Mabadiliko ya Kanuni za Mpira wa Miguu kwa Msimu wa 2019/2020

Mabadiliko ya Kanuni za Mpira wa Miguu kwa Msimu wa 2019/2020

Yeah Man
Ilikua inaleta mkanganyiko sana bhana hii Sheria ya Ball to Hand

Sent using Jamii Forums mobile app
Man U Kimpembe utawajua tu.
Subiri siku mchezaji wa timu yako atakapofanya ile inaitwa Kimpembe Bin PSG vs Man U UCL2018/2019.
Utajuta kufaidika na hii dhambi ya pale Pac de Prince.
 
Ngoja nipate uji. Nije kusoma hiyo​
The International Football Association Board (The IFAB) , imebadilisha baadhi ya kanuni za mchezo wa soka kwenye kikao kilichofanyika wiki iliyopita nchini Scotland . Mabadiliko hayo ni kama ifuatavyo:-

1. KUTAKUWA HAKUNA MREJESHO KUTOKANA NA PIGO LA PENATI

Mchezo utasimama kwa kuanzishwa kama penati imeokolewa au imegonga mwamba , hii ina maana hakuna tena nafasi ya kufuata mpira na kufunga ( Rebound ) kwa maana hiyo wachezaji hawatokuwa na uhitaji wa kujipanga nje ya 18.

2.MPIRA KUCHEZWA NA MKONO.

Kuanzia Juni mosi goli litakalofungwa ambalo limegusa mkono wa mchezaji kwa maksudi au bahati mbaya ( Mfungaji ) halitakubaliwa.

3.MABADILIKO YA MCHEZAJI

Mchezaji ambaye atakuwa anafanyiwa mabadiliko ataruhusiwa kutoka kupitia upande wowote ule wa uwanja

4. GOAL KICK

Mchezaji ataruhusiwa kugusa mpira hata ndani ya eneo la 18 kutoka kwa kipa , ambapo sasa hivi ni mpaka mpira utoke kwenye 18 ndio unaruhusiwa kuugusa.

5. KADI KWA MAKOCHA.

Makocha sasa nao watakuwa wanaoneshwa kadi ya njano na nyekundu tofauti na sasa hivi wanaambiwa tu toka kwenye eneo la benchi la ufundi.

6. KWENYE UKUTA WA KUZUIA MIPIRA ILIYOKUFA

Wachezaji wa upande ambao wanapiga mipira iliyokufa ( freekick ) hawatoruhusiwa kwenda kujumuika kwenye ukuta wa timu ambayo inazuia mipira hiyo , tofauti na sasa huwa wanachanganyika kama kuwatoa mchezoni.

7. PENATI .

Magolikipa wataruhusiwa kuweka mguu mmoja tu kwenye mstari na huo mwingine wataamua wao wenyewe waweke wapi , tofauti na sasa kwamba miguu yote lazima iwe kwenye mstari wakati anapigiwa penati.

Kusoma zaidi [emoji116]

Football rules: How will new IFAB laws affect the game?

Update: Sheria ya penalty itabaki kama ilivyokuwa kufuatia clarification kutoka IFAB kuhusu sheria ya rebounds. [emoji116]
 
hapo kwenye mkono mbona wameangalia sehemu moja tu hii sio haki haiwezekani mtu akifunga goli huku mpila ukigu mkono kwa bahati mbaya goli likataliwe alafu akaachwa beki kaunawa kwa bahat mbaya eti isiwe penat ni bora wangefanya tu hakuna ball hand wala hand ball huku ni kumuonea mfungaji
 
You're deeply so well in football cases, receive more congrats from me Mr.
Unajua sasa hivi makampuni ya betting yanachangia kipato kikubwa sana kwenye mpira, in terms ya matangazo, subscriptions na sponsorships.

Kwa hiyo basi, ili kuzuia/kupunguza iwezekano wa makampuni hayo ku-influence matokeo, inabidi power ya referees ipunguzwe na maamuzi yawe ya wengi.

Pia zile incidences zinazoweza kuleta utata pia zinatengenezewa sheria ili kuondoa mikanganyo.

Tafuta makala kuhusu sports betting zinavyoathiri michezo utanielewa.
 
Hiyo kanuni namba mbili nashauri FIFA waende mbali zaidi wadhibiti na kwenye chama chetu pendwa.
 
Back
Top Bottom