SoC04 Mabasi maalum kutatua changamoto za usafiri kwa wafanyakazi

Tanzania Tuitakayo competition threads

Kidaya

Senior Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
108
Reaction score
95
Kutokana na ukuaji wa miji na majiji, wafanyakazi wengi wanaishi (kujenga makazi au kupanga) maeneo ya mbali kidogo (zaidi ya kilomita kumi) kutoka maeneo wanayofanyia kazi hali inayowalazimu uhitaji wa usafiri wa kwenda kazini na kurudi nyumbani. Kwa mfano katika jiji la Mwanza, wafanyakazi wengi wanaofanya kazi maeneo ya mjini kati (city center), wanaishi maeneo ya Buhongwa, Usagara, Igoma, Kisesa, Kiseke, Buswelu nk. ambapo ni takribani kilomita ishirini kutoka mjini kati. Baadhi ya wafanyakazi wanalazimika kununua magari ili waweze kuwahi kazini na kurudi majumbani kwao huku wengi wao wakitegemea usafiri wa umma (daladala, bajaji na bodaboda) katika safari za kwenda kazini kila siku.
Changamoto za usafiri binafsi
Usafiri binafsi wa kwenda kazini una changamoto zinazoathiri ustawi wa wafanyakazi, uzalishaji wao, na ubora wa maisha kama;
• Gharama kubwa za uendeshaji wa chombo cha usafiri zinazotokana na matumizi ya mafuta na gharama za matengenezo na huduma (service) za mara kwa mara kutokana na uchakavu wa haraka.
• Kuongezeka kwa msongamano wa magari barabarani kutokana na kila mfanyakazi kwenda kazini na gari lake binafsi katika barabara chache zilizopo, hali inayoongeza hatari ya kupata ajali, na husababisha kuchelewa kazini hivyo kuathiri uzalishaji na kuongeza msongo wa mawazo kwa wafanyakazi.
• Uchovu wa dereva kutokana na kuwahi kuamka alfajiri ili kuwahi foleni, kushinda kazini siku nzima na kuchelewa kutoka kazini ili kusubiri foleni ipungue husababisha dereva kupoteza umakini barabarani, hali inayoongeza uwezekano wa kupata ajali na kuathiri utendaji kazi wa mfanyakazi.​
Ajali ya gari niliyoipata tarehe 11 Mei 2024 baada ya kusinzia nikiwa naendesha gari kutokana na uchovu

• Kupoteza muda wa familia na wa kushiriki matukio ya kijamii kutokana na kuamka mapema sana ili kuwahi foleni na kuchelewa kurudi nyumbani wakisubiri foleni ipungue.
• Uhaba wa muda wa burudani na kupumzika kutokana na muda mwingi unaotumika barabarani, hivyo kuathiri afya zao ya kiakili na ubora wa maisha.
• Matumizi ya magari binafsi mengi barabarani kila siku huongeza utoaji wa moshi hatarishi kwa mazingira hivyo kuchangia uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya tabianchi.
Changamoto za Usafiri wa Umma
Usafiri wa umma uliopo sasa katika miji mikubwa na majiji nchini una changamoto kama;
• Msongamano wa watu kutokana na daladala, bajaji na bodaboda kubeba watu wengi kupita uwezo wa chombo. Hali hii huwaweka wasafiri katika hatari ya kupata madhara makubwa endapo ikitokea ajali, huwaongezea wasafiri uwezekano wa kuambukizana magonjwa kama vile mafua na kupelekea wasafiri kuwa na msongo wa mawazo.
• Usalama mdogo wa mali za wasafiri kutokana na msongamano mkubwa katika vituo vya usafiri na kwenye vyombo vya usafiri. Wasafiri wengi hujikuta wakiibiwa na kupoteza mali zao kama simu, pochi na mizigo yao.​
Changamoto za usafiri wa umma Dar (picha kutoka ukurasa wa gazeti la mwananchi)

• Ratiba zisizo thabiti za huduma za usafiri wa umma kuwa usafiri unaanza saa ngapi na unaisha saa ngapi, hali inayosababisha wasafiri kukosa huduma ya usafiri hasa nyakati za usiku au kuchelewa sana kurudi nyumbani.
• Upotevu wa muda wa kusubiria usafiri na wakati wa safari huwasabibishia wasafiri msongo wa mawazo na kupelekea ugomvi mara kwa mara baina ya wasafiri, wasafiri na watoa huduma, na wasafiri na wanafamilia zao. Muda unaopotea pia huwachelewesha wasafiri katika shughuli za uzalishaji mali.
• Magari ya usafiri wa umma mara nyingi ni ya zamani na yamechakaa, na hivyo kuhatarisha usalama wa abiria. