Kwa mabachela wanaishindwa kupika wali. Tumia hesabu ndogo tu. Si lazima uwe na rice cooker. Kiasi cha maji ya kupikia mchele ukaiva ni mara mbili ya kiasi cha mchele unaotaka kuupika. Kama umepima kikombe kimoja cha mchele (level), basi pima maji kwa kikombe hicho au kingine chenye ujazo huo. Kumbuka kupunguza moto mchele unapokaribia kuiva.
Kumbuka, kuna grades mbalimbali za mchele. Utaratibu huu unaweza ukakataa kwa baadhi ya mchele. Ila, siyo kwamba hautaiva, unaweza kuwa boko kidogo au ukapungukiwa na maji kodogo. Soma mazingira haya halafu utaamua ama kuongeza au kupunguza maji kidogo.
Hakuna sababau ya kula tena wali bokoboko au ambao haujaiva vizuri.