Mabasi aina ya Scania na Mercedes Benz vs Yutong na Zongtong: Mchina ameuza ramani ya vita kwa adui

Mabasi aina ya Scania na Mercedes Benz vs Yutong na Zongtong: Mchina ameuza ramani ya vita kwa adui

Myth!
Kwenye real world Mercedes haina uimara huo, Yap zamani walitamba Sana kwa kuwa walikuwa wa kwanza kutengeneza magari , lakini Kuna watu wapo serious kwenye hiyo baishara, huoni basi nyingi za Mercedes kwa sababu Ni sumbufu! Hata south Africa ambao walijatibu basi za Mercedes translux na city to city wengi waliangukia pua, sababu they are serious underpowered and they don't last long!!
Kwa faida ya wengi, tunaomba ufafanue "drive train" ni Nini na inafanyeje kazi?
 
...kwa watu wenye kuijua hii biashara hawezi kuhangaika na gari ya kichina

Nimeingia stand ya mkoa Ubungo last week nikaona Abood amepanga YUTONG kama nane hivi, mchanganyiko wa single na double axle, sasa sijui Abood nae hajui biashara ya magari??

Halafu nikisikia mtu mzima anaongelea sifa ya spidi ya gari nakuona bado hujakomaa, bado infantile...

Vyombo vya biashara , basi, treni, ndege, tanker la mafuta, meli, vinaenda na ratiba iliyopangwa kibiashara na kiserikali, sio kwa sababu havina mbio. Sasa basi la Dar Bukoba likiwahi kufika leo leo ndio litageuza leo, leo jioni??? Litaondoka na mteja usiku??
 
Miaka ya nyuma Scania ndio alikuwa mfalme wa kusafirisha abiria na mizigo hapa nchini. Wamiliki wa mabasi waliziamini sana Scania kwa uimara wake na mwendo barabarani.

Miaka ya katikati Mchina akaleta mabasi ya YUTONG na Zongtong. Matajiri wengi wakazimbilia basi hizi kwasababu ya ulaji mdogo wa mafuta, bodi nzuri, interior design, na unafuu wa vipuri..
Pamoja na hayo lakini kuna hujma kubwa sana kuna kampuni kama Rungwe, New force na Dar Lux wameungana kumpiga vita.
 
Mchina yule yule wa tecno,itel na infinix ndiye yule yule wa zhongtong,higher,youtong hajawahi kuwa serious kwenye kazi.

Basi kama lake linauzwa mil 900,yeye anaunda lake anauza ml 250,halafu mtu anakuja kubeza scania/benz/volvo si lolote si chochote,basi unamuangalia halafu unfanya ihiiiiiiiiiiiiiiiiiiii(kwa sauti ya magu).
Scania ni hatari sana mkuu
 
Nimeingia stand ya mkoa Ubungo last week nikaona Abood amepanga YUTONG kama nane hivi, mchanganyiko wa single na double axle, sasa sijui Abood nae hajui biashara ya magari ???

Halafu nikisikia mtu mzima anaongelea sifa ya spidi ya gari nakuona bado hujakomaa, bado infantile...

Vyombo vya biashara , basi, treni, ndege, tanker la mafuta, meli, vinaenda na ratiba inayokwambia hii basi inafika mwisho wa njia saa fulani, ndio imepangwa hivyo kibiashara na kiserikali, sio kwa sababu havina mbio. Sasa basi la Dar Bukoba likiwahi kufika leo leo ndio litageuza leo, leo jioni??? Litaondoka na mteja usiku ???
Abood na shabiby wanabebwa na geographical location walizopo, hizo basi zote ulizoziona hapo hakuna hata moja inayotanya safari ya Zaid ya masaa manne, zinapata muda wa kupumzika na check up ya kutosha same applies to shabiby,

Batch ya abood terias zilianza kuja superfeo akafatia lakini nyingi zilisumbua zamani Sana na nyingi hazipo barabarani.
Kiufupi mkuu route ya dar Moro haichoshi gari na ndo mana abood anaendelea mbele.

