Mabadiliko TRA: Kamishna wa Forodha Mtanganyika Said Athuman Kiondo aondolewa awekwa Juma Bakari Hassan kutoka Zanzibar

HUYU MAMA ASIPOSHTUKIWA MAPEMA MAMBO YATAHARIBIKA SANA HUKU TANZANIA BARA. INAONEKANA HATAKI MCHEZO KTK MIAKA HII TISA ATAKAYOKUWA KITINI. INAONEKANA HATAKI KURUDIA MAKOSA ALIYOFANYA BABA YAKE ALI YA KUCHEZEA FURSA KWA AJILI YA WAZANZIBAR. MZEE ALI ANGEFANYA SEMA MZEE JULIUS ALIKUWA HAI KIPINDI KILE HIVYO ALIKUWA AKIDHIBITIWA; LAKINI BADO ALIFANYA UFISADI TUU UNAOFANANA NA HUU. MFANO, KUUZA WANYAMA HAI KWA WAARABU.
JAMBO AMBALO THE SO CALLED WATANGANYIKA WANALOJIFANYA HAMNAZO NI KUWA, ... WAZANZIBAR HAWATAKI KABISA KUWA KTK MUUNGANO. WALILAZIMISHWA NA WANAENDELEA KULAZIMISHWA. WAZANZIBAR (AKIWEMO MAMA, HUSSEIN, AND THE LIKE) WANAJUA MUUNGANO UMEFIKIA MWISHO WAKE, HIVYO, WANAFANYA MAANDALIZI KABAMBE KUHAKIKISHA "WANATUMIA FURSA" KUIANDAA ZANZIBAR KUKABILIANA NA ATHARI ZOTE ZITAKAZOJITOKEZA ZITOKANAZO NA ZANZIBAR KUWA PEKE YAKE. NI ILE TU VIJANA WETU WA USALAMA WA TAIFA (WATANGANYIKA) UZALENDO MDOGO, LAITI WANGEFUATILIA KWA MAKINI MAMBO YANAYOENDELEA KATI YA HAWA NDUGU ZETU WA ZANZIBAR NA WAARABU WA HUKO FALME ZA KIARABU NA OMAN, WANGEGUNDUA MAMBO MENGI SANA. WAARABU WANAAMINI VISIWA VYA ZANZIBAR NI MALI YAO. WATU HAWA WANAUNGANISHWA PIA NA IMANI YA KIDINI (ISLAMU) NA HATA UNDUGU WA DAMU KWANI WAMEJICHANGANYA. WAZANZIBAR WEENGI WANA UHUSIANO WA DAMU NA WAARABU WA HUKO UARABUNI. HAIYUMKINIKI, WAWEZA MKUTA NA MAMA IKO HIVYO UKIFUATILIA MNYORORO WA NASABA YA UKOO WAKE. NI HATARI.
MAMBO HAYA NAAMINI YATAKAJA KUWA NA ATHARI MBAYA MNO KWA THE SO CALLED "TANGANYIKA" IN FUTURE.
MAMBO YA MZEE JULIUS AMBAYO HAYANA UZITO TENA HAYAFAI KUENDELEA KUFUATWA. KWA MFANO, SIASA ZA UJAMAA NA KUJITEGEMEA, MUUNGANO, MBIO ZA MWENGE, AND THE LIKE; ATI KWA KUMUENZI TU. HAPANA. HATA HILI LA KUHAMISHA MAKAO MAKUU HALIKUPASWA KUFANYWA SASA. TULIKWISHACHELEWA. LILITAKIWA KIPINDI KILE KILE MZEE JULIUS AMEAGIZA.
NAWASIKITIKIA SANA VIJANA WA THE SO CALLED "TANGANYIKA". WANAWAZA SIMBA NA YANGA TU! HATA VIJANA WALIOHITIMU NA WANAOHITIMU SHAHADA KWENYE LEVELS MBALIMBALI. NI HAYO HAYO. WATAKUJA SHTUKA MAMBO YAMEHARIBIKA KABISA. HAPO NDIPO WATAJITIA KUINGIA BARABARANI AU MSITUNI; TOO LATE!
VIJANA AMKENI, NO LONGER AT EASY!
 
Kuwalaumu marehemu hakutasaidia chochote. Sisi tulio hai ndiyo wenye wajibu wa kurekebisha makosa yao.

Muungano una mapungufu. Mabadiliko hayakwepeki.
 
Kama
Kama Tanganyika haipo Watanganyika wametokea wapi?
Rais wa Tanganyika ni nani?
Na Bunge la Tanganyika liko wapi?! Na mkuu wa majeshi wa Tanganyika ni nani?! Hakuna watanganyika Bali Kuna wachaga,wamakonde, wasukuma, Wahaya, wamasai nk. Bila Tanganyika hakuna watanganyika.
 
