Maaskofu na Mashekhe: Tunataka tume huru ya Kijaji kuchunguza matukio yanayoendelea Tanzania kati ya Serikali na Chama cha Upinzani

Maaskofu na Mashekhe: Tunataka tume huru ya Kijaji kuchunguza matukio yanayoendelea Tanzania kati ya Serikali na Chama cha Upinzani

Wakiongea kupitia BBC maasikofu na wachungaji wamesema wanasikitishwa na hali inayoendelea Tanzania juu ya matukio ya watu kushambuliwa na hata kuvunjwa mikono. wanasema wanataka iundwe tume huru ya kijaji kwa kuwatumia majaji wastaafu.

Wanasema majaji wastaafu wanaweza kutokuwa na upendeleo wakitoa report yao pia wameonya iwapo haitafanyika na kutoa haki sawa kwa wote taifa litagawanyika

Wameongeza kuwa pamoja na kwamba sio watu wa siasa ila wanao wajibu wa kukemea maovu maana wanao umizwa ni moja ya waumini wao ivyo ni wajibu wao kuikumbusha serikali kama kuna mambo hayaendi vizuri wayarekebishe haraka wasisubiri mpaka amani itoweke.

Chanzo: BBC.

======

Kamati ya Kitaifa ya pamoja ya Maaskofu na Mashekhe ya Maadili, Amani na Haki za Binadamu kwa Jamii ya Madhehebu ya Dini nchini Tanzania wataka kuundwa tume huru ya kijaji, kuchunguza mvutano unaoendelea kati ya Serikali na Chama cha upinzani, kufuatia Sakata la wabunge wa CHADEMA kupigwa na kuumizwa huko Gereza la Segerea.

Wamesema jopo hili la majaji ndio linakwenda kumaliza minong'ono na chuki inayoendelea katika jamii.


Wasitumie mwamvuli wa dini wajitokeze tu hadharani maana hao inaonesha dhahiri ni viongozi vivuli wa CHADEMA na si viongozi wa dini kama wanavyojinasibu
 
Chadema mnataka kutupeleka kwenye udini na hao maaskofu wenu. Mkiambiwa na chama cha kidini mnakataaga lakini kila uchaguzi mnatumia udini na ukasikazini.

Hii coincidence vipi maaskofu wenye asili ya ukasikazini wanakuwa na stand moja na chadema? Hii ni conspiracy na ni udini plus ukabila
Hazikutoshi ongeza akili kidogo hata za kuku

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hujasoma kuwa ni kamati ya viongozi wa dini ndiyo iliyotoa tamko hilo? Hiyo kamati inajumuisha viongozi wawakilishi toka dini zote na madhehebu yote.
Hakuna kamati ya uongozi wa dini zote Tanzania labda uliko huko!
 
Bams

Kwa bahati mbaya sana, uliyoandika hapo juu #14 ni kama umeyatupa tu jalalani au yamechukuliwa na upepo na kutokomea kusikofahamika.

Hivi, JF hapawezi pakawepo na utaratibu maalum wa ku'highlight' michango ya kipekee kabisa kama huu uliouweka hapa watu waka'focus' juu yake na kuyatafakari yaliyoandikwa humo?

Najua kuna ile "Sticky" hapo juu.

Nazungumzia "HIGHLIGHT",hata ya siku moja au wiki hivi.
3) Kama walitenda kosa linalostahili adhabu, ni nani mwenye haki za kisheria kutoa adhabu? Ni Polisi, ni mahakama au ni magereza?

4) Kama walitenda kosa, ni hatua gani zilistahili kuchukuliwa? Ni kuvunjwa mikono na askari magereza, kufikishwa mahakamani au kuuawa na hao Askari magereza?

Hivi vyombo hivi vya serikali havioni kabisa kwamba wanakiuka sheria?
 
Jipeni tu moyo
Hao maaskofu hawatutendei haki,nchi inahangaika na corona,wao wanataka tume huru kuchunguza mdee kuvunjwa mkono!

Siasa za kitoto hizi,unakwenda magereza kufanya fujo unategemea nini?tume ya kijaji ichunguze nini hapo kila kitu kipo wazi.

Maaskofu wamechoka na ushwari wa nchi
Kuchunguza tukio ndio kufunja amani ? hii IQ yako nimeipenda
 
Wasitumie mwamvuli wa dini wajitokeze tu hadharani maana hao inaonesha dhahiri ni viongozi vivuli wa CHADEMA na si viongozi wa dini kama wanavyojinasibu
Yatakapo kukuta utalazimishwa kuyasema,huu kipofu sababu u mnufaika
 
Na
Hiyo ni fallacy...nilifikiri tutazame hoja yenyewe bila kujali anayeitoa hoja anatokea upande gani? Unataka kutuambia Askofu akitoka au mwenye asili ya kaskazini hoja yake inakosa umuhimu kwa sababu tu anatokea kaskazini? Hivi huu ujinga wa kutaka kuligawa taifa hili kwa misingi ya ukabila na udini nani anawajaza vichwani mwenu? Juzi tumemsikia mwenyekiti wenu pale Mbezi anamtaja Mushi kama mtu mwenye jina hilo kuwa "hapaswi kuaminiwa". Huu ni ujinga na komeni!
Na nyinyi mkome kutufanya watanzania wote hatuna akili. Tuna macho, masikio so tunajua kufanya tathimini.
 
Kitima ana moral values kumevaluate magu?

Kwani majaji ndiyo wanatoa haki pekee?
Kwa nn isiwe tume ya wanasheria wabobezi wenye Nguvu kuliko wazee.

Hatuhitaji tume tunataka taarifa ya tume ya haki za binadamu ktk haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom