Maaskofu wameitendea haki Katiba mpya - Warioba

Greenwhich

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
1,337
Reaction score
968
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema amefurahishwa na uamuzi wa Tamko la Maaskofu wa Makanisa yote nchini ya kuikataa Katiba Pendekezwa.

Jaji Warioba amesema ni ukweli ulio wazi kwamba maoni mengi watanzania waliyotoa yamepuuzwa kwenye Bunge la Katiba la Samwel Sitta na badala yake kuingizwa maoni ya watawala.

Jaji huyo mstaafu amesema Tamko la Maaskofu kuomba muda zaidi wa kusoma katiba pendekezwa kabla ya kura ya maoni ni muafaka kabisa hasa ikizingatiwa viongozi wa dini ndiyo wenye waumini.

Tayari leo Jumapili Makanisa yote ya Kikatoliki nchi nzima umesomwa waraka wa kinabii wa kuikataa katiba pendekezwa kwani imebeba maoni ya chama kimoja tu cha CCM.Na waraka umesisitiza katiba hiyo ilipatikana kwa njia ya HILA kubwa.

Mwaka jana Shura ya Maimamu wa dini ya Kiislamu ndiyo ilikuwa taasisi ya kwanza ya dini kuikataa katiba Pendekezwa na kuwataka Waislam wote kupiga kura ya HAPANA
 
ni kwel huko nakanisa yote ya roman imesomwa? ngoja niulizie
 
  • Thanks
Reactions: nop
Sio Leo tu tamko linasambazwa mpaka ngazi ya jumuiya ndogondogo. CCM mpaka watie adabu.
 
Mtu mwenye akili zako timamu huwezi kuunga mkono uchafu wa kina Chenge na wenzake hata kama zimeluka mbili tatu kichwani, ule ni ujuha kabisa...!!!

Ninawashukuru viongozi wangu wa dini kwa kuliona hili kwani sauti ya yenu ni sauti ya Mungu. Tutalifanyia kazi.

BACK TANGANYIKA
 
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba amesema amefurahishwa na uamuzi wa Tamko la Maaskofu wa Makanisa yote nchini ya kuikataa Katiba Pendekezwa.

Jaji Warioba amesema ni ukweli ulio wazi kwamba maoni mengi watanzania waliyotoa yamepuuzwa kwenye Bunge la Katiba la Samwel Sitta na badala yake kuingizwa maoni ya watawala.

Jaji huyo mstaafu amesema Tamko la Maaskofu kuomba muda zaidi wa kusoma katiba pendekezwa kabla ya kura ya maoni ni muafaka kabisa hasa ikizingatiwa viongozi wa dini ndiyo wenye waumini.

Tayari leo Jumapili Makanisa yote ya Kikatoliki nchi nzima umesomwa waraka wa kinabii wa kuikataa katiba pendekezwa kwani imebeba maoni ya chama kimoja tu cha CCM.Na waraka umesisitiza katiba hiyo ilipatikana kwa njia ya HILA kubwa.

Mwaka jana Shura ya Maimamu wa dini ya Kiislamu ndiyo ilikuwa taasisi ya kwanza ya dini kuikataa katiba Pendekezwa na kuwataka Waislam wote kupiga kura ya HAPANA

Sio limesomwa katoliki tu hata huku kwetu KKKT tumesomewa na hatuwezi kwenda kinyume na tamko hlo.
 
ni kwel huko nakanisa yote ya roman imesomwa? ngoja niulizie

ni kweli imesomwa.na wamesisitiza kama serekali italazimisha huo mchakato wa kura basi wananchi wajitokeze kwa wingi kupiga kura ya HAPANA
 
Katiba pendekezwa ni kaburi letu kataa kwa nguvu Zote
 
Nimefurahi sana leo kisikia tamko hilo likisomwa na askofu Lebulu hapa Arusha hakika tutapata Tanzania yunayoitaka kwa waraka huu!
 
Back
Top Bottom