Mabasi aina ya Scania na Mercedes Benz vs Yutong na Zongtong: Mchina ameuza ramani ya vita kwa adui

Sio kwamba wanaotumia mabasi ya kichina hawana akili, naweza kusema hawana taarifa kamili , milioni 900 ni nyingi sana , ilq basi ya 250 mil inapoanza kuzingua ilhali bado ni mpya nayo ni nightmare.
Basi sita mpya marcopolo g series za superfeo ni karibu bilioni sita , unaongelea karibu basi 20 za kichina hapo, superfeo amekua muumini wa fleets za kichina toka anaanza biashara ya mabasi makubwa jiulize kwanini ameamua kufanya Expensive U turn . Angeweza kuongeza mabasi 20 ya zhongtong, lakini asingeweza kutangaza route ya songea mwanza , songea moshi au mbamba bay dar kwa fleets za kichina.
 
Mkuu L 360 Dongfeng Cummins ni euro 2 na f95 -310 HB ni euro 3

Kwa bongo hamna Buses zenye Carbon Emissions euro 5.
Kweli kabisa
Unajua by the time naandika nilikuwa nina reference ya 95 , ya ulaya, ambayo ni purely euro 5, huku kwetu kumbe kuna agreement ilifanywa kutokana na mafuta yetu tunayotumia kuwa na high sulphur content , hakuna gari mpya inayouzwa huku kwetu ambayo ni euro 5, zote ni euro 3 hata hiI next gen ni euro 3.
 
Abood analeta

Youtong kwa sababu route yake ni fupi mno, location yake ya biashara inambeba sana ,
Uko sahihi, Dar - Morogoro ni kilometa 194, akienda na kurudi ni 392. Hazitachoka mapema.
Abood bado anapelekea Marcopolo Mwanza na Tunduma zenye namba A, ndo uone ugumu wa Scania. 😀 😀 😀
 
Isuzu ilikuwa ni MV 118,CVR zilikuja special kwa lori na mv 118 zilikuwa na piston10 wakati cvr ni6
 
Mmmh abiria ndiye anaeku-remote,sasa kama spidi haijalishi ni kwanini wanatengeneza injini zenye hp kubwa?kuna haja gani ukizingatia ukubwa wa injini unaendana na ulaji wa mafuta je wanapenda hasara?
 
Isuzu ilikuwa ni MV 118,CVR zilikuja special kwa lori na mv 118 zilikuwa na piston10 wakati cvr ni6
Mkuu, you might want to make corrections to your post kama ikikupendeza
Isuzu Mv 118 haikuwahi kuwa na engine ya piston 10, bali ilikuwa na straight six engine with natural aspiration.
Basi hizo alikuwa nazo, saddiq line (moro dar) likungu bus( dar songea ) Raha leo (dar Tanga) Mwendo wa saa, (dar songea) Matema beach( Dar kyela) Tawaqal (Dar mbeya) Safina (Dar mbeya) n.k baadaye Mv 118 ilikuja kuwa replaced na the turbocharged intercooled Mv 123, Mv 123 hazikuwa popular huku kwetu , na hata kenya pia ,maana Kenya ndo walikuwa wameanza kuzielewa scania if my memory serve me correct nadhani Mv123 nimeiona kwa Raha leo peke yake.
Uwe na usiku mwema!!!
 
Tawaqal(dar-tunduma) hajawahi kuwa na mv 118 mkuu fuatilia ila hao wengine sawa na akina meridian,bembea,confort,lucky star,ilangamoto,special coach nk also owned mv 118.
 
I cannot be corrected when Iam right sir,u have to ask those who knows much about the vehicle,without going deep technically one simple thing I give u is to hear how it sounds mkuu.View attachment 1995167
Haha !
Document yako inaongelea cars not trucks , nadhan huu uzi upo zaidi kwenye mabasi , sikutarajia kuwa ungeleta maongezi ya magari madogo

Mv118 ilikuwa ni model ya basi na sio engine code , nikipata wasaa nitakuwekea engine code za engine hiyo
 
Tawaqal(dar-tunduma) hajawahi kuwa na mv 118 mkuu fuatilia ila hao wengine sawa na akina meridian,bembea,confort,lucky star,ilangamoto,special coach nk also owned mv 118.
Inawezekana najibushana na mtu wa enzi hizi
Tawaqal amewahi kuwa na isuzu , na nimepanda basi hiyo mara kadhaa, nakumbuka nilikuwa siipendi kwa sababu haikuwa na mwendo ilikuwa inafika dar kwa kuchelewa saa tisa alasiri, kama sikosei namba TZJ 7110,

Enzi hizo Masia bus inaingia mnazi mmoja saa nane alasiri kutokea mbeya .
 
Saa nane? Aisee

Siku hz zinafika saa moja tunaona zinakimbia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Saa nane? Aisee

Siku hz zinafika saa moja tunaona zinakimbia [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Saa nane mkuu , enzi hizo Radio one stereo ndo inaanza , ilikuwa mtu ukikiwahi kipindi cha dj show ya kina mike mhagama na blandina mungezi unajiona bingwa
Masia , Tawaqal, matema beach ndo zilikuwa badi za kuingia mida hiyo ya kibabe
Siku hizi ati inatamba sauli kwa kuingia saa moja Dar , ..what a joke!!!
 
Mpaka mbishi dar express kadaka Zhongtong Climber[emoji38][emoji38][emoji38]
 
Kwann tunarud nyuma sasa badala ya kwenda mbele? Nilidhan baada ya miundombinu kua bora mambo yangekua bora zaid
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…