Mabadiliko ya Sheria: Rais, Makamu wake, Jaji Mkuu, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge kutofunguliwa kesi Mahakamani

Mabadiliko ya Sheria: Rais, Makamu wake, Jaji Mkuu, Waziri Mkuu na Spika wa Bunge kutofunguliwa kesi Mahakamani

Prince ndie spika ajae Kama watz watakosea tena,kwa watakayotendewa watz again 5 yrs yatakuwa ni Mara 10 ya walivotendewa 5yrs back.
 
Nyerere angekuwa hai angekuwa anatawala tena kwani angeisha kuwa ametoka BUTIAMA zamani!!! Hivi huko ccm hakuna wanaume wanaoweza kuthibiti udikteta huu wa Jiwe?
Hakuna walishauza chama kwenye chattle family.
Mmiliki wa chama ndie mwenye ccm rejea chaguzi za marudio.
 
We kilaza kaa kimya. Kwanza Rais akiwa madarakani hashitakiwi kwa jinai yoyote. Pili mwanasheria mkuu atawasimamia hao viongozi kwa ishu ambazo watakuwa wanmeshitakiwa wakifanya kazi zao. Na imeruhusiwa kuwashitaki ila mashitaka yanapelekwa kwa Ag. Hata mpaka sasa Ag ndio huwa ana wakilisha viongozi wakishitakiwa kwa kazi wanazozifanya.
Ashtakiwi kwa makosa ya maslai ya taifa na si kwa makosa binafsi ya kuvunja katiba.Sema huwa wanalindana tu
 
Amesema, Kifungu namba 7(4), ikiwa malalamiko ya uvunjifu wa haki unaelekezwa kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania au, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, au Jaji Mkuu wa Tanzania, malalamiko hayo yatafungliwa dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali ikiwa na maana hakutakuwa na uwezekano wa kufungua kesi dhidi ya viongozi hao.
Aisee . . . yaani wahsaanza kujiandalia kinga ? We are doomed aisee. Nina mashaka sana na utawala wa sherika kwa siku zijazo
 
Sijui ni uzee, hii taarifa jinsi ilivyowasilishwa ninapata tabu sana kuelewa.Kama si uzee basi itakuwa UWAFE(UPUNGUFU WA FEDHA)
 
Mbona wanaturudisha nyuma ninkwanini viongozi wa kiafrica wanapenda Sana kuabudiwa yanj kuwa untouchable
 
Yaliyotabiriwa yanaanza kutimia na ndivyo serikali zote za kidikteta,zinaanzaga kwa style hii
 
Dr. A. Lwaitama : Wananchi hawashirikishwi kuamua mambo makuu ya nchi , mkoa au wilaya. Wachache wamejitwalia haki hiyo ya wananchi




Bunge halina meno, hivyo kushindwa kuchambua miswada inayoletwa mbele yake kwa manufaa ya wananchi. Bunge limejaa watu wa chama kimoja ambao ni waoga kukataa jambo au kurekebisha jambo kutokana na mfumo mbovu wa utawala wa nchi unaofanana na ukoloni. Wabunge wamekuwa mateka wa kisiasa.

Source : Mwanahalisi TV
 
Hapo kabla walikuwa wanafunguliwa kesi?
Ndiyo ilikuwa ukitafuna Pesa ya serikali kama mil 800 unafunguliwa kesi na kuhukumiwa adhabu kali ya kufakia hospital mwezi mzima
 
Wanataka kutufanyaje mbona wanajihami mapema!!!??????
 
Tukiishi kwa imani ya "ipo siku" tutashindwa kutumia vyema akili zetu na haki yetu ya kuhoji na kuwawajibisha viongozi kikatiba

Hawa ccm taratibu wanataka kuigeuza Tanzania koloni lao na wanaweza kwasababu wananchi
TUNANYAMAZA!
Kinga ya kutoshtakiwa si Kinga ya kutolipwa kulingana na matendo yako.
Ukiwatendea mabaya wenzio jiandae tu kulipwa mabaya yako
 
Maana ya Nguvu ya Umma yafafanuliwa :

Mtu-Huru hawezi kuuza uhuru wake kwa vitu yaani kwa sababu tu ya Maendeleo ya Vitu mtu afanywe mateka ndani ya nchi yake.





