Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Mabalozi wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Ulaya (EU) leo Juni 8, 2026 wamefanya mazungumzo ya kisiasa ya ngazi ya juu na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Thabit Kombo jijini Dar es Salaam.
Taarifa iliyopatilana kupitia ukurasa wa X wa Umoja wa Ulaya (EU), imesema mazungumzo yanejikita katika Haki za Binadamu na Demokrasia, ambapo umija huo umewasilisha masikitiko na wasiwasi wake kuhusu hali ya haki za binadamu na demokrasia nchini Tanzania na vipaumbele vya Sera za Kigeni.
Ajenda nyingine iliyojadiliwa ni ushirikiano kati ya EU na Tanzania utaendelea kujengwa juu ya misingi ya demokrasia, tawala wa sheria, maadili ya pamoja na maslahi ya pande zote.
Mazungumzo hayo yanakuja wakati kukiwa na shinikizo la kimataifa limeongezeka kuhusu kukamatwa kwa baadhi ya wanasiasa na wanaharakati miezi ya hivi karibuni.