Rais wa Tanganyika ni nani?
Na Bunge la Tanganyika liko wapi?! Na mkuu wa majeshi wa Tanganyika ni nani?! Hakuna watanganyika Bali Kuna wachaga,wamakonde, wasukuma, Wahaya, wamasai nk. Bila Tanganyika hakuna watanganyika.
Kabla sijakujibu, nikuulize kwanza! Wewe ni Mtanganyika au Mzanzibar?
 
Kuwalaumu marehemu hakutasaidia chochote. Sisi tulio hai ndiyo wenye wajibu wa kurekebisha makosa yao.

Muungano una mapungufu. Mabadiliko hayakwepeki.
Lakini kumlaumu Samia pia hatumtendei haki kwakuwa yeye anafanya mambo aliyokuta yameshaandikwa na kusainiwa yeye anatekeleza tu. Yeye Samia siye aliyepanga mambo ya muungano na ambayo siyo ya muungano.
 
Kabla sijakujibu, nikuulize kwanza! Wewe ni Mtanganyika au Mzanzibar?
Mimi siyo mtanganyika Wala siyo mzanzibari.
Mimi ni mtanzania. Kwetu ni mkoa wa Kagera. Zanzibar nimewahi tembelea mara Moja tu mwaka 2017 nikakaa siku tatu nikarudi zangu nyumbani na sijapata nafasi ya kwenda huko tena.
 
Na kwa mantiki hiyo mnyaturu asiruhusiwe kuhiji kwenye kaburi la msukuma🤣🤣🤣
 
Mimi siyo mtanganyika Wala siyo mzanzibari.
Mimi ni mtanzania. Kwetu ni mkoa wa Kagera. Zanzibar nimewahi tembelea mara Moja tu mwaka 2017 nikakaa siku tatu nikarudi zangu nyumbani na sijapata nafasi ya kwenda huko tena.
Asante sana mkuu. Nimefurahi kulisoma neno Tanganyika. Tanganyika ni nchi nzuri sana.

Hata wewe umekubali kuwa kuna Tanganyika ila umechagua kutokujitanabaisha nayo, uamuzi ambao ni sahihi pia kama nami nilivyochagua kutokuikana Tanganyika. Naipenda Tanganyika.

Kwa sababu nilisema nitakujibu, acha nitimize ahadi yangu.

Ni hivi mkuu, inavyosemekana, Rais wa Tanganyika ni Kassim Majaliwa. Ndivyo inavyosemekana, ila naomba usinihoji zaidi.

Wewe fahamu tu kuwa Rais wa Tanganyika kwa sasa ni Majaliwa na mipaka yake ya utawala inaishia Tanganyika.

Rais wa Tanganyika anaichukulia Zanzibar kama nchi jirani.
 
Kazi tuliyompa huyo mama ni kubwa kwake. Na wananchi washamchoka, atasingiziwa kila jambo ilimradi tu.

Yeye mwenyewe ajisaidii kwa kutengeneza nepotism kwenye teuzi zake.

Lakini kwenye hili commonsense tu hana hayo mamlaka ya kuteua watu kwenye vitengo vya ndani TRA. Baada ya kuteua commissioner wa taasisi na labda kuunda body ya wakurugenzi.

Kwenye structure za ndani hana hayo mamlaka huyo mtu atakuwa mwajiriwa wa TRA muda mrefu tu, kama kawekwa hapo ni sababu za mkurugenzi wa sasa but it has nothing to do na ‘Bi Tozo’ hana hayo mamlaka.

Kwa kifupi ni kwamba nchi imemshinda watu wanajifanyia mambo watakavyo. Busara ni kutangaza mapema 2025 hatagombea.
 
JUMA BAKAR, KWA JINSI NINAVYOMFAHAMU MCHA MUNGU HUYU, WATU WA MAMBO YA CHINI CHINI MMEKWISHA,JAMAA AMENYOOKA VIBAYA SANA,PIA HANA MARINGO KABISA,HONGERA!
Juma Bakari siyo mzanzibar wa kwanza kukamata nafasi hii sababu TRA navyoijua ni ya Tanzania maana Bara na Visiwani. Kumbukumbu zangu zinanikumbusha marehemu Walid Juma aliwahi shika nafasi hiyo hivo sioni kama kuna jambo la ajabu. Hii ni Taasisi ambayo inafanya kazi pande mbili hivo siyo ajabu kiongozi kutoka kati ya pande hizi mbili. Binafsi namfahamu sana Said na pia namfahamu sana Juma wachamungu na sioni cha ajabu mabadiliko ni kitu cha kawaida.Sisi kama importers tumpe ushirikiano kama tulivyokuwa tukimpa ndugu Said sababu wote ni watumishi wa umma wenye weledi.
 
Sema inasemekana wengine walikuwa na ukabila kupendeleana kwenye uongozi?!

