SoC04 Mabadiliko yanayotakiwa kufanyika katika stesheni za mabasi ya usafirishaji (abiria) ili kuifikia tanzania tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads

Genius46

New Member
Joined
Jun 5, 2024
Posts
1
Reaction score
1
Sekta ya usafirishaji ni moja Kati ya sekta muhimu Sana kwenye maendeleo ya nchi yetu Tanzania. Sekta hii inahusisha usafirishaji wa mizigo pamoja na abiria. Sekta hii imeonekana haina mchango mkubwa katika pato la taifa kutokana na usimamizi mbovu haswa katika Stesheni nyingi za mabasi ambapo mapato yanayokusanya hayaendi moja kwa moja katika mfumo wa serikali bali yanapitia katika mikono ya watu wachache ambao sio waaminifu.

Sekta ya usafirishaji unatakiwa ifanyiwe marekebisho makubwa Sana ili iweze kuongeza kiasi cha pato la taifa kwani inachangia kiasi kidogo Sana cha pato la taifa wakati wakati ni sekta hii Ina uwezo wa kuchangia kiasi kikubwa Sana kwani kila siku usafirishaji ( abiria na mizigo) unafanyika.

Kwa Tafiti ndogo niliyofanya katika Stesheni ya mabasi ya abiria msamvu morogoro. Nimegundua mambo matatu

Kwanza nimegundua, Asilimia kubwa ya watu wanakwepa ushuru wa tsh300/= kuingia kwenye stesheni kwa ajili ya kukata tiketi za kusafiria na badala yake wanasubiria mabasi yakitoka Getini ndipo wanapanda magari. Hali hii inapunguza mapato katika sekta ya usafirishaji.

Pili, nimegundua kwamba katika stesheni ya mabasi ya msamvu mapato mengi yanayopatikana yanaenda katika mikono ya watu na hayaingii moja kwa moja kwenye serikali kwani zile tiketi wanazopewa abiria kuingilia stesheni kwa kulipa ushuru wa 300/=huwa zinafanya kazi kwa nusu saa pekee na wanazitoa tiketi nyingi kwa wakati mmoja hivyo Kuna uwezekano mkubwa wa kufanyika udanganyifu mkubwa katika ukusanyaji wa mapato.

Tatu, nimegundua kwamba wamiliki wengi wa magari wanafanya udanganyifu kwenye malipo ya kodi ya serikali kwani wanatumia tiketi zisizo za kielektroniki ambazo wanazitengeneza wenyewe. Katika suala hili la udanganyifu wamiliki wengi wa magari wanapata mapato mengi lakini wanachangia kiasi kidogo katika pato la taifa kwakuwatoza hela kubwa abiria na kulipa kodi kidogo katika kuliongeza pato la taifa.
KIPI CHA KUFANYA,
Serikali inatakiwa itengeneze mazingira mazuri ya ukusanyaji wa mapato katika stesheni za mabasi ya abiria kwa kubadilisha vituo vya kukatia tiketi za ushuru wa tsh 300/= za kuingilia stesheni na kuwa vituo vya kukatia tiketi za kielektroniki za abiria kwa ajili ya mabasi yanayotoka katika stesheni husika. Hii itapunguza udanganyifu unaofanywa na wamiliki wa magari na hivyo kuchangia katika kuongeza pato la taifa
Katika ukataji wa tiketi za mabasi ya abiria katika stesheni zote serikali inatakiwa kuajiri wafanyakazi wake waadilifu ili kuondoa udanganyifu mkubwa unaofanywa na madereva , makondakta pamoja na wamiliki wa magari. Kwa kuajiri wafanyakazi wa serikali kukata tiketi za kielektroniki kwenye stesheni zote hii itachangia kiasi kikubwa kwenye kuongeza asilimia za ukusanyaji wa mapato kwenye sekta ya usafirishaji ili kuongeza pato la taifa kwa ujumla.
Serikali inatakiwa kuondoa ushuru wa tsh 300/= uliowekwa kama kiingilio cha abiria kuingilia katika stesheni za mabasi ya abiria zote nchini. Hii itapunguza udanganyifu mkubwa unaofanywa na abiria kwenye kukwepa kulipa ushuru na badala yake ushuru huu uunganishwe kwenye nauli za abiria ili pale abiria anapokata tiketi hapo hapo anaulipa ushuru, hii itachangia kwa kiasi kikubwa kuongeza pato la taifa katika sekta ya usafirishaji nchini.
HITIMISHO;
Serikali inatakiwa Kutoa motisha kwa uwekezaji katika sekta ya usafirishaji, Hii inaweza kujumuisha kutoa misamaha ya kodi, ruzuku, na fedha za maendeleo pia inatakiwa Kulinda haki za watumiaji wa huduma za usafirishaji, Hii itasaidia kuhakikisha kuwa wanapata huduma bora kwa bei nafuu ili kuwahamasiha kukipa kodi kwa wakati lengo likiwa kuongeza pato la taifa letu Tanzania.

