Dar - Temeke, Kata ya Toangoma
Tulivokuwa wadogo tulikuwa tumeshakariri kabisa huu ni msimu wa mvua, huu ni msimu wa kipupwe, huu ni msimu wa jua ila kipindi hiki mambo ni tofauti kabisa haijulikani ni kipind cha mvua,vuli,kipupwe wala masika ni mwendo wa jua Tu, so sad ni kwamba haya mabadiliko yanatokea kwa haraka mnoo, nawaza sijui wajukuu zetu wataishi katika ulimwengu wa namna gani
Nakumbuka kipindi cha mvua mito (Sisi tulikuwa tunaita mabwawa) yalikuwa yanafurika kwa maji tukiyatumia kuoga, Hadi kuvua samak wadogo wadogo ila sasa hv Yale mabwawa yote yamepotea kabisa nyumba zimeshajengwa maeneo hayo, hata mvua zinyeshe hayafuriki tena