Mabadiliko makubwa ya viongozi wa serikali yakamilika; yatawagusa pia viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama

Mabadiliko makubwa ya viongozi wa serikali yakamilika; yatawagusa pia viongozi wa vyombo vya ulinzi na usalama

Nitamuona wa maana akijiuzuru yeye na Majaliwa, huku akiacha amewafuta kazi Nape, Mwigulu na Wambura. Hawa kina msukuma tutadili nao huku Nkome wenyewe.
 
Mkuu hongera na shukrani kwa mchango wako mzuri.

Ni vizuri kwamba Bunge lingetumika kuchuja watendaji wa baadhi ya taasisi, lakini pia ili tuwe na imani na bunge, ni vyema utaratibu wa kuwapata wagombea ubunge pia ubadilike.

Kwa mchakato uliopo wa upatikanaji wa Wabunge, ni sahihi mtu kusema kuwa wananchi tunawapigia kura wawakilishi na chaguo la chama badala ya kupigia kura machaguo au mapendekezo yetu. Haiwezekani mtu wa Mchambawima na Geita wakakae kamati kuu ya chama X waamue ni nani miongoni mwa watia nia ya ubunge anafaa kugombea jimbo la Ngorongoro.

Tuache Wana-Ngorongoro waamue nani awe mgombea wao maana wao ndo wanajua watu wao na si kamati kuu ya chama. Hii itaepusha kupeleka bungeni wabunge ambao si wawakilishi wa wananchi.

Hakika yapo mambo mengi ya kubadilisha nchi hii.
Mkuu hoja yangu ni rahisi kabisa na inaweza kutekelezeka.

Mwanzoni kabisa nimesema tukitaka kulikomboa hili taifa ni lazima serikali zigawanyika katika nyanja mbili zinazojitegemea lakini zinashirikiana. Serikali Kuu (Central Government) na Serikali za mitaa (Local Government). Tukiweza kufanya jambo kama hili tutakuwa tumesaidia wananchi kwenye mambo mengi sana. Serikali za mitaa zikiwa zinajiendesha (Fully Autonomous) kwenye baadhi ya mambo basi ushirikishi wa wananchi utakuwa mkubwa sana.

Siyo lazima kila kitu kipelekwe kwenye bunge ambalo kiuhalisia lina watu wasiofahamu baadhi ya mambo. Kama ulivyosema mtu wa Mchambawina anashughulika na mambo ya mtu wa Ngorongoro. Binafsi naamini baadhi ya vitega uchumi na mapato vinaweza vikaachwa kwenye serikali za mitaa huku serikali kuu ikiwa inachukua asilimia kadhaa. Tunaweza kufanya kwamba asilimia 35% kwa Serikali za mitaa, na asilimia 75% kwa Serikali kuu.

Binafsi wizara ya TAMISEMI naona ingefutwa na kiundwe chombo maalumu cha kikatiba au baraza la uratibu linalojitegemea (Fully Autonomous), ambalo litafanya kazi za utekelezaji wa sera, sheria na usimamizi wa taasisi za Serikali za mitaa. Baraza hili liwe na wawakilishi ndani ya bunge ambao watakuwa ni wabunge, pia liwe na mwakilishi ndani ya baraza la mawaziri. Nasema hivi kwasababu kuna jambo ambalo wengi wanalitaka sana ila wanaogope endapo likitokea muungano utavunjika: Jambo la Tanganyika.

Mimi naoni yangu ni haya: Kama dola la Tanganyika na Serikali yake haviwezi kutengenezwa katika ngazi ya serikali kuu au serikali za shirikisho, kwa hofu ya kuwagawa watanzania na kuvunjika muungano. Basi nashauri tuitengeneze Tanganyika katika ngazi ya Serikali za mitaa (Local Governments). Tanganyika itakuwa ina maeneo/majimbo huru yanayojitegemea kiuchumi (Economic Municipalities or Economic Counties) bila kuwepo kwa serikali yake kuu, wala bunge lake, wala Raisi, jambo ambalo litazua taharuki.

