Mabadiliko ya Sheria: Rais, Makamu wake, Jaji Mkuu, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge kutofunguliwa kesi Mahakamani

Nimeandika nkafuta, nkandika tena nkafuta.

Kweli miaka 60 baada ya uhuru tunawaza kupeleka miswada bungeni ya kuwalinda viongozi kwa makosa yao wanapokuwa madarakani, tena karne ya 21??? Dah![emoji854][emoji6]
 
06 JUNE 2020
Utawala wa Sheria

Uchambuzi wa Mswada Na. 3 wa Mwaka 2020, mtaalamu wa sheria afafanua


Uchambuzi wa Mswada Na. 3 wa Mwaka 2020 Mei 29, 2020, Bunge la Tanzania limekaribisha wadaua na wananchi kutoa maoni yao kuhusu Mswada Na. 3 unaorekebisha sheria mbalimbali ikwemo Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Kimsingi na Wajibu, 1994 (BRADEA) na Sheria ya Uongozi wa Mahakama namba 4 ya 2011.

Moja ya mambo yanayopendekezwa katika mswada huo wenye lengo la kubadili sheria 13 ni pamoja na kuongezwa kinga ya kisheria kwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, na Jaji Mkuu kutokushitakiwa moja kwa moja na badala yake mashitaka kuelekezwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Mapendekezo hayo pia yanapekwenda kuwapa kinga wafanyakazi wa mahakama, ambapo kinga hiyo ikitumika vibaya itapelekea uvunjifu mkubwa wa haki. Tazama uchambuzi huu kisha toa mano yako.

Source : HAKI TV
 
June 9, 2020
Dodoma, Tanzania

MBUNGE ATAKA RAIS ALAZIMISHWE KUONGEZEWA MUDA HATA KAMA HATAKI "ATAKE ASITAKE TUTAONGEZA MUDA-NDUGAI
Spika aunga mkono hoja , ahaidi katiba inaweza kubadilishwa maana Bunge lina mamlaka ya kubadilisha katiba ikiwemo muda wa Rais kukaa madarakani kama pendekezo litawasilishwa Bungeni

 
Mfano kuweka kinga ya kutokushtakiwa kwa viongozi waandamizi.Kwangu hili si tatizo.Hata akishtakiwa,sioni ni jinsi gani hiyo itabadilisha maisha yangu.Mungu atahukumu yeye mwenyewe kwa haki.

Kuongezewa Rais muda wa kuongoza nchi.Naam,waongeze tu.Kama aishivyo Mungu wangu,sielewi hata sekunde chache zijazo nitakuwa hai au mfu.Ni nani ajuaye?Mungu mwenyewe atahukumu kwa haki.Akiruhusu,mimi ni nani nikatae?Akikataa,hata kama mtu atakubali,hakuna anayeweza kushindana naye
 
Ila kweli maana hiyo nafasi yenyewe ni moja tu haiwezekani wote kupata hata tungekuwa tunabadilisha kila mwaka,kuna watu wametumia nguvu muda na mali zao ila hawakupata hiyo nafasi. Tatizo ni kwamba wanaoonekana kung'ang'ania na wanaopinga hilo jambo wote wana tatizo aina moja.
 
Naomba kuuliza mbona cheo cha Makamu wa Rais hakipo kwenye orodha ya viongozi wasioshtakiwa baada ya kustaafu??

Ikumbukwe Bunge la 11 katika shughuli zake imependekeza kufanya mabadiliko ya sheria mbalimbali ikiwemo ya kutoshtakiwa kwa Rais, Jaji Mkuu, Spika, Naibu Spika na Waziri Mkuu, kama katika kutekeleza majukumu yao ikatafsiriwa kutenda kinyume na Katiba ya nchi.
 

Siku akipatikana Rais akaamua mfano unaishi jirani na makazi yake kuwa nyumba zote ikiwemo za ukoo wenu zivunjwe kwa kuwa anataka kujenga kiwanja 'chake' cha ndege ndipo utajua maana na umuhimu wa sheria ya kuwadhibiti na kuwawajibisha. Hilo ni dogo, viongozi wanaweza wakafanya mambo ya ajabu zaidi ya mfano huo ukisoma historia za watawala ulimwenguni na ktk vitabu vya imani.
 
Wananchi wote tuwe na kinga

These motherfuvkers want to get away with murder...

Wanajipotezea muda tu,....wenyewe wafanye crime tu....tukiingia tunafunga wote wether watake au wasitake....

Upumbavu huu
 
Kwa upande wangu sijaelewa Magufuli kupeleka muswada bungeni wa kutoshitakiwa yeye na viongozi wote wa mihimili ya nchi kwa makosa wanayofanya wakiwa madarakani.

Inakuwaje mtu muadilifu, mcha Mungu, kiongozi wa wanyonge, mtu asiyependa rushwa na ufisadi akawa muoga wa kushitakiwa? Una hofu na uwoga gani unatarajiwa kufanywa au ushafanywa hadi kujiwekea kinga kubwa kiasi hicho?

Bila shaka anatuambia yeye sio msafi hata kidogo kwa sababu ukiwa wewe ni msafi unapata uwoga gani wa kushitakiwa?
 
Nyerere hakutaka hakuogopa japo kuna watu waliumia wakati wa vijiji vya ujamaa
 
Basi mimi nlijua rais ata akitoka madarakani hawezi kushtakiwa apa kwetu. Kumbe waliopita tunaweza kuwashtaki?
 
Acha mzuka we, Magu hajaiweka yeye, ameikuta ipo tangu na tangu! Huo mzuka peleka ufipa!
 
Kwani shida ipo wapi mkuu. Si yeye mwenyewe amekwishaonyesha mifano kadhaa?

Kwani sheria inapotungwa haiwezi tunguliwa?

Labda useme huyo anayetakiwa kuhakikisha na kuona haki zikitendeka naye awe bwege!

Sioni tatizo kwa hizi sheria mbovu kutunguliwa kama anayeheshimu haki anaamua kuzitupilia mbali na kuwawajibisha waliojitungia sheria ziwalinde kwa kufanya maovu.
 
Inashangaza sana..
Raisi pendwa wa dunia, muadilifu, mnyenyekevu, mpenda wanyonge, mzalendo, msomi, anayechukia wapiga dili..........

Everyday is Saturday.......................... 😎
 
Swali la msingi kabisa hili na wangekupata wangekuvunja shingo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…