nipende kuchukua fursa hii kuipongeza sana serikali ya Tanzania KATIKA jitihadaa zake za kuhakikisha kila Mtanzania anapata elimu angalau ya sekondari ili kufukuza ujinga ,hii Ni baada ya kuifanya ELIMU ya msingi na sekondari kuwa bure, lakini ELIMU ya Tanzania bado haijafanikiwa kumkomboa Mtanzania ,hii Ni Kwa sababu Kijana aliyemaliza kidato Cha nne au sita anakuwa hawezi kufanya kazi yoyote ya kitaaluma maana kwa wakati huo anakua anajua kusoma na kuandika tu na hana ujuzi wowote(amepoteza muda mwingi amepata kidogo).
Kwa Kijana anayefaulu masomo ya kidato Cha sita na kuingia chuo kikuu akimaliza naye hatakuwa na ujuzi Ila nadharia,kijana huyu asipoajiliwa na kufundishwa kazi hawezi kufanya kazi kwa kutumia taaluma yake(ukiondoa mwalimu) maana anakuwa hana ujuzi wa kuhimili mahitaji ya soko na hivyo taifa linashindwa kuendelea kwa Kasi kwa sababu watu wengi waliotarajiwa kufanya SHUGHULI za kuchochea uchumi hawafanyi kazi
Nini kifanyike?
1)Serikali ihakikishe kila kijana anayemaliza shule ya msingi aweze kujieleza vizuri kwa lugha ya kiswahili na kiingereza ,lugha ya kiingereza imekuwa ikiwasumbua sana vijana wa kitanzania na kuwakosesha fursa nyingi katika soko la ajira ,Wengi wa wasomi wa chuo kikuu waliosoma shule za serikali hawawezi kujieleza vizuri kwa lugha ya kiingereza ambayo ndiyo lugha kubwa ya kiofisi na kibiashara ,ili vijana wetu waweze KUSHINDANA katika soko la ajira KITAIFA na KIMATAIFA Ni lazima lugha ya kiingereza iwekewe mkazo katika shule za msingi ,hii itawezekana tu kama masomo yote yataanza kufundishwa kwa lugha ya kiingereza isipokuwa kiswahili ,inawezekana!
2) Masomo yanayofundishwa shuleni ni lazima yaendane na uhalisia na mahitaji ya dunia ya leo inayoendeshwa kwa sayansi na teknolojia ,vijana waanze kujifunza program za kompyuta (coding) wakiwa shule za msingi,mataifa yaliyoendelea katika kuzalisha program za kompyuta na teknolojia huwafunza watoto wao katika umri mdogo na wanapokuwa wakiendelea na masomo ndipowavumbuzi hupatikana ni Jambo la kusikitisha katika nchi yetu kusikia kuwa Kijana aliyemaliza kidato Cha sita hajui kuwasha kompyuta!
3) Muundo wa shule za sekondari zote (form 1-form 4) uwe wa shule za ufundi ,vijana wa sekondari wajifunze ufundi umeme, elektorniki ,mawasiliano angani ,ujenzi ,magari ,udereva ,upishi ,compyuta , hisabati, sayansi ya viumbe, uchoraji, ushonaji, biashara na ujasirimali katika Karne ya 21 nk vitu ambavyo ni halisi katika maisha.
Kijana akimaliza kidato Cha nne anapewa na leseni ya udereva maana anakuwa anajua kuendesha magari,mfano nzuri wa hiki Ni Hawa (thttps/alphaschools.ac.tz/aviation/)
Huyu hata asipoendelea kusoma anakuwa na pa kuanzia katika maisha yake maana anajua kiingereza vizuri tangu shule ya msingi , ana leseni ya udereva, ana ujuzi.
4) Tuondoe kitadato Cha tano na sita, hakuna sababu ya mwanafunzi kusoma kidato Cha tano na sita badala yake kwa wanaofaulu kidato Cha nne wote waende kusoma diploma kwa fani watakazozichagua, huko wataendelea kuweka mizizi kwa Yale waliyojifunza sekondari na shule ya msingi, Kijana anayemaliza diploma anakuwa tayari kwa kuingia soko ajira akiwa ameelimika kwelikweli
5) Wanafunzi wa chuo kikuu wawe ni wale waliomaliza diploma kwa fani walizochagua ,vyuo vikuu hasa katika masomo ya sayansi na uhandisi vitumie teknolojia iliyopo sokoni kufundishia, Kuna wakati vyuo vinatumia teknolojia ya mwaka 1800 kufundishia kijana wa mwaka 2022, anapomaliza masomo anakuta vitu alovyojifunza chuoni havipo duniani inabidi aanze kujifunza upya . Hapo ndipo tutapiga hatua katika ELIMU yetu ,tutakuwa na wasomi na wavumbuzi, wanaoweza kujiajiri na kuajirika, wanaoweza kuanzisha mambo mapya kwa manufaa ya wengi nk
Nawasilisha

Upvote
0