Source: DarMpya TV
 
Msitishike. Siku ya siku UNA SUSPEND KATIBA, UNAUNDA MAHAKAKAMA MAALUMU UNAWASHITAKI NA KUWAFUNGA. Ni ujinga mchana kweupe kujitungia sheria za kuwadhulumu, kuwakandamiza wengine and then zisimame after you! Common sense, reason and justice dictate that katika udhalimu kama huu you act that way to make sure that Justice is done after them!

Lex malla, lex nulla. A bad law is no law
Nimelisema hili hata Romania chini ya Ceausescu walikuwa na sheria za namna hii, siku ilipofika wananchi wakasema enough is enough wakatunga sheria zao na mwisho wake ukawa aibu
 
Kuna conditions zimewekwa ili uweze kufungua kesi. Sio kwamba unazuiliwa. Hata hivyo toka hapo awali hata ukimshitaki Rais ni Ag ndio alikuwa anamuwakilisha. Mimi nafikiri Chadema wamepanick kila kitu mnadandia mkizani kitawasaidia.
Kama hata sasa hivi iko hivyo, mabadiliko ya sheria ni ya nini?
 
Makosa binafsi ya kuvunja katiba kama yapi? Fafanua.
Soma vizuri speech ya Jaji Mstaafu Samatta.

Kuna tofauti ya "kama" na "akiwa" Rais.

Mfano, hata kama umekerwa sana na kuachiwa huru Babu Seya na wanawe, huwezi kumshitaki. Amefanya kazi kwa kutumia mamlaka yake kama Rais.

Lakini akichukua rushwa kwenye ujenzi wa kiwanja cha ndege, hilo halifanyi kama Rais, amelifanya kama yeye. Hilo unaweza kumshitaki.
 
MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) kwa kushirikiana na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) wamepinga muswada wa sheria wa marekebiaho ya sheria mbalimbali nchini namba 3 wa mwaka 2020.

THRDC na LHRC wametoa tamko la kupinga muswada huo leo Alhamisi tarehe 4 Juni 2020 mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amesema katika mswada huo kuna marekebisho ya Sheria ya utekelezaji wa Haki za Kimsingi na Wajibu ya 1994 (BRADEA).

Olengurumwa amesema, marekebisho ya kifungu Kifungu namba 4 cha BRADEA kinarekebishwa na kusomeka kwamba, maombi ya kufungua kesi Mahakama Kuu hayatakubaliwa endapo hayajaambatanishwa na kiapo cha mlalamikaji kuelezea jinsi alivyoathiriwa na uvunjifu wa haki na wajibu katika ibara ya 12 hadi 29 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977.

“Tumekuwa tukipeleka kesi ya kulalamika ukiukwaji wa haki za binadamu uliopo katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 12 mpaka 29, sasa kwa mujibu wa mabadiliko ambayo yanakuja sasahivi ni lazima uwe na cheti cha kiapo cha kuonyesha kiasi gani wewe mwenyewe umeathirika na ukiukwaji huo,” amesema.

Amesema, Kifungu namba 7(4), ikiwa malalamiko ya uvunjifu wa haki unaelekezwa kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania au, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Spika wa Bunge, au Jaji Mkuu wa Tanzania, malalamiko hayo yatafungliwa dhidi ya mwanasheria mkuu wa serikali ikiwa na maana hakutakuwa na uwezekano wa kufungua kesi dhidi ya viongozi hao.

View attachment 1468939

Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC), Onesmo Olengurumwa (wakwanza kulia), Mkurugenzi wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Anna Henga (Wapili kulia).

“Sasa hivi, tuna kesi nyingi tumefungua dhidi ya Spika na kuna kipindi Rais alifunguliwa kesi na akina Fatma Karume na Ado Shaibu hizo zote zitaondolewa maana yake Tanzania hatutaweza kumshtaki mtu kama yeye kwa kukiuka Katiba,” amesema.

