Mabadiliko ya Tabia Mitandaoni: Je, Kuonyesha Maumbo Kumekuwa Sehemu ya Utamaduni Mpya Afrika?

Mabadiliko ya Tabia Mitandaoni: Je, Kuonyesha Maumbo Kumekuwa Sehemu ya Utamaduni Mpya Afrika?

franci45

Member
Joined
Nov 8, 2023
Posts
76
Reaction score
113
Kwa heshima kabisa, kuna tabia ambayo imekuwa ya kawaida sana siku hizi hasa kwenye mitandao ya kijamii. Wadada wengi wanapojirekodi video mara nyingi hugeuka makusudi kuonyesha maumbo yao hasa makalio, hadi imekuwa kama ni sehemu ya kawaida ya content nyingi za Afrika na hasa Tanzania.

Swali la kujiuliza ni je, hii ni sehemu ya utandawazi na kutafuta attention/umaarufu, au ni mabadiliko ya maadili na namna jamii inavyojieleza siku hizi? Maana imefika hatua hata video ambazo hazihusiani kabisa na urembo au mavazi bado lazima kuwe na ‘geuzo’.

Binafsi naona imekuwa trend kubwa sana huku kwetu kuliko hata maeneo mengine ninayoona mtandaoni. Je, wenzangu mnaonaje kuhusu hili?
 
Back
Top Bottom