Greenwhich
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 1,337
- 968
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema amefurahishwa na uamuzi wa Tamko la Maaskofu wa Makanisa yote nchini ya kuikataa Katiba Pendekezwa.
Jaji Warioba amesema ni ukweli ulio wazi kwamba maoni mengi watanzania waliyotoa yamepuuzwa kwenye Bunge la Katiba la Samwel Sitta na badala yake kuingizwa maoni ya watawala.
Jaji huyo mstaafu amesema Tamko la Maaskofu kuomba muda zaidi wa kusoma katiba pendekezwa kabla ya kura ya maoni ni muafaka kabisa hasa ikizingatiwa viongozi wa dini ndiyo wenye waumini.
Tayari leo Jumapili Makanisa yote ya Kikatoliki nchi nzima umesomwa waraka wa kinabii wa kuikataa katiba pendekezwa kwani imebeba maoni ya chama kimoja tu cha CCM.Na waraka umesisitiza katiba hiyo ilipatikana kwa njia ya HILA kubwa.
Mwaka jana Shura ya Maimamu wa dini ya Kiislamu ndiyo ilikuwa taasisi ya kwanza ya dini kuikataa katiba Pendekezwa na kuwataka Waislam wote kupiga kura ya HAPANA