SoC03 Mabadiliko katika imani kwa vijana

SoC03 Mabadiliko katika imani kwa vijana

Stories of Change - 2023 Competition

pescop bin lucky

New Member
Joined
Jul 1, 2023
Posts
2
Reaction score
2
STORY OF CHANGE

Katika maada yangu ya mabadiliko mimi napenda kuzungumzia suala zima la iman,kuwa na imani na viongozi tuliowachagua/ wanao tuongoza ni jambo lingine lakini suala zima la iman nalielekezea katika dini, Mungu ndie kiongozi wetu mkuu na ni mfalme wa aman tukimuamini yeye yote yanawezekana, lakini sasa vijana wa siku hizi walio wengi hawawazi kuhusu imani ama tuseme wanapuuzia suala la imani katika dini na kujikita katika kutafuta pesa wazipate watumie katika starehe

, na hata midomo yao imekuwa michafu kuzungumza matusi na lile janga la ushoga vijana hupenda kulizungumzia katika kugombana kwao, wengi wao hata wanadiliki kuto amini kama Mungu yupo eti tu kwasababu hawamuoni mi niseme tu hata kama msomaji huamini kama Mungu yupo najua unajua kuwa kuna nguvu flani inayokuweka hai, kuna nguvu flani iliyo chanzo cha uhai, kuna nguvu flani iliyo chanzo cha vitu vyote nayo hiyo nguvu iliyo ya kimiujiza ndio tuna iita Mungu basi nazo hizo nguvu ndizo nguvu za ki Mungu,

ewe mwana sayansi usiye amini uwepo wa Mungu kwasababu hakuna nazalia inayo thibitisha uwepo wake je kwanini unaiamini pumzi(hewa) usiyo iona unaamua kuivuta mpaka ndani ya mapafu na kuitoa ile inayo aminika kuwa haifai na je kwanini unaendelea kuivuta asubuhi, mchana na hata ukiwa usingizini kama sio uweza wa nguvu za kimiujiza ambazo naweza sema ni nguvu za ki Mungu, hivyo basi niseme ili kuibadilisha Tanzania yetu na hata dunia kwa ujumla inabidi tuwe na imani na uwepo wa Mungu naye ndie muumba wa vyote na hata njia zote zipo kwake, tukiwa na kiongozi mcha Mungu lazima tutaongozwa katika njia za kweli na kufikia malengo yetu.Ahsante.
 
Upvote 2
Back
Top Bottom