Mwisho,
Kupitia makala hii na uchunguzi mdogo ambao umefanyika kwenye stesheni moja ya mabasi ya abiria msamvu morogoro hii inamaanisha kwamba stesheni zote za magari ya abiria nchini zinafanya vivyo hivyo.

Hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau wote wa maendeleo wanatakiwa kushirikiana katika kutatua matatizo haya ambayo yanaikumba sekta ya usafirishaji kama ukosefu wa mashine za kisasa za kielektroniki katika kukata tiketi kwenye stesheni nyingi nchini ambapo zinazababisha udanganyifu wakati ukusanyaji wa mapato. Upatikanaji wa hizi mashine za kisasa utaweza kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa asilimia kubwa hivyo itapelekea kuongeza pato la taifa kwa kiasi kikubwa.
 
Upvote 3
Sekta ya usafirishaji ni moja Kati ya sekta muhimu Sana kwenye maendeleo ya nchi yetu Tanzania. Sekta hii inahusisha usafirishaji wa mizigo pamoja na abiria. Sekta hii imeonekana haina mchango mkubwa katika pato la taifa kutokana na usimamizi mbovu haswa katika Stesheni nyingi za mabasi ambapo mapato yanayokusanya hayaendi moja kwa moja katika mfumo wa serikali bali yanapitia katika mikono ya watu wachache ambao sio waaminifu.

Sekta ya usafirishaji unatakiwa ifanyiwe marekebisho makubwa Sana ili iweze kuongeza kiasi cha pato la taifa kwani inachangia kiasi kidogo Sana cha pato la taifa wakati wakati ni sekta hii Ina uwezo wa kuchangia kiasi kikubwa Sana kwani kila siku usafirishaji ( abiria na mizigo) unafanyika.

Kwa Tafiti ndogo niliyofanya katika Stesheni ya mabasi ya abiria msamvu morogoro. Nimegundua mambo matatu

Kwanza nimegundua, Asilimia kubwa ya watu wanakwepa ushuru wa tsh300/= kuingia kwenye stesheni kwa ajili ya kukata tiketi za kusafiria na badala yake wanasubiria mabasi yakitoka Getini ndipo wanapanda magari. Hali hii inapunguza mapato katika sekta ya usafirishaji.

Pili, nimegundua kwamba katika stesheni ya mabasi ya msamvu mapato mengi yanayopatikana yanaenda katika mikono ya watu na hayaingii moja kwa moja kwenye serikali kwani zile tiketi wanazopewa abiria kuingilia stesheni kwa kulipa ushuru wa 300/=huwa zinafanya kazi kwa nusu saa pekee na wanazitoa tiketi nyingi kwa wakati mmoja hivyo Kuna uwezekano mkubwa wa kufanyika udanganyifu mkubwa katika ukusanyaji wa mapato.

Tatu, nimegundua kwamba wamiliki wengi wa magari wanafanya udanganyifu kwenye malipo ya kodi ya serikali kwani wanatumia tiketi zisizo za kielektroniki ambazo wanazitengeneza wenyewe. Katika suala hili la udanganyifu wamiliki wengi wa magari wanapata mapato mengi lakini wanachangia kiasi kidogo katika pato la taifa kwakuwatoza hela kubwa abiria na kulipa kodi kidogo katika kuliongeza pato la taifa.
KIPI CHA KUFANYA,

HITIMISHO;
Serikali inatakiwa Kutoa motisha kwa uwekezaji katika sekta ya usafirishaji, Hii inaweza kujumuisha kutoa misamaha ya kodi, ruzuku, na fedha za maendeleo pia inatakiwa Kulinda haki za watumiaji wa huduma za usafirishaji, Hii itasaidia kuhakikisha kuwa wanapata huduma bora kwa bei nafuu ili kuwahamasiha kukipa kodi kwa wakati lengo likiwa kuongeza pato la taifa letu Tanzania.

Mwisho,
Kupitia makala hii na uchunguzi mdogo ambao umefanyika kwenye stesheni moja ya mabasi ya abiria msamvu morogoro hii inamaanisha kwamba stesheni zote za magari ya abiria nchini zinafanya vivyo hivyo.

Hivyo serikali kwa kushirikiana na wadau wote wa maendeleo wanatakiwa kushirikiana katika kutatua matatizo haya ambayo yanaikumba sekta ya usafirishaji kama ukosefu wa mashine za kisasa za kielektroniki katika kukata tiketi kwenye stesheni nyingi nchini ambapo zinazababisha udanganyifu wakati ukusanyaji wa mapato. Upatikanaji wa hizi mashine za kisasa utaweza kuongeza ukusanyaji wa mapato kwa asilimia kubwa hivyo itapelekea kuongeza pato la taifa kwa kiasi kikubwa.
Good
 
Back
Top Bottom