Mabasi Dar yaruhusiwa kushusha vituo binafsi

Mabasi Dar yaruhusiwa kushusha vituo binafsi

Asingeweza vita na mabilionea wa mjengoni kina madelu, abood shabiby na wengineo nadhan amegundua alidandia mtumbwi vibwengo ameamua kuchumpa kwa ustad mkubwa
 
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla, ameondoa katazo lililokuwa likizuia mabasi yaendayo mikoani kutoruhusiwa kupakia abiria au kushusha katika vituo binafsi na badala yake ameruhusu utaratibu huo kuendelea kwa sharti la kila basi kuingia ndani ya kituo kikuu cha Magufuli.

RC Makalla ametoa maamuzi hayo wakati wa kikao cha pamoja baina ya LATRA, wamiliki wa stendi binafsi na Halmashauri ya Ubungo na kubaini pasipokuwa na shaka kuwa waliotengeneza vituo binafsi walifuata taratibu na kupatiwa vibali na LATRA baada ya kukidhi vigezo.

Miongoni mwa vigezo vilivyotolewa na LATRA ili kuruhusiwa kuanzisha stendi binafsi ni pamoja na uwepo wa vyoo, sehemu ya mapumzimo kwa abiria, viburudisho na sehemu ya maegesho.

Kutokana na hilo RC Makalla ameridhia vituo binafsi vitano vilivyohakikiwa kuendelea kutoa huduma na kufungua milango kwa wamiliki wengine wanaohitaji kuwa na vituo binafsi kushirikiana na LATRA ili wapatiwe vigezo vinavyohitajika ambapo wamepewa mamlaka ya kufuta au kutoa leseni.

Aidha RC Makalla ameagiza Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kukaa kikao mara moja na wamiliki wa stendi binafsi ili kuona njia bora ya ukusanyaji wa mapato.
Uamuzi mzuri.
Utasaidia pia kupunguza kero ya WapigaDebe
 
Machinga wameteswa sana nchi hii,hawathaminiwi,Mali zao zimeharibiwa,wameitwa kila aina ya majina mabaya.
Wamenyanganywa Mali zao mwisho wa siku wametengewa maeneo yao.....lakini wamerudi na wanauzia maeneo yao ya zamani.
swali: Je serikali huwa inakurupuka katika maamuzi ya baadhi ya mambo yenye kuhitaji umakini?

Mfano: stendi zimejengwa nchi nzima isipokuwa bukoba....ila utaratibu wa uendeshaji wa hizo stendi ni wizi,unyanganyi,vitisho na kubebeshana misalaba....why?
Hili suala Hata mjinga atalipatia...iko hivi, abiria washukie kwenye vituo vyovyote vile kulingana na eneo analoona ni sahihi then bus Hata likiwa tupu liingie stendi kuu. Just simple as that.
Ila bukoba Stand cjui itakuja lini
Mji mdogo na Stand ndogo

Sent from my TECNO KG6 using JamiiForums mobile app
 
Wale mliokuwa mnapinga kanuni hii sijui sasa hivi mnajisikiaje.

Wacheni roho za mawe.
 
Back
Top Bottom