Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Mababa Askofu.
Nakuandikieni barua hii kuwaombeni kuwa msihadaike, msishawishike na wala msiingie msukumo wa kujibishana na masheikh wanaotoa matamko ya kuwashambulia. Hao masheikh wengi wanaowashambulia ni masheikh wa mfumo, wapo kimkakati, wapo kazini.
1. Kazi ya Masheikh hao ni kutumika kupoza waislamu ili serikali itawale bila misukosuko
Mababa maaskofu, bila shaka mnafahamu historia ya uanzishwaji BAKWATA, ni moja ya matunda ya akili nyingi za Julius Nyerere. Hata hivyo kama ambavyo mnajua Nyerere alisimika mambo mengi yaliyomsaidia kutawala kwa miaka 24, hata hivyo kadri siku zinavyokwenda tunatambua mambo mengi aliyoyaasisi yaliweza kufanya vyema kwa wakati ule kukiwa na ufinyu wa taarifa, ila sasa dunia imejaa taarifa na mabadiliko mengi na hivyo mambo mengi yanahitaji kubadilishwa, baadhi ya vitu alivyoviasisi Nyerere lakini baadae vikabadilishwa na uongozi uliofuata ni kama vile kuondoa azimio la arusha, kuleta vyama vingi, soko huria n.k. Baadhi ya vitu ambavyo havijabadilika ni kama Katiba ya mwaka 1977 na hizi taasisi za kimkakati kama vile BAKWATA. Na kwa kweli kwa mujibu wa nyakati hizi, taasisi hizi ni kikwazo mno katika kuleta uwajibikaji wa watu maana katika nyakati kadha wa kadha zinatumika kama mabeseni ya kubrainwash watu ili watawalike kiurahisi.
2. Lengo la Masheikh hawa wa "mfumo" ni kukoroga maji (muddy the waters) ili kuwavuruga watu wajigawe katika makundi ya dini zao
Kwa sasa dola iliyofanya mauaji ya halaiki iko kikaangoni, inalaumiwa kila kona, haina mtetezi wa maana. Isipokuwa sasa imeona kundi la kuvurugavuruga akili za watu ili wajigawe katika makundi yao ya kidini ni hili kundi la masheikh wa "kimkakati". Lengo la hawa masheikh ni kuwakera nyie maaskofu ili mjibishane nao halafu nchi igawanyike katika makundi ya dini zao halafu wauaji wa wananchi wasipigiwe kelele kwa mauaji yao. Msiwape nafasi hii, nyie waacheni wapige kelele zao lakini nyie endeleeni kutetea maslahi mapana ya umma.
3. Mnafahamu hawa masheikh wakubwa wa BAKWATA wapo kwenye payroll ya serikali, mnategemea nini kutoka kwao?
Mababa askofu mnafahamu vyema Sheikh Mkuu wa BAKWATA analipwa mshahara na serikali, ana ulinzi wa serikali na ana marupurupu kibao kutoka serikalini, Je mlitegemea BAKWATA na masheikh wake wamtumikie nani kama siyo kumtumikia anayewalipa?. Kwa hiyo hizo kelele za baadhi ya masheikh wa BAKWATA kelele zao ni katika kupigania kula zao. Kwa hiyo msiwashangae.
4. Hao Masheikh wanapuuzwa hata na waislamu wenzao kwa hiyo wasiwaumize vichwa
Mababa askofu, hao masheikh uadilifu wao kwa waislamu wenzao ni mdogo, wanadharauliwa kwa matendo yao ya kinafiki, wanauza mali za WAKFU za Waislamu, hawana vision ya maana ya kuwasaidia waislamu wenzao, huwezi kuwasikia wakikemea madhambi ya watawala kama vile rushwa, ubadhilifu, n.k. Sasa kama hawa hawana radhi ya waislamu wenzao, kwa nini nyie muumizwe kichwa nao?. Puuzeni mashambulizi yao.
5. Mababa askofu endeleeni kupigania haki kwa wote, hao masheikh wa BAKWATA hawajui walitendalo
Haki huinua Taifa, na Taifa lililoinuliwa ni kwa faida ya wote, hivyo basi msisite kupigania Taifa maana huu ni mtumbwi wa wote, ukizama tunazama wote. Hawa masheikh wanapigania maslahi mafupi sana ya muda mfupi, hata hivyo nyie endeleeni kupigania maslahi mapana ya Taifa hili. Nawapongezeni sana kwa kusimama kwenye kweli. Mmetetea wamasai, Mmepigania rasilimali za nchi hii kama vile bandari, mmepigania uchaguzi huru na haki n.k. Unfortunately ni kwamba hawa Masheikh wao hawana Interest ya kutetea haki za wananchi wao wanasimama na watawala tu nyakati zote.
6. Mababa Askofu nyie mna rekodi ya kutetea haki nyakati zote bila kujali rais ni mtawala wa dini gani.
Kipindi cha magufuli mlitoa nyaraka kadhaa za kulaani uminywaji wa demokrasia, za kupinga utekaji na hata jaribio la mauaji ya Tundu Lissu. Hawa Masheikh wa BAKWATA walikuwa kimya na badala yake walikuwa msitari wa mbele kwenye dhifa za kitaifa na kuzungumzia amani ili tu kuupoza umma, Leo mababa askofu mnatoa nyaraka za kukemea mambo hayohayo, hawa masheikh wa "kimkakati" wanaibuka na kuanza kuwashambulieni, muelewe tu hawa wapo kazini ili kutumia kete ya "WAGAWE UWATAWALE" kuwagawa wananchi wasiungane kuondoa udhalimu nchini
MWISHO.
Mimi nawapongeza sana mababa askofu kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kutetea haki za wananchi nchini, endeleeni hivyohivyo msirudi nyuma. Na chondechonde msijibazane na hawa masheikh wa "kimkakati" hao wapo kazini wanapigania kula yao.