Sent
 
Miaka ya nyuma Scania ndio alikuwa mfalme wa kusafirisha abiria na mizigo hapa nchini. Wamiliki wa mabasi waliziamini sana Scania kwa uimara wake na mwendo barabarani.

Miaka ya katikati Mchina akaleta mabasi ya YUTONG na Zongtong. Matajiri wengi wakazimbilia basi hizi kwasababu ya ulaji mdogo wa mafuta, bodi nzuri, interior design, na unafuu wa vipuri...
Wakazimbilia ndio nini.
Tatizo mnaandika mkiwa mmepiga faru john.
 
China vs Europe, Machina hawezi vitu, the master of copy cat kama to @mo Dewji
 
Unataka kusema nn. Mabasi yote yamefungwa speed limit, barabarani Kuna touch, huo mwendo Ni upi? Issue kubwa hapo Ni unafuu wa manunuzi na uendeshaji wa mabasi ya kichina basi
Ndio yamefungwa vts lakini shughuli inaanzia mikumi ambapo ndio vilima huanza maana gari za kichina kwenye kupanda sio kivile
 
Kuna Mabasi sijui yana injini za treni nakumbuka siku moja tunatoka dar tunaenda mbeya tukakuta jam zito lililokuwa linaanzia kwa msuguri mpaka maili moja ikabidi tupite njia ya tegeta totokee kibaha mbele zaidi ya maili moja.

Kabla ya kuibukia barabara kuu kibaha kuna sehemu tulikuta barabara inatengenezwa ipo katika hali vumbi na mvua ilinyesha asubuhi ile kukawa na utelezi ile barabara pia ina kilima kikali Mabasi yakawa yanaserereka likiwemo Marco polo letu.

Mara nikaona basi moja Scania jeupe hivi likiwa linapanda kile kilima kama hamna matope nikashangaa sana maana Mabasi yalikuwa yako kwenye fulani ya kuserereka lenyewe likawa linatuovertake tu.
 
Myth!
Kwenye real world Mercedes haina uimara huo, Yap zamani walitamba Sana kwa kuwa walikuwa wa kwanza kutengeneza magari , lakini Kuna watu wapo serious kwenye hiyo baishara, huoni basi nyingi za Mercedes kwa sababu Ni sumbufu! Hata south Africa ambao walijatibu basi za Mercedes translux na city to city wengi waliangukia pua, sababu they are serious underpowered and they don't last long!!

Mercedes nyingi zinafanya vizuri zikiwa mpya 0km to 700000 huko baada ya hapo tegemea majanga , swedish zipo vizuri Hadi second life zikija africa unazungumzia km Hadi milioni kadhaa...
Mkuu kuhusu benzi south huwambii kitu wanapenda sana benz hao watu nikuwambie tu na kudumu benz usiseme
 
Scania ni hatari sana mkuu
Wababe wa kusini
IMG-20200610-WA0200.jpeg
IMG-20200611-WA0006.jpeg
IMG-20200610-WA0191.jpeg
 
Pamoja na hayo lakini kuna hujma kubwa sana kuna kampuni kama rungwe new force na dar lux wameungana kumpiga vita

Tatizo la mchina ujeuri mwingi alijiamini sana na hizi golden deer zake. Akiamini ndiyo kiboki ya scania ko akawa hataki hata kidogo kuenda sawa na wenzake

mfano. Route ya Kyela-DSM watatu yaani rungwe kyela na majinja walikubaliana ziwe zinaondoka kampuni mbili na kurudi kampuni mbili yaani kama leo kutoka kyela kwenda dsm iondoke kyela na new force na kutoka DSM kuja kyela zije rungwe na majinjah ingeleta ufanisi wa biashara mchina akagoma ikabaki kung’ang’aniana abiria sasa tabu yake yeye tukuyu hadi iringa nauli ni elfu 30 wakati akina majinjah hata buku 10 wanabeba. Mwisho wa siku kaishia kuomba poo na sasa hana hii route.
 
Back
Top Bottom