Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 378
- 766
Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC) limetoa tamko kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, leo Novemba 15, 2024 likisistiza una umuhimu mkubwa kwa ustawi wa Jamii na Nchi kwa ujumla
Tamko hili limewasilishwa na Rais wa TEC, Askofu Wolfgang Pisa, amesema "Tunasisitiza TAMISEMI ina jukumu kubwa la kufanya na kuhahakisha zoezi zima la kupiga kura linafuata misingi ya #Demokrasia na kuwa wale tu walioshinda kihalali ndo wanapaswa kutangazwa kuwa Viongozi halali wa eneo husika."
Anasema "Tusitengeneze Jamii ya ulaghai, tujenge Taifa linalolelewa kwenye ukweli na linafanya kazi katika ukweli. Maaskofu wa Tanzania tusingependa nchi yetu itumbukie kwenye vurugu zinazosababishwa na Uchaguzi huu, hii ni njia ya kupata Viongozi wataoweza kuendesha Uchaguzi wa kupata kwa uhuru na haki."