Mabango ya GSM yaondolewa Uwanja wa Mkapa

Mabango ya GSM yaondolewa Uwanja wa Mkapa

Akikujibu nitag boss
Sana tu, TFF na bodi ya league kama wanaamini kisheria wako sawa na wamekuja kuambiwa na wizara wafunike kombe mwanaharamu apite basi walitakiwa waachie madaraka mara moja sababu ni udhalilishaji mkubwa chombo chochote kikishindwa kusimamia sheria hakina faida maana kesho takuja mwingine kuvunja sheria hamtakuwa na kusema. Watu walipiga chini Juventus sembuse vijitimu vyetu.

Sheria ni lazima zifuatwe na kila team bila kujali ukubwa wako. TFF kama mnaona hamna meno tena basi mresign aibu kubwa kama mnaona mko sawa basi msikubali kuvunja sheria zenu wenyewe.
 
Taarifa iliyopo mabango yametolewa kwenye vibanda vya mabenchi ya ufundi peke yake ila kwenye mzunguko wa uwanja yapo kama kawa.

IMG_3323.png

Haya mtafute GSM hapo kama yupo [emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wizara Ya Michezo Imeoza Muda Wote Ipo Kimya
kama niko sawa hiko hivi
Serikali hairuhusiwi kuingilia maswala ya tff, ikifanya hivyo tutafungiwa na fifa kushiriki mechi za kimataifa. Kama nakumbuka vzr tulishawai fungiwa enzi za fat baada ya serikali kuingilia fat. Naomba kukosolewa
 
kama niko sawa hiko hivi
Serikali hairuhusiwi kuingilia maswala ya tff, ikifanya hivyo tutafungiwa na fifa kushiriki mechi za kimataifa. Kama nakumbuka vzr tulishawai fungiwa enzi za fat baada ya serikali kuingilia fat. Naomba kukosolewa
Hapana, inaweza kuingilia.
 
Unadhani ni wateja wangapi mashabiki wa Simba kawapoteza kupitia hili seke seke la kulazimisha Simba wavae logo yake kwa mgongo wa TFF?

Tunapoongelea hili ujue kushabikia Simba au Yanga ni kama Imani ya Dini, kama ni magodoro, wapo wengi tu wanauza na hata ukitaka ya quality ya Juu kabisa wapo supplier kibao wanaleta kutoka nnje ya Nchi, upande wa nguo za watoto ndiyo kabisaa, zimejaa tele hadi viduka vya mtaani, kama ni nguo za michezo napo wapo wanaoingiza mzigo wa kutosha.

Tukija kwenye vyombo vya ndani hapo ndiyo usiseme.GSM analetaj ujuaji wakati huo huo anawahitaji hao hao mashabiki wa Simba wanunue bidhaa zake.
Kongole chane mkuu,🤝
 
Back
Top Bottom