Mabasi aina ya Scania na Mercedes Benz vs Yutong na Zongtong: Mchina ameuza ramani ya vita kwa adui

Kwa faida ya wengi, tunaomba ufafanue "drive train" ni Nini na inafanyeje kazi?
 
...kwa watu wenye kuijua hii biashara hawezi kuhangaika na gari ya kichina

Nimeingia stand ya mkoa Ubungo last week nikaona Abood amepanga YUTONG kama nane hivi, mchanganyiko wa single na double axle, sasa sijui Abood nae hajui biashara ya magari??

Halafu nikisikia mtu mzima anaongelea sifa ya spidi ya gari nakuona bado hujakomaa, bado infantile...

Vyombo vya biashara , basi, treni, ndege, tanker la mafuta, meli, vinaenda na ratiba iliyopangwa kibiashara na kiserikali, sio kwa sababu havina mbio. Sasa basi la Dar Bukoba likiwahi kufika leo leo ndio litageuza leo, leo jioni??? Litaondoka na mteja usiku??
 
Pamoja na hayo lakini kuna hujma kubwa sana kuna kampuni kama Rungwe, New force na Dar Lux wameungana kumpiga vita.
 
Scania ni hatari sana mkuu
 
Abood na shabiby wanabebwa na geographical location walizopo, hizo basi zote ulizoziona hapo hakuna hata moja inayotanya safari ya Zaid ya masaa manne, zinapata muda wa kupumzika na check up ya kutosha same applies to shabiby,

Batch ya abood terias zilianza kuja superfeo akafatia lakini nyingi zilisumbua zamani Sana na nyingi hazipo barabarani.
Kiufupi mkuu route ya dar Moro haichoshi gari na ndo mana abood anaendelea mbele.

Sent
 
Wakazimbilia ndio nini.
Tatizo mnaandika mkiwa mmepiga faru john.
 
China vs Europe, Machina hawezi vitu, the master of copy cat kama to @mo Dewji
 
Unataka kusema nn. Mabasi yote yamefungwa speed limit, barabarani Kuna touch, huo mwendo Ni upi? Issue kubwa hapo Ni unafuu wa manunuzi na uendeshaji wa mabasi ya kichina basi
Ndio yamefungwa vts lakini shughuli inaanzia mikumi ambapo ndio vilima huanza maana gari za kichina kwenye kupanda sio kivile
 
Kuna Mabasi sijui yana injini za treni nakumbuka siku moja tunatoka dar tunaenda mbeya tukakuta jam zito lililokuwa linaanzia kwa msuguri mpaka maili moja ikabidi tupite njia ya tegeta totokee kibaha mbele zaidi ya maili moja.

Kabla ya kuibukia barabara kuu kibaha kuna sehemu tulikuta barabara inatengenezwa ipo katika hali vumbi na mvua ilinyesha asubuhi ile kukawa na utelezi ile barabara pia ina kilima kikali Mabasi yakawa yanaserereka likiwemo Marco polo letu.

Mara nikaona basi moja Scania jeupe hivi likiwa linapanda kile kilima kama hamna matope nikashangaa sana maana Mabasi yalikuwa yako kwenye fulani ya kuserereka lenyewe likawa linatuovertake tu.
 
Mkuu kuhusu benzi south huwambii kitu wanapenda sana benz hao watu nikuwambie tu na kudumu benz usiseme
 
Pamoja na hayo lakini kuna hujma kubwa sana kuna kampuni kama rungwe new force na dar lux wameungana kumpiga vita

Tatizo la mchina ujeuri mwingi alijiamini sana na hizi golden deer zake. Akiamini ndiyo kiboki ya scania ko akawa hataki hata kidogo kuenda sawa na wenzake

mfano. Route ya Kyela-DSM watatu yaani rungwe kyela na majinja walikubaliana ziwe zinaondoka kampuni mbili na kurudi kampuni mbili yaani kama leo kutoka kyela kwenda dsm iondoke kyela na new force na kutoka DSM kuja kyela zije rungwe na majinjah ingeleta ufanisi wa biashara mchina akagoma ikabaki kung’ang’aniana abiria sasa tabu yake yeye tukuyu hadi iringa nauli ni elfu 30 wakati akina majinjah hata buku 10 wanabeba. Mwisho wa siku kaishia kuomba poo na sasa hana hii route.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…