Mabadiliko: Taasisi za Kidini sasa Kusajiliwa kila baada ya Miaka 5 kwa Malipo ya Tsh 100,000

Mabadiliko: Taasisi za Kidini sasa Kusajiliwa kila baada ya Miaka 5 kwa Malipo ya Tsh 100,000

Serikali imesema imefanya marekebisho ya kanuni kuhusu taasisi za dini hasa makanisa na misikiti amabyo yatalazimika kuomba usajili kila baada ya miaka mitano tofauti na ilivyokuwa zamani ambapo usajili wa taasisi hizi hasa dini na misikiti na vyama vingine vya kijamii hupewa usajili wa kudumu.

Serikali imesema kuwa inataka kuweka kanuni ambapo mapato na matumizi ya taasisi za dini yatakaguliwa.

Pia imesema kuwa kuna viongozi wa dini wana fanya kinyume na usajili wao na wengine wanatumia nyumba zao za ibada kufanya siasa.

Hivyo kila baada ya miaka mitano watatakiwa kuomba upya na kama watakuwa na vigezo ndio watapewa usajili na kibali cha kuendelea na taasisi zao au makanisa.

My take:
Gwajima , Bagonza na wenzao wajipange
 
Wawe wanaomba kila mwaka kupunguza wachungaji njaa


USSR
 
Ni Jambo jema maana pia waliokuwa hawajasajiliwa watakuwa ni wengi sana, pia viwango vya nyumba za ibada viwekwe siyo mchana ibada na usiku bar, mabango na utambulisho wa eneo uwe ni lazima.
 
Vibali vya huduma za kiriho hutoa Mungu.Hii kauli ni chembechembe za siasa kuwafunga kutokuwa na WARAKA WA MAASKOFU.
Madhara yakunyamazisha kila kundi la kijamii litakuwa na chuki na madhara makubwa sana
 
Wanawaita Wafuasi wao Kondoo na wanawachukulia kama Kondoo kweli...hivyo serikali ikikaa karibu ni kwa faida ya Kondoo (Waamini) ambao hawaoni hawasikii kwa hawa Viongozi wao..kila wanachoambiwa wao ni sawa tu.
 
Salaam Wakuu,

Wizara ya mambo imefanya mabadiliko katika usajili wa Taasisi za Kidini kutoka wa Kudumu na kuwa wa Miaka 5. Lengo ni kutathimini Jumuiya zilizo hai na kuhakiki kama zinatii Masharti ya Usajili. Taasisi hizo zitatakiwa kulipia laki moja.

View attachment 1887885View attachment 1887886
Kuna mtu anatafutwa hapo

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Salaam Wakuu,

Wizara ya mambo imefanya mabadiliko katika usajili wa Taasisi za Kidini kutoka wa Kudumu na kuwa wa Miaka 5. Lengo ni kutathimini Jumuiya zilizo hai na kuhakiki kama zinatii Masharti ya Usajili. Taasisi hizo zitatakiwa kulipia laki moja.

View attachment 1887885View attachment 1887886
Ilianza salama NAWASALIMIA KWA JINA LA JAMHURI YA MUUNGANO.... KAZI IENDELEE.

Ikaja MBOWE GAIDI......... mapichapicha, na hukumu ya Mbowe ikasomwa kwenye BBC Swahili TV.

Sasa ameshika waya mwekundu wa TANESCO, Mungu hata siku moja haachi ufalme wake uchezewe, litakalo tokea tusilaumiane, MUNGU ALIFANYA KA FARAO, time will tell.
 
Hiki kitu kitaongeza nidhamu kwenye baadhi ya nyumba za Ibada, ambazo hazitaki kufauata utaratibu sahihi unaotakiwa kufuatwa Makanisani, kwamba wasiofuata utaratibu wakiendelea ku-misbehave the next registration wananyimwa. Wewe unakuta nyumba ya Ibada haina hata lile bango linaloonyesha ratiba ya vipindi kwa wiki, ratiba ipo kichwani kwa Mchungaji utafikiri kanisa ni lake wakati linamilikiwa na taasisi.
Naomba kukiri kuwaponngeza sana Wizara ya Mambo ya ndani katika hili pia. Zaidi nawashauri waweke na kanuni nyingine ya ziada kwenye usajili huo kwamba: Nyumba ya Ibada lazima iwe na Bango nje linaloonyesha ratiba ya vipindi kwa muda wa wiki nzima, na kwamba ratiba hiyo lazima ifuatwe.
Ibada sio lazima ziwe na ratiba rasmi. Huwezi kuwapangia watu muda na namna ya kuwasiliana na Muumba wao.Ratiba ni za wanasiasa.
 
Kule mbeya Kuna kanisa viongozi wake walipigana ngumi sababu ni mapato ya kanisa!

Nini maoni yako?
Kwa nini hukushangazwa na yule mbunge aliyemkong'ota mwenzake rungu kwa kisa cha kutaka kugombea "jimboni kwake"!
 
Back
Top Bottom