Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Si bure, kuna mtu unampigia debe!Muda wowote mabadiliko makubwa yanategemea kutokea katika baraza la mawaziri ambapo mawaziri kadhaa watatemwa kutokana na sababu kadhaa.
1. Jenister Muhagama - Anatuhumiwa kwa kuzunguka mamlaka za teuzi (Rais na Waziri Mkuu) katika sakata la kumteuwa kaimu mkurugenzi wa NSSF... Mhagama alitenda kosa hilo akishirikiana na Balozi Ombeni Sefue ambaye kwa sasa kashatumbuliwa.
2. January Makamba - Maranyingi amesikika na kurekodiwa akimsema vibaya Rais, akimsengenya Rais pamoja na kuratibu mipango mbalimbali ya kumdhoofisha Rais Magufuli. haya anayatenda katika Hotel ya Protea Dar es Salaa., na Dodoma ambapo amekuwa akifanya vikao vya siri usiku wa manane na baadhi ya wabunge wa upinzani, pamoja na wafanyabiashara wakubwa wakiwemo wa sukari
3. Ummy Mwalimu - Inasemekana kasi na uwezo wake mdogo haumrithishi Rais kwa sasa..
Katika mabadiliko hayo Adadi Rajabu, Mbunge wa Muheza inasemekana anaweza kuingia kuchukua nafasi ya Kitwanga, wengine wanaotajwa ni Bashe, mbunge wa Nzega ambaye anaweza kupewa docket ya Mazingira au Maliasili na pia Serukamba amekuwa akitajwa.
Mytake: wananchi kwa umoja wetu tumuunge mkono Rais Magufuli ana dhamira njema kabisa la kuwatumikia watanzania.
Hao maskini milioni 12 wameupata kuanzia lini? unahusishaje na utawala uliyoko madarakani kwa miezi hii 7?Duuh hii panga pangua hadi hii half time timu haijafunga goli. WB inasema wananchi milioni kumi na mbili ni masikini hoe hae... Ngoja tuendelee kujipa moyo...
Kweli jf ni kiboko, nakumbuka kuna member alikuja humu akasema aliyekuwa naibu katibu mkuu wa UN ,MIGIRO wakati wowote anatangazwa kuwa balozi uingereza,na kweli mda mfupo ikatangazawa hivyo. Yani huko ikulu hakuna siri
Ila kuna jembe moja analisahu, huyu dogo anaitwa Masele (MP shinyanga), ataendana na kasi ya NgoshaNasubiri breaking news
Ummy hata mimi ningemteuwa bila sababu yoyote ya msingiHata mimi bado nashangaa kilichomsukuma Pombe kumtuea Ummy.
mkuu kwa nini usifiche ujinga wakoKwa hiyo ni kifungu kipi unafikiri kitabadili mfumo?? Kero yako ni nini unayodhani itatatuliwa na katiba mpya?? Au umekariri tu kuwa tunahitaji katiba mpya??
mkuu nafahamu namjibu huyu anayejifanya hamjui masele kwe jukwaa la siasaHapa tunamzungumzia masele ambaye ni mbunge wa shinyanga huko
Kabisa.... Kaonyesha uwezo mkubwa
Acheni kukariri, sio mnasema katiba mpya ila hamjui mnachokitaka!!mkuu kwa nini usifiche ujinga wako
sema wanaccm ,.usiwajumlishe wananchi wote wengine hatumuungi mkono kwakuwa mapendekezo yetu jp hayatumii mfano,.kumteua muhongo huku ni muhusika wa escrow,.mwakyembe nkMytake: wananchi
mkuu yaani kwa mtu mwenye akili timamu,.ccm siyakushabikia kabisaaaaaAliyafanya kikwete haya, alibadilisha mawaziri kila uchao lakini hakupata mavuno yaliyo bora, ccm ni ileile hakuna anae faa huko ndani. Bora angebaki mwenyewe na waziri mkuu makini zaidi. Tena kwenye listi angeongezwa Mwakyembe aliekuwa anacheka kama juha wakati waziri mlevi akitoa majibu ni aibu kubwa kama waziri wa sheria apishe tu na yeye.