Sehemu nyeti zote anaweka wa kabila lake?!

Kila lenye Mwanzo halikosi kuwa na mwisho !

Hii tabia sijui itatibiwa namna gani?!

Halafu huwa ni rahisi kutambua maana watu wanakwambia sehemu fulani yupo fulani na pale na pale .
 
Hivi AG unamshauri nini Rais??? Mana haya makosa ya wazi yanavunja Katiba ya Nchi hivi nyie watu vipi??? Mnatuona mabwege sana nchi hii???
 
Kwa hiyo 'Tanganyika' inahujumiwa ikiwa ndani ya muungano sio ?

.....ina maana kwa sasa Tanzania bara ndio mna kero za muungano ?

JokaKuu zitto junior Nguruvi3 Yoda Kalamu

Mzee Warioba alieleza hili wazi kwamba Tanganyika ilikuwa na kero zake akazianisha, si jambo geni. Umewahi kusoma taarifa ya Tume ya Warioba?

Mjumbe wa Tume ya Warioba Prof. Kabudi akasema ' Ogopa watu wenye yao moyoni, Watanganyika wana yao siku wakiyatoa itakuwa tabu, wapewe Tanganyika yao kabla hajaitaka ''

Watanganyika hawakuwahi kusema wanaonewa na Zanzibar. Watanganyika walikubali kubeba mzigo wa muungano wenyewe kwa 'spirit' ya muungano.

Kinachoendelea sasa hivi kinatisha. Mfano, kero za Zanzibar zilimalizwaje?
Je wewe unajua mambo gani yalikuwabaliwa? Nani alisimamia masilahi ya Tanganyika ?

Kinachokera Watanganyika ni Katiba ya JMT haiheshimiwi na Wazanzibar na hakuna hatua yoyote inayochukuliwa.

Mfano, suala la Zanzibar kujiunga na IOC miaka ya 90 ilikuwa ni ukiukwaji wa katiba na lilizua mjadala mkubwa na G55 kaba ya Mwlaimu hajaingilia kati

Ni kama Rais SSH ameridhia Wazanzibar wafanye watakavyo hata kama ni kukiuka katiba.
Jambo linalokera kwasababu huwezi kuwa na ushirika ambao mmoja ana 'Uhuru' na mwingine ana wajibu.

Mfano, Wazanzibar wana madai ya kutaka yasiyo ya muungano yaondolewe, lakini SSH anadharau madai ya Watanganyika kwa kuweka Wazanzibar wajihusishe na yasiyo ya muungano.

Mfano ni suala la Bandari. Wizara ya Mbarawa si ya muungano lakini Waziri na katibu mkuu ni Wazanzibar.

Bandari Zanzibar wanasema haiwahusu lakini wao ndio wanaongoza mikataba ya Bandari za Tanganyika.
Mapato ya bandari za Tanganyika yanawahusu Wazanzibar kupitia Hazina na BoT

Kuna taarifa za TRAsasa ni mzanzibar lakini kuna TRA Zanzibar ZRB ambazo ni zao.
Kimantiki tu, hili lina ukakasis sana. Hapa watu watauliza, mapato ya Zanzibar kuja Hazina Dar yako wapi?
Mapato ya TRA Zanzibar hayavuki bahari, swali la kujiuliza ni kwavipi huyu asisimamie 'kisichomhusu'?

Kauli ya Watanganyika ni kwamba mambo yao yaachwe kwao ili wasivae koti la Muungano kama inavyodaiwa

Kisaikolojia unaona kwanini Watanganyika wana hasira. Ni kwamba wao wamebeba muungano lakini hawana kauli juu ya nchi yao. Tanganyika inatumika kama kapu la ajira kwa Wazanzibar hata kama hawana uwezo na ukweli kwamba hawana uchungu.

Mbunge wa Zanzibar Ali Saleh Alberto aliwahi kusema '' Nina furaha hilo la Bandari ya Bagamoyo limefeli'
Huyu ni mtu anayelipwa kwa kodi za Watanganyika lakini anachuki hadi nchi inaposhindwa anashangilia.

Watu kama hawa kuongoza taasisi zenye masilahi na Tanganyika ni jambo la hatari. Ni watu wasio na uchungu na wenye kushangilia anguko la Tanganyika. Unaweza kuona kwanini Watanganyika wamekuwa sensitive!

Muungano unahitaji kura ya maoni kwa Wazanzibar, wakitaka iwe ni 3, hawataki njia nyeupe.
Tanganyika haina cha kupoteza zaidi kwa hali yoyote ile iwayo.

Kinyume chake ipo siku Tutaamka hakuna muungano maana walioubeba sasa wamechoka.
Huenda ''mipango yake na ACT'' itafanikiwa na ikiwa ni hivyo, na iwe tu

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…