Sioni hoja. Hakuna uhusiano wowote wa soko la magari ya Ulaya kuchukuliwa na magari ya Japan, na nchi za Ulaya kukazania demokrasia na utawala wa sheria.
Nchi za Ulaya na America, wana nafasi kubwa sana ya kuisadia Afrika katika kujenga tawala zenye kuheshimu utawala wa sheria, haki na katiba. Lakini wakati wanafanya hivyo wakaangalia namna watakavyoweza kuwafanya Waafrika kuwa wateja wa bidhaa zao.
Waafrika wengi wanapenda bidhaa za Ulaya na America kwa sababu ni za kiwango cha hali ya juu, lakini wanashindwa kumudu bei. Kama mataifa ya Ulaya na America wakaweza kuziuza bidhaa zao kwa bei wanayoifikia Waafrika, bidhaa za China hazitaweza kuwa mshindani katika soko kutokana na uhafifu katika ubora