Mabadiliko ya maisha yangu baada ya kuoa

Mabadiliko ya maisha yangu baada ya kuoa

Usioe kisa mie nimeoa mzee, maana si rahisi kupata mke bora,
Tizama nikiangalia list ya wanawake niliodate nao, wenye hadhi ya kuwa mke hawazidi hata wa3, sasa ukiiona hiyo list yenyewe ndio utajua ni namna gani ilivyo ngumu kumpata mke sahihi.

Ukitaka kyoa kuwa makini sana.
Usi nambie ni kikosi Cha Chelsea 😆😆
 
Weka nyama nyama
christ within .....sijui nikuambiaje ili upate kunielewa ila iko hivo unajua kuna kitu kinaitwa mwez je unajua mwez huu moon una leta au unasababisha mood changes na mambo mengine sasa kipind hiki kila week kuanzia alhamis mpaka jumamosi inabid ujitoe kwa kufunga ili kuactivate jicho la ndani na sikio la ndani ..


tutaendelea
 
Tunawatakia maisha marefu wanandoa wote , ndoa changa, na ndoa za muda mrefu. Maisha ya ndoa ni matamu sana, ndoa ni chuo cha aina yake mkiishi kwa kusaidia na,kushauriana,kubuni miradi midogo na mikubwa mtaona maisha ni mazuri sana penye changamoto mnasameheana na kusahau kama ilivyopita 2024.
 
Ndoa ni tamu inategemea na uliyempata, mie nikiambiwa ndoa mbaya, namcheka moyoni, sababu mke wangu hanipi kero kubwa kubwa, zipo zile ndogo ndogo ambazo kwa yale mazuri yake ni sawa na hakuna kero.
Wacha wee wifi kiboko aisee 😄
 
Kusema kweli ndoa yangu bado changa, ndio kwanza mwaka mmoja. Najua changamoto nyingine zinaweza kuja na nimejiandaa
Kumbe mwaka tu, ngoja tukuache kwanza mfikishe walau 7 yrs, utakuja kufuta mwenyewe hiki ulichoandika
 
Ongeza sasa wapili na wa tatu kabla hajaanza kusema tulichuma wote....

Utanishukuru baadae
 
Kitu cha kwanza kitakacho kugharimu ukiingia kwenye NDOA ni uhuru wako.....kuna muda unalazimika kuyakubali mambo ili tu kuwe na amani hata kama nafsi yako haitaki......

Bado NDOA inabakia kuwa ni taasisi ngumu sana kimaumbile ndio maana kuvumiliana ni jambo la msingi kwa kuwa kero na changamoto nyingi sana.......

Nawashauri vijana wafikirie mara mbili mbili kabla ya kufanya maamuzi ya kuoa..... unatakiwa ujipange kimwili na kiakili kuyakabili mazito hata yale ambayo hukuyatarajia kabisa.......

NDOA NDOANO.......
Siko tayari kupoteza uhuru wangu kwa ajili ya limtu nililoliokota barabarani.
 
Kazini pia boss wako na workmates wanaweza wakawa wanakupa kero ila huwezi kusema uache kufanya kazi ukae nyumbani.
Kazini nitavumilia kero kwa sababu natafuta ugali.

Tofautisha kati ya NECESSITY na LUXURY.

Ndoa ni LUXURY YA KIJINGA yenye mateso ya kujitakia.
 
hapo kwenye channel naangalia kwa masimamgo, nalipia compact lakin mbungi zinanipita 🤣,,
 
KUOA NI KUKOSA AKILI NI UPUUZI USHAMBA NA UKICHAA...
Mwanaume rijali unaoa?
 
Haya ni mabadiriko ya maisha yangu baada ya kuoa.

POSITIVE.

1. Kabla ya kuoa nilikuwa naweza lala bila kula au nikala mkate na juisi tu nikalala ila sasa nikitoka kazini na njaa nakuta mke wangu amenipikia chakula nikipendacho.

2. Kabla ya kuoa nilikuwa naweza amka asubuhi,nataka kwenda kazini nakuta nguo zote chafu. Sasa hivi hata sifikilii kuhusu nguo za kuvaa, wife ana deal vizuri na hilo.

3. Kabla ya kuoa nilikuwa nateswa sana na njaa ya sex ( nyege) inafikia wakati umekaa kwenye daladala unashangaa baba wa taifa anasimama bila sababu.Sasa hivi mke wangu ananitosheleza vizuri.

4. Nilikuwa nateswa na stress za kazi. Nikitoka job na stress, najifungia ndani na stress zangu, nakosa hata usingizi. Sasa hivi nikitoka job nikifika home tu stress zinaisha kesho yake nakuwa mtu mpya.

5. Nilikuwa nakwepa kupokea wageni sababu nyumbani kwangu mazingira yalikuwa hovyo. Sasa hivi natamani kupokea wageni, na wageni wakija wanaondoka wamefurahi.

6. Nilikuwa nateswa na underweight, nguo hazikai kiunoni sababu ya kukonda kupitiliza. Sasa hivi nalazikika kufanya mazoezi kuepuka overweight.

7. Jumamosi naamka asubuhi nakula chakula cha kiume( morning Glory) kisha nalala tena nasubiri kuamshwa kupata breakfast 😀.

NEGATIVES

1.Matumizi ya pesa ya matunzo kwa mke kama nguo, kusuka, mafuta, kumtoa out siku moja moja.

2. Kukosa uhuru wa kufanya ninacho taka nikiwa kwangu kama vile kuweka Chanel ya TV ninayo taka ( sasa hivi nalazikika kuangalia vitu vya kijinga kama juakali)

3. Kukosa uhuru wa kutoka na kurudi muda ninao taka.

4. Maudhui madogo madogo ya wanawake kama kununa kwa sababu za kijinga na kudeka.

5. Sasa hivi sifanyi vitu kwa kujiangalia mwenyewe lazima nimfikilie na mke wangu.

NB: ndoa ina postives na negatives, ombea postives ziwe nyingi na negatives ziwe zinazo vumilika. Usiwasikilize team kataa ndoa, ni losers. Za kuambiwa changanya na zako

Mazara ya ndoa ni Kati ya miaka 10 mpaka 15. Kama ujafika hapo mwombe Mungu n funga mdomo; ndo ni jambo gumu sana ukikosea
 
POSITIVE NA NEGATIVE zote light points. Subiri baada ya miaka mitano plus utakuja heavy points
 
Back
Top Bottom