje uwepo wake!?
 
Hakuna dini hakuna shetani, dini na shetani ni vitisho walivyotuletea wahuni Wazungu na Waarabu ili kutugawa na kututawala, kupitia dini na shetani binadamu tunatiwa hofu sana ili tusijitambue na kujipambania kifikra na kiakili.
 
Sawq ili tuondoke kwenye imani,

Nieleze shetani ni nani/nini!?

Na unathibitishaje uwepo wake!?
Hayo ni maswali yangu pia na ningependa tujadiliane na wadau kulingana na kila mtu mitazamo yake na experience zake. Tukijadiliana kwa staha bila kukaza mafuvu mbona ukweli tutaujua humu humu ndani?
 
Mjue sana Mungu ili uwe na amani ndipo mema yatakapokujia. Pamoja na hayo, lazima ujue mwanadamu pasipo Mungu, hawezi shinda ufalme wa giza hapa duniani. Ndiposa Yesu alikuja, na kwa damu yake akatununua kwa gharama kubwa.
 
Shetani ni Serafi mkuu, sio Kerubi. Maandiko mengi yanamtambua Shetani kama "An angel of THE HIGHEST ORDER, once loved above all others."

Kuna kitabu cha mwandishi mmoja anaitwa Dr Dyaboli kinaitwa HOW TO SELL YOUR SOUL TO SATAN kimeichambua kwa undani sana nadharia ya shetani kwamba huyu shetani ni nani au nini na uwezo wake. Na kimsingi hatupaswi kumwogopa shetani, adui yako ukimwogopa tu unakuwa umedhihirisha udhaifu wako tayari

Nakuwekea hapa attachment ya hicho kitabu
 

Watu wanarukaruka tu hawataki kujibu swali lako linauliza 'MIMI NI NANI'
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…