Hili baraza la Uratibu ambalo nimelipendekeza, mbali na kusimamia utekelezaji wa sera na sheria, pia litakuwa na ofisi ya maalumu ya Tanganyika, ambayo kazi yake itakuwa ni kusimamia tu utekelezwaji wa sera za kiuchumi kwenye maeneo/majimbo huru ya Tanganyika. Hivyo hata wawakilishi ambao watakwenda bungeni watakuwa ni wabunge wa Tanganyika, lakini pia hata waziri atakayepelekwa kwenye baraza atakuwa Ex-Officio Ministerial Representative of Tanganyika. Tukifanya haya tutapata faida zifuatazo:

1. Tutapunguza urasimu mkubwa uliopo nchini.
2. Tutaweza kudhibiti na kuona mianya mingi ya rushwa.
3. Tutalidhibiti bunge la jamhuri linapofanya uzembe (Kumbuka hizi serikali zitakuwa huru kabisa)
4. Tutapunguza idadi ya wabunge wengi wasio na lazima maana serikali zinajiendesha zenyewe.
5. Tutaongeza ufanisi mkubwa katika utekelezaji wa sera kuanzia ngazi za kaya, vijiji na mitaaa.
6. Tutaimarisha sana ulinzi na usalama, maana serikali za mitaa zitarudishiwa nguvu za usimamizi.

Binafsi naamini, tunaweza kuitengeneza Tanganyika ndani ya muundo huu-huu wa serikali mbili, japo siyo katika ngazi ya shirikisho (At a Federation Level) bali katika ngazi ya Serikali za mitaa (Local Governments), kupitia maeneo/majimbo huru ya kiuchumi ambayo yanajiendesha bila kuingiliwa na bunge wala serikali kuu. Huku yakiwa na baadhi ya wawakilishi ndani ya bunge na baraza la mawaziri.

Wawakilishi ambao watakuwa ni wabunge watateuliwa na majimbo yote, ilhali mawaziri (Ex-Officio Ministerial Representatives) watachaguliwa kutoka kwa watendaji wenye uwezo ndani ya baraza la Uratibu au kutoka kwa kwenye orodha ya wakuu wa maeneo/majimbo huru ya kiuchumi. Lengo hapa ni kwamba kama mawaziri wawakilishi ambao wanaingia kwenye baraza la mawaziri, watachaguliwa moja kwa moja na watu wote kama wabunge , basi dhana ya kwamba huyo waziri ataanza kujiita Raisi wa Tanganyika itazaliwa taratibu. Hivyo ataueliwe kutoka kwa watendaji au viongozi wa majimbo, huku muda wake (Office Tenure) ukiwa ni miaka 3, ambapo anaweza kuteuliwa tena.

NB: Naamini hili linawezekana vizuri tu kikatiba, tukiendelea kulimbikiza nguvu zote kwenye serikali kuu na bunge, tutaendelea kusalitiwa na kuuzwa bila sababu za msingi. Tena matatizo yetu yatakuwa mikononi kwa watu wasio na uelewa mpana kuhusu mambo halisi ya wananchi. Tubadilike.
 
Wakiniteua Mimi tutapiga hatua kubwa mno,sitaruhusu upuuzi upuuzi hata kidogo,nafaa kuwa mshauri wa rais,na shu shu shu.👵
 
Mama apitishe fagio la chuma
Sidhani kama ataweza. Maana wanao mzunguka wamekuwa chawa. Hawampi ushauri wa maana.
Kama Mama angekuwa na maamuzi yake mwenyewe ninge shauri aachane na walio kuwa karibu na JPM. Kuna walioko karibu na Mama lakini wana furahia anguko lake
 
Sidhani kama ataweza. Maana wanao mzunguka wamekuwa chawa. Hawampi ushauri wa maana.
Kama Mama angekuwa na maamuzi yake mwenyewe ninge shauri aachane na walio kuwa karibu na JPM. Kuna walioko karibu na Mama lakini wana furahia anguko lake
Kuna nyuzi nimeiona humu kuhusu mabadiliko makubwa yaja kuanzia top to bottom

Ila sisi Wapinzani na Wananchi kwa ujumla tunauliza mbona maridhiano ya kisiasa na mchakato wa KATIBA MPYA unapelekwa very slow?
 
Kuna nyuzi nimeiona humu kuhusu mabadiliko makubwa yaja kuanzia top to bottom

Ila sisi Wapinzani na Wananchi kwa ujumla tunauliza mbona maridhiano ya kisiasa na mchakato wa KATIBA MPYA unapelekwa very slow?
Wanufaika wa mgogoro uliopo kati ya upinzani na Ccm hawataki hayo maridhiano. Mmoja wao ni msajili wa vyama vya siasa na msaidizi wake.
Anajua suluhu ikifikiwa na yeye hana kazi
 
Wanufaika wa mgogoro uliopo kati ya upinzani na Ccm hawataki hayo maridhiano. Mmoja wao ni msajili wa vyama vya siasa na msaidizi wake.
Anajua suluhu ikifikiwa na yeye hana kazi
Basi sisi kama CHADEMA tuchague Plan B kuiwekea hii Katiba ya 77 ya chama kimoja viraka haswa ili tupate Tume HURU ya UCHAGUZI ili tuingie kwenye UCHAGUZI 2025 halafu mchakato wa KATIBA MPYA uendelee baada ya UCHAGUZI mkuu
 
Kuna wakati huwa nakasirishwa sana na jinsi mambo ambavyo Raisi Samia aliamua kuendesha nchi, ili kuna mahali huwa nakifiri huwa namuonea sana huruma. Amekumbatia wapambe ambao tangu mwanzoni hakutakiwa kabisa kuwarudisha ofisini, kwasababu mbali na kuondolewa na Raisi Magufuli ukweli ni kwamba walikuwa na makandokando makubwa. Katika ngazi ya kiutendaji ndani ya Baraza la Mawaziri, kwenye hili sakata la Bandari Raisi ameachwa peke yake.

Ila kundi baya zaidi ni wale ambao wanamuunga mkono kwa maslahi binafsi, kama fedha, uzanzibari na dini. Bahati mbaya hili ndilo kundi ambalo sauti yake inasikika zaidi kuliko hata lile kundi ambalo linamuunga mkono kutokana na sera za kichama au utendaji wake. Kiufupi, hili kundi ndilo linazidi kumwaga chumvi kwenye kidonda kadiri ya siku zinavyoenda.

Mbinu ambazo hili kundi linazitumia ni zile za Tu QuoQue Fallacy za kusema, kama ninyi mlifanya kwanini Raisi Samia asifanye. AU Kama ninyi mlikosea kwanini Raisi Samia naye asikosee. Kiufupi limemponza sana mama wa watu. Yote tisa, mbali na kufanya mabadiliko makubwa ya kiuongozi inabidi mfumo mzima ufumuliwe. Itakuwa ngumu, lakini kama ana nia njema ya kulisaidia hilo taifa itabidi afanye hivyo.

Kiongozi wa Ufaransa na Baba wa Umoja wa Ulaya,
Jean Monnet aliwahi kusema hivi "If you want things to work, you need to people. But if you want things to last then you need institutions".

Uzembe mwingi, rushwa na urasimu mkubwa ambao unaendelea nchini Tanzania, chanzo kikubwa ni kuendelea kutumia mifumo, falsafa na miundo ya kitaasisi ya karne iliyopita ilhali tuko ndani ya karne mpya. Nchi imekuwa kubwa sana ila mifumo haikui wala sera hazibadiliki kuweza kukidhi mahitaji mapya ya kimfumo. Hivyo basi ili mambo yafanikiwe ni lazima:

Mosi, muundo wa muungano uangaliwe upya. Hata kama hatutakuwa na Serikali tatu, basi ni lazima tupunguze nguvu kutoka serikali kuu (Central Government) na kuzipeleka chini kwa serikali za mitaa (Local Government) ambazo zitakuwa huru kwenye baadhi ya mambo. Muhimu ni kwamba watanganyika wanachokitaka ni ile hali ya wao kuwa na maamuzi kwenye baadhi ya rasilimali zao.

Pili, sheria za usimamizi na matumizi ya rasilimali ziwekwe bayana na zianze kusimamiwa kuanzia ngazi za serikali za mitaa na maamuzi mengine yafanyike huko bila kuliachia kila kitu bunge ambalo limejaa wala rushwa wasiokuwa na ufahamu wala uchungu na watu.

Tatu, mawaziri wa wizara nyeti kama Elimu, Nishati, Ulinzi, Mambo ya Nje na Mwanasheria Mkuu lazima wachaguliwe na Raisi na kuidhinishwa na Bunge. Hii tabia ya uswahiba na undugu ndiyo inatuletea hizi changamoto zinazoendelea. Kama Waziri Mkuu anapitishwa na Bunge lote, nini kinazuia mawaziri wengine wasipitishwe na Bunge, ??

Nne, wakuu wa vyombo vya usalama ni lazima nao wapitishwe na bunge na uzoefu wao ndani ya taasisi uwekwe wazi. Wametumikia taasisi husika kwa muda gani na katika nafasi zipi, ni mambo ambayo hayatakiwi kufichwa kabisa. Hata kama hatutazungumzia utendaji wa taasisi kwa undani, basi walau haya mambo ni lazima yawekwe bayana. Tabia ya kufanyia mambo gizani ndiyo yanajenga mazingira ya uzembe, rushwa na uvunjifu mkubwa wa sheria.

NB: Raisi akishafahamu kwamba wateule wake ni lazima watapitishwa na bunge, basi sidhani kama atateua watu kiholele tu. Tena hata ile tengua-tengua isiyo na kichwa wala miguu itapungua. Nafasi za Majaji, Mawaziri na Wakuu wa vyombo vya usalama ni lazima ziangaliwe upya na kurekebishwa ndani ya katiba ili tuondokane na hili jinamizi linaloendelea sasa. Unajiuliza mpaka dude la DP-World linapita hivi hakuna hata mmoja aliyesanua mchongo kweli,?

Bonge ya ushauri,ila kwa watawala hawa waliogeuka wezi wataona kama unataka kuwaharibia dili.
 
Kuna nyuzi nimeiona humu kuhusu mabadiliko makubwa yaja kuanzia top to bottom

Ila sisi Wapinzani na Wananchi kwa ujumla tunauliza mbona maridhiano ya kisiasa na mchakato wa KATIBA MPYA unapelekwa very slow?

Tunasema ‘top down or bottom up’ siyo top to bottom! Wakikusikia wajukuu wa malkia watakupa cha mtema kuni!
 
Mkuu inaonekana una imani na bunge. Kama wabunge wanapatikana kwa maagizo ya rais unategemea kuwa na bunge la kufanya maamuzi sahihi? Mfano hili suala la bandari umeona bunge likifanya lolote nje ya utashi wa rais?
Tunahitaji, nafikiri, nje ya mambo mengi mengine;
  • mbunge kuwa mwakilishi wa kweli wa wanajimbo wake, kwa kupitia chama cha siasa au binafsi
  • wanajimbo waweze kisheria kumvua ubunge mbunge wao kabla ya uchaguzi
  • raisi asiruhusiwe kuwa na majukumu mengine yoyote nje ya majukumu ya raisi kikatiba, e.g asiwe kiongozi wa shirika au chama chochote.
 
Back
Top Bottom