Tetesi: Mabadiliko Baraza la Mawaziri; J. Makamba, Mhagama, Ummy Mwalimu nje; Adadi Rajabu, Bashe watajwa

Adadi Rajabu mbunge wa Muheza ni mtu sahihi pale Mambo ya ndani ya nchi Magu usifanye kosa hata kidogo mchukue huyu mtu atakusaidia vizuri tu kwani wizara itakuwa chini ya majeshi kuanzia katibu mkuu na waziri wake.
 
teh teh teh

naona umejitahidi kuedit, ila bahati mbaya ukasau kuwa tayari watu walikuwa wamesha ku qoute kwenye original post
Ngoja na mimi nikusaidie kucheka mkuu, teh teh teh teheeeeee!!! Huyu jamaa amejivua nguo mchana kweupe, eti anajiona mjanja kumbe bonge la faraaa!! Eti tulivyolisakama ndo likakurupuka usingizini kwenda kuongeza "nimeota" Mods wasimwonee huruma huyu mbwiga lazima ashikishwe adabu!!
 
AGREY MWANRY bonge la striker, JPM sijui anamwona, atamsaidia sana, ni jembe haswa, Hana maskhara huyu mtu.
 
Ko mwanajeshi tena mstaafu ndo awe bosi wa polisi???!
Huoni kama itakuwa tatizo juu ya tatizo kwa Magu make wawili hawa(polisi v/s wanajeshi) hawalandani hata kidogo!!
 
Umesema mengi sana! Yanatosha. Tatizo ni huu mfumo wa local gvt. Ni sekta zote huko kwenye local govt. hazina connection na serikali kuu. Unawezaje kukuza elimu ya msingi inayosimamiwa na local govt? au kilimo? Sera ziko wizarani Dar. Mkoani hakuna msimamizi wa sera, halafu ukute Halmashauri ndo isimamie sera wakati unaelewa uwezo wa wataaamu wake uko chini.
 
Mtoa post hukumuelewa mwanzoni kabisa,yeye amesema Anaota! Kwahiyo muache aendelee kulala ili aote tena[emoji1] [emoji1]
 
Mods mpige ban ya miaka 100 huyu...!! Huu ni upuuzi..!!

Masele ni wa kumpa UWAZIRI..? Haya matusi kabisa..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…