Mabadiliko ya jina la tume ya uchaguzi

Mabadiliko ya jina la tume ya uchaguzi

Tatizo kubwa la ccm na watu wake ni kufikiri Watanzania wote ni wajinga na hawana akili. Jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo.

Unaiita tume huru halafu wasimamizi na watangaza matokeo ni makada wa chama tawala! Unaiita tume huru, halafu viongozi wote wa hiyo tume wanateuliwa na mwenyekiti wa chama tawala!!

Sitokuja kupoteza muda wangu hata siku moja kushiriki kwenye hayo maigizo yenu.
Safi kabisa,susa hivyohivyo.endelea tu kupigania chama chako hapa jukwaani
 
Pongezi kwa serikali yetu sikivu, mimi ni miongoni mwa tuliotoa maoni kuhusu sheria hii na nilipendekeza jina liwe Tume Huru na Shirikishi ya Uchaguzi.
View: https://youtu.be/3a4SjkV46JY?si=lqufL6e34DyB2Gjr
Japo mapendekezo yangu mengine yote yamekataliwa, ukiomba mambo 10, mambo 9 yakakataliwa, jambo moja likakubaliwa, hatua ya kwanza ni kushukuru kwa hilo moja lililokubaliwa, halafu uendelee kupigania yale 9 yaliyobakia.

Naendelea kusisitiza Watanzania tuwe ni watu wa shukrani, tushukuru kwa madogo ili tujaaliwe makubwa!.
P
 
Back
Top Bottom