Aidha, Olengurumwa amesema sheria nyingine ambayo inaelekea kufanyiwa mabadiliko ni sheria ya uongozi wa Mahakama namba nne ya 2011.

Amesema, kifungu namba 64 (a) cha sheria hiyo kimerekebishwa na kuandikwa kuwa mfanyakazi yoyote wa mahakama hatoshtakiwa kwa jambo lolote atakalolifanya au kutolifanya kwa nia njema atakapikuwa anatekeleza majukumu yake.

“Hii inaweka kinga kwa mtu yoyote alioko mahakamani hata kama si Jaji au Hakimu na madhumuni ya marekebisho hayo ni kuipa mahakama nguvu ya kukataa maombi ambayo hayajakidhi matakwa ya ibara wao ndio wanadai hivyo.”

“Madhumuni ya marekebisho haya yanakwenda kuondoa nguvu za mtu mmoja mmoja au taasisi kama zakwetu kufungua kesi kwa sababu ya kulinda haki zozote zinazokiukwa Tanzania na hii ni kinyume na ibara ya 26 ya Katiba ya Tanzania ambayo imemruhusu mtu yoyote kwenda mahakamani kudai haki,” amesema.

Kwa upande wake, Anna Henga, Mkurugenzi Mkuu wa LHRC, amesema mapendekezo ya marekebisho ya sheria ya utekelezaji wa haki za msingi na wajibu yanapingana na ibara ya 26 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Baada ya Tanzania kujitoa kwenye mahakama ya Afrika sasa Azaki hatuwezi kwenda huko sasa hata kwenye mahakama za ndani hatutaweza kwasababu sheria hii inaweza kuzuia haki hiyo,” amesema.

Hata hivyo, Henga amesema marekebisho anayaona kama ni muendelezo wa kutaka kunyima haki kwasababu hata sababu za Tanzania kujitoa katika mahakama ya Afrika hazijajulikana hadi sasa.

“Ni kitu cha ajabu sana kwamba Afrika Mahakama ipo nyumbani kwako kama inakuletea heshima wewe ndo unayeitunza halafu unajitoa kwanini? hata hii, unaweza ukashangaa ni kwanini wazuiwe watu ambao wanataka kutetea haki za watu? Ukitafsiri kikawaida maana yake haki itavunjwa zaidi,” amesema.

THRDC na LHRC wametoa wito kuwa mapendekezo hayo ya mabadiliko ya Sheria ya Utekelezaji wa Haki za Kimsingi na Wajibu yaondolewe kabisa Bungeni kwakuwa maandalizi ya mapendekezo hayo hayakuhusisha
kabisa wadau mbalimbali wakiwemo wadau wa haki za binadamu tangu mwanzo.

Aidha, wamesisitiza kuwa kifungu cha mapendekezo ya sheria kinachotaka kutoa kinga kwa wafanyakazi wote wa Mahakama kutokushtakiwa kirekebishwe na kinga hiyo iendelee kuwepo kwa Majaji na Mahakimu pekee kwa mujibu wa Katiba.

Muswada huo unaopendekeza mabadiliko makubwa ya sheria mbalimbali ambayo THRDC na LHRC wanalaani wakieleza kuwa yanalenga kuondoa haki ya kufungua kesi za kikatiba kwa niaba ya wananchi, uliwasilishwa bungeni na umepangwa kujadiliwa kwenye mkutano wa 19 wa Bunge (Mkutano wa Bajeti) ambao ulianza tarehe 05 Mei na utamalizika
Juni 19 mwaka 2020.



Ccm plz plz plz tunawaomba muokoe hili taifa linaenda kupotea tumieni chama chenu kuwajibisha serikali kupitia watu wenu hi nchi inaingia shimoni mkiwa mnachekelea Kama mna BEt kuishinda chadema wakati nchi in angamia.
 
Nimekuwa najiuliza kwanini Serikali inapeleka Muswaada wa kuwakinga Viongozi kwani wanataka kufanya nini ili Wakingwe?
The growth of totarianism in Tanzania. The growth of Nazism in Germany started slowly but steadily at last, it took Germany with gush of fire. Very dangerous.
 
Back
Top Bottom