Mabadiliko ya tabia nchi yameleta athari gani sehemu unayoishi?

Mabadiliko ya tabia nchi yameleta athari gani sehemu unayoishi?

Idrissou02

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2018
Posts
354
Reaction score
656
Athari za mabadiliko ya tabia nchi zimekuwa kubwa mno ikiwemo Joto kali lisilostahimilika, Mafuriko yanayoharibu makazi na miundombinu, Ukame unaosababisha kupotea kwa rotuba ya ardhi na Kuzorota kwa sekta ya kilimo.

Katika kupaza sauti juu ya suala hili ambalo linahitaji nguvu kubwa ya wadau mbalimbali kulikabili, tueleze kwenye uzi huu ni madhara gani yaliyosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi katika eneo lako?

NB: Sehemu ambayo itaonekana imekumbwa na madhara makubwa zaidi, tutamuhusisha atakayekuwa amepaza sauti hiyo kwenye harakati ya kuleta mradi wa kuleta nafuu madhara yaliyosababishwa eno husika. Asante.
 
Huku kwetu Basotu, wilayani Hanang hali mbaya. Mahindi yamekauka, Boko hawaonekani tena. Kambale wameadimika sana na kupelekea kupanda bei.
 
Kama kampeni ya vyama vya siasa ingekuwa inaendanaga na utuzaji wa mazingira,mfano kupanda miti,leo hii tungekuwa mbali sana.Lakini kinyume chake watu huendekeza kunywa pombe na kuambukizana ukimwi,huu ndiyo uharibifu wa mwanadamu kwa dunia aliyoikuta
 
Moro siyo km ile ya zamani teena maji ya tiririka, imebaki mawe tuu, W-end nilipeleka watoto Rock garden aisee yamebaki mawe tuu mto hauna maji kabisa. Maji shida sana Bong'ola, Nugutu,Visole sehemu zote ni chini ya milima na hali ni mbaya sana
 
Dar - Temeke, Kata ya Toangoma

Tulivokuwa wadogo tulikuwa tumeshakariri kabisa huu ni msimu wa mvua, huu ni msimu wa kipupwe, huu ni msimu wa jua ila kipindi hiki mambo ni tofauti kabisa haijulikani ni kipind cha mvua,vuli,kipupwe wala masika ni mwendo wa jua Tu, so sad ni kwamba haya mabadiliko yanatokea kwa haraka mnoo, nawaza sijui wajukuu zetu wataishi katika ulimwengu wa namna gani

Nakumbuka kipindi cha mvua mito (Sisi tulikuwa tunaita mabwawa) yalikuwa yanafurika kwa maji tukiyatumia kuoga, Hadi kuvua samak wadogo wadogo ila sasa hv Yale mabwawa yote yamepotea kabisa nyumba zimeshajengwa maeneo hayo, hata mvua zinyeshe hayafuriki tena
 
Moro siyo km ile ya zamani teena maji ya tiririka, imebaki mawe tuu, W-end nilipeleka watoto Rock garden aisee yamebaki mawe tuu mto hauna maji kabisa. Maji shida sana Bong'ola, Nugutu,Visole sehemu zote ni chini ya milima na hali ni mbaya sana
Nimetoka Turiani majuzi yaani ni pakame ile mbaya, mvua za vuli hata dalili hakuna.
 
Back
Top Bottom