w0rM
Member
- May 3, 2011
- 81
- 192
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria inawaalika wadau kutoa maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 7 wa Mwaka 2021 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 7) Act, 2021.
Mkutano wa kupokea na kusikiliza maoni ya wadau (Public Hearing) utafanyika siku ya Alhamisi tarehe 03 Februari, 2022 saa 5:00 asubuhi katika Ukumbi Na. 9
Jengo la Utawala, Ofisi ya Bunge, Dodoma. Kamati inawaalika Wananchi wenye maoni kuhusu Muswada huo kufika na kuwasilisha mani yao kabla haujapelekwa katika hatua nyingine.
Aidha, Kamati itapokea maoni kwa njia ya posta au baruapepe kabla ya Jumamosi tarehe 5 Januari 2022 saa 5:00 asubuhi kwa anuani
Katibu wa Bunge
Ofisi ya Bunge,
Mtaa wa Makole,
S. L. P. 941,
41105 DODOMA.
Au baruapepe cna@bunge.go.tz au Kamati@bunge.go.tz
My take:
Muda uliyoweka kwa ajili ya kutolea maoni ni muda mchache sana hasa ukizingatia kwanza madaliko yenyewe ya sheria yameandikwa kwa lugha ya Kiingereza.
Kama kweli Kamati ingelikuwa inataka maoni haya ingeweka muda mrefu na sheria zingekuwa kwa lugha zote mbili ili Wananchi waelewe na kuweka maoni yao.
Hili naona ni bora liende tu na ili kuweka ‘justification’ kuwa mabadiliko haya yalipitiwa na Wadau
Kuona mabadiliko yaliyopendekezwa angalia pdf niliyoambatanisha hapa