Mabachela: Ni chakula gani kigumu kupika geto?

Maharage ukiondoka yanaungua au mkaa unaisha halafu unayakuta hayajiva.. Ukikaa kusubiri utaongeza mkaa mpaka unachukia huku ukijisahau kidogo yanaungua
 
sure,mkuu..dagaa,na..wali.nahitaji..sana,kujifunza.
msaada
Dagaa, ni kiasi upendacho kama unakula na vichwa au laa toa vichwa chambua vizuri,
Kisha (kupua) amabayo ni kuwakaanga kidogo wakavu hivyo hivyo,
Baada hapo tia maji acha kama daki 2 hivi wasafishe vizuri weka katika chombo kingine kisafi,
Chukua ndimu au limau kipande kamulia humo tulia hapo,
Chukua sufuria lako bandika jikoni tia mafuta yakipata moto,
Tia kitunguu chako ambacho ulishakata, kiiva kiasi weka dagaa wako tia chumvi,
Kaanga mpaka uone maji yako yamekauka angalia usiunguze si unajua gase,
Baada ya hapo nyanya yako uliokwisha anadaa tia mule funika muda kidogo,
Koroga vizuri hapo wewe kama watakauka sana ni wewe laa utaona hii mboga ipo tayari ruksa,
Then enjoy your food
 
Nashukuru sana mkuu, kama hutojali unaweza kunimalizia na wali.
 
Maharage ukiondoka yanaungua au mkaa unaisha halafu unayakuta hayajiva.. Ukikaa kusubiri utaongeza mkaa mpaka unachukia huku ukijisahau kidogo yanaungua
acha uongo mkuu
maharage ni kuchemsha tu
na kuongeza maji...kuunguza ni
uzembe wako...
 
MIMI SIPENDI HARUFU YA KITUNGUU INAYOBAKI KATIKA MIKONO
 
Back
Top Bottom