Mabadiliko ya maisha yangu baada ya kuoa

Ndoa ni tamu inategemea na uliyempata, mie nikiambiwa ndoa mbaya, namcheka moyoni, sababu mke wangu hanipi kero kubwa kubwa, zipo zile ndogo ndogo ambazo kwa yale mazuri yake ni sawa na hakuna kero.
Hakupi kero kubwa ila anakupa kero, ungekua mwenyewe hizo kero usingezipata. Kukishakua na kero, whether kubwa ama ndogo bado ni hasara.

Unaoa ili iweje hasa?
 
Ndoa ni nzuri wakikutana wawili wanaoelewana.kila mmoja anatimiza wajibu wake bila kulazimishwa.ama alishindwa anajieleza.
Ila Sasa wakikutana wawili wenye viburi vyao kutoka kwenye makuzi Yao huko🙆
Yeah. Ndoa inahitaji unyenyekevu. Mtu mwenye kiburi, jeuri na mbinafsi anajifikilia yeye tu ndoa haimfai. Sisi tumekaa tukaorodhesha tabia ambazo kila mmoja wetu hazipendi kwa mwenzake na tumeahidiana mwaka 2025 kuziacha, na tunaombeana kuzishinda.
 
Umepoteza uhuru wa kufanya unachokipenda, unaudhiwa na mtu mwingine bila sababu, kati ya kataa ndoa na wewe ulieoa, wewe ndio loser na umesema mwenyewe kwamba umepoteza uhuru, maana yake uko jela, sasa alieko jela na alie huru ni nani loser?
 
Yaani na umeshaanza kuona negative na ndoa bado mbichi kabisaa..
 
Hapo kwenye Tv,mmh noma sana!
 
Hakupi kero kubwa ila anakupa kero, ungekua mwenyewe hizo kero usingezipata. Kukishakua na kero, whether kubwa ama ndogo bado ni hasara.

Unaoa ili iweje hasa?
Hakuna mtu mkamilifu. Hata mshikaji wako anaweza kupa kero ndogo ndogo ila huwezi kusema usiwe na rafiki uwe mwenyewe mwenyewe.
Kazini pia boss wako na workmates wanaweza wakawa wanakupa kero ila huwezi kusema uache kufanya kazi ukae nyumbani. Kama hautaki kero kabisa basi ni vizuri kwenda ukaishi milimani, ingawa na penyewe wanyama, wadudu na ndege watakukera tu.
 
Umepoteza uhuru wa kufanya unachokipenda, unaudhiwa na mtu mwingine bila sababu, kati ya kataa ndoa na wewe ulieoa, wewe ndio loser na umesema mwenyewe kwamba umepoteza uhuru, maana yake uko jela, sasa alieko jela na alie huru ni nani loser?
Kwani mkuu unapo ajiriwa kwenye kampuni ya mtu au serikalini si unapoteza uhuru na unakutana na kero mbali mbali? Mbona hauachi kazi? Kwa sababu kuna manufaa makubwa unayapata ( kipato) ukilinganisha na hizo negatives unazo kutana nazo. Hata mvua ni nzuri ila inaleta tope na vingine, hatuwezi sema tukatae mvua.
 
Negative hazikosekanagi mkuu sisi ni people , kuna mwamba alikua analalamika mkewe dawa ya mswaki anabinya sehemu yeyote na hilo ndio pungufu kuu la mkewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…