Bibititi1
JF-Expert Member
- Sep 28, 2014
- 464
- 218
Waswahili wana msemo Tabia hushawishi kwenye kundi mkitembea wacha Mungu na wewe utakuwa mwenye kumcha Allah, mkitembea Wezi pamoja na wewe utakuwa miongoni mwa wezi, Ukitembea na viongozi bora na wewe utakuwa miongoni mwa viongozi bora.Msemo huu unaumba kwa muktadha huu.
1. Rais Samia amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Abu Dhabi Sheikh Maktoum ambaye ndiyo kiongozi mkuu wa chi za falme za kiaarabu.(UAE)
2. Rais Samia amekaa meza moja na Rais Biden, Boris Johnson PM uingereza kujadili masuala ya Dunia.
3. Rais Samia amehutubia mkutano wa baraza kuu la umoja wa Mataifa jijini New York.
4. Rais Samia amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Dunia, Rais wa Taasisi ya fedha IMF.
5. Rais Samia amehutubia mkutano maalum wa Umoja wa Ulaya.
6. Rais Samia amekutana na Makamu wa Rais Marekani.
7. Rais Samia amekutana na Rais wa Ufaransa na kufanya mazungumzo.
8. Rais Samia ameingia kwenye Jarida la watu 100 Maarufu Duniani (TIME). Akiwa miongoni mwa viongozi 100 wenye ushawishi.
9. Rais Samia ameingia kwenye Jarida la Forbes likimtaja kama kiongozi mwenye ushawishi Duniani kwa 2022.
10. Rais Samia ameingia kwenye orodha ya Jarida la The Muslims viongozi waislamu mashuhuri 500 wenye ushawishi Duniani.
11. Rais Samia amepewa Tuzo ya miundombinu bora Afrika.
12. Rais Samia amekutana na kufanya mazungumzo na mfalme wa Oman.
Haya yote yanaonyesha marafiki wa Rais Samia na kutambua tabia yake
Angelikuwa mzandiki na jeuri Ikulu ya Marekani isingempatia nafasi. Ingemtupilia mbali. Ikulu ya marekani haipo tayari kujinasibu kuwapokea wenye mikono yenye Damu.
Angelikuwa muuaji asiye penda Uhuru wa Habari pale Ufaransa majarida makubwa Duniani yangemzihaki Rais wa Ufaransa kumpokea Dikteta kwa wasiofahamu Dunia Ufaransa ndiyo kitovu cha habari Duniani manguli wakubwa wa Habari wako pale na Majarida yanayoongozwa kusomwa yapo pale.
Angelikuwa mbinafsi na katili Dubai isingempatia ukarimu ule wa hali ya juu kwa wasiofahamu Dubai ndiyo kitovu cha Utalii na Ukarimu kwa sasa Duniani sheikh Maktoum asingekuwa tayari kuipoteza hadhi yake hata kidogo.
Angelikuwa mkandamizaji wa haki za jinsia abadani asingeipata meza ya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Marekani Bi. Kamala Harris
Angelikuwa mtu fisadi na mfujaji wa pesa za Umma kamwe asingeipata nafasi ya kukaa kwenye mkutano maalum na Rais wa Benki ya Dunia wala kuhudhuria mkutano maalum wa Taasisi ya fedha duniani IMF.
Angelikuwa mwenye kuyakanyaga mahusiano ya mataifa au asiyejali diplomasia asingepewa mimbari katika mkutano wa Umoja wa chi za ulaya kwani mtu asiyejali Diplomasia hana hadhi kwenye mabaraza ya watu wenye heshima.
Matone machache ya mvua za chuki za hapahapa na pale hayawezi kuichafua bahari ya Wema wa Rais Samia Suluhu Hassan na Dunia inalitambua hilo.
Moyo wake Sultani asiyetamani cha mtu nyumba alikabidhiwa ingali chafu yenye kunguni wa dhiki na kiu ya maendeleo mwachenni atoke na atekeleze kwa faida ya wenetu. Rais Samia ni matoekeo ya Dua zetu njema mtu mwema roho yake ana kivuli chake kesho katika Imani yake kwenye siku ya hesabu.
kiogompina@hotmail.com