Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Mabadiliko ya mwonekano JamiiForums - Juni 2022

Maxence Melo

JF Founder
JF Staff
Joined
Feb 10, 2006
Posts
4,324
Reaction score
13,967
Wakuu,

Tupo kwenye hatua za mwisho kuja na JF yenye mwonekano mpya ambayo inaendana na mabadiliko ya teknolojia. Kwa wanaohitaji kuwa sehemu ya majaribio, mnakaribishwa...

Katika mabadiliko haya, huenda ukakutana na kitu kikakufurahisha, kikakuchanganya, kikakufanya uone kuna haja ya kuongeza au kupunguza n.k - usisite kutujulisha kupitia uzi huu.

Thread hii itatumika kukusanya maoni yenu na yatazingatiwa ajili ya kujenga sehemu bora na salama zaidi kwa ajili ya kila mmoja wetu.

Kwa wale watumiaji wa App, tunashauri kujaribu App Mpya ya JamiiForums: Fuata hatua hizi kwani itaendana vema zaidi na kinachokuja.

Tunawashukuru kwa ushirikiano mnaotupa kila mara kwani hadi toleo hili ni tokana na maoni yenu.

Kutakuwa na features kadhaa hazitakuwa released mapema hadi zikamilike kufanyiwa testing ndipo ziwe applied.

Tunawapenda, tunawajali na tunaahidi kuendelea kutoa huduma bora.

Asanteni sana!

===== UPDATES======

Changes on the new version:

1) Kuna urahisi wa kufichua mambo mazito bila data zako zozote kuchukuliwa na bila post kwenda public kwanza (utaona button ya Fichua Uovu). Hii itasaidia hata wasio wanachama (baadae) kushiriki kikamilifu kupinga ufisadi na rushwa kwa ujumla.

2) Faragha ya mwanachama imelindwa zaidi, hakuna wa kujua wewe ni nani on JF bila wewe kumpa access ya kifaa chako (simu, tablet au pc). Tulipata vilio vya watu kuchunguliwa IDs tukaja na suluhu.

3) Unaweza kuchagua kutumia JF ikiwa light version, dark mode au dark blue mode (my favorite).

4) Maandishi ya sasa yanasomeka kirahisi zaidi na wenzetu wenye uoni hafifu. Wasioona kabisa lakini wana vifaa vya kusomea wataweza kuitumia JF kwa urahisi zaidi.

5) Soon kuna mambo mapya yanaanza kufanyika via JF, mabadiliko haya yamelenga kupokea yajayo kuanzia mwezi huu na kuendelea.

6) Ukiwa kwenye forum yoyote, huhitaji kubonyeza Page 2, Page 3, Page 4. Wewe vuta kwenda chini tu, mada zitakuja (scroll down).

Nitaendelea…
 
nimekuwahi mjomba
Hahaha... Mnanifurahisha.

Nikiri, thread hii nitakuwa karibu nayo ili kuhakikisha kila maoni yanafanyiwa kazi.

Kufikia Jumatatu next week tutakuwa tumekamilisha kuweka fixes (kama zitahitajika).

Timu yetu itakuwa hapa kukuhudumia; ni furaha yetu kusikia toka kwako
 
Mbona mi sipati notification?

Kuna watu tunawablock ila bado wakianzisha mada twaona mada zao

Kwanini msiweke ukimtia mtu block usione mada yoyote anayoanzisha wala hata changizo zake zozote zile

Pia kwanini msituwekee uwezo wa kuzuia mada fulani, tusizione kabisa ie mada za kukashfu dini za wengine etc
 
Back
Top Bottom