Dini zote itabidi zisajiliwe upya na cheti cha Usajili kitakuwa cha miaka 5 tu kisha Dini zisajiliwe upya. Masharti Mengine ni pamoja na kupeleka kwa msajili ripoti ya mapato na matumizi ya pesa za sadaka kwa kipindi cha miaka mitano nyuma.
Watakaoshindwa kutoa ripoti hizo kwa kigezo pesa wamenunua ndege binafsi au magari na majumba watafutiwa Usajili.
JE DINI YAKO ITAPITA VIGEZO NA MASHARTI YA SERIKALI?
Au tutashuhudia makanisa mengi kwenda underground waabudu bila Usajili? Unaona Serikali wangefanya nini badala ya kuja na masharti Makali? Ukisema ni kwa sababu rais ni muislamu, utaambiwa hata misikiti itapaswa kufuata
hayo hayo.
IFUATAYO NI TAARIFA RASMI YA SERIKALI.ISOME KWA MAKINI
UELEWE
.Serikali imefanya mabadiliko ya usajili wa taasisi za kidini na Jumuiya mbalimbali kutoka kuwa wa kudumu na kuwa wa muda. Katika mabadiliko hayo taasisi zote za dini zilizosajiliwa (yakiwemo makanisa) zitalazimika kuhuisha (renew) usajili wake kila baada ya miaka mitano. Taarifaya serikali ya mwaka 2020 inaonesha jumla ya taasisi za kidini zilizosajiliwa nchini ni 36,000 zikihusisha Makanisa, Misikiti na jumuiya zake.
Ofisi ya Msajili wa taasisi za kidini na Jumuiya za kijamii imetoa taarifa ya kuanza uhakiki wa Jumuiya hizo kuanzia August 24 hadi November 30 katika mikoa mbalimbali, na kila taasisi itatakiwa kulipa TZS 100,000/= ya uhakiki. Hivyo basi serikali inatarajia kukusanya 3.6Bilioni ikiwa taaisi zote zitafanya uhakiki.
Miongoni mwa matakwa ya uhakiki ni taarifa ya fedha pamoja na taarifa ya mabadiliko ya uongozi katika taasisi na jumuiya hizo. Taasisi itakayoshindwa kukamilisha uhakiki kwa kipindi kilichowekwa itafutwa.
Yamekuwepo maoni kinzani kuhusu mabadiliko haya, baadhi wakiunga mkono na wengine wakipinga.Mmoja wa wanahabari wakongwe nchini amesema "Kuna makanisa tangu yameanzishwa hayajawahi kubadilishwa uongozi. Askofu ni huyohuoyo tangu mtoto anazaliwa hadi anaoa au kuolewa. Wala taarifa za fedha za kanisa hazipo wazi kwa waumini wake wao wanatoa tu na hawatakiwi kuhoji matumizi, kwahiyo ni muhimu serikali kufuatilia
"Mchungaji Alex Mwaipaja amesema "sidhani kama ni sahihi serikali kudhibiti imani za watu. Kanisa halipo kwenye nyaraka za serikali. Tukikaa nyumbani na familia na kumuabudu Mungu katika roho na kweli hilo ni kanisa hata kama hatuna usajili. Halafu kwanini serikali inakerwa na wingi wa makanisa, haikerwi na wingi wa bar au guest house?"Nini maoni yako? Unadhani ni sahihi serikali kufanya uhakiki wa taasisi za kidini? Je ni sahihi kupewa usajili wa miaka mitano badala ya usajili wa kudumu kama ilivyokua awali? Unaonaje Taasisi kutakiwa kufanya mabadiliko ya uongozi badala ya kuwa na kiongozi mmoja kwa muda mrefu? Ikiwa baadhi ya taasisi zitafutiwa usajili, je mabadiliko haya yataathiri imani za watu kwa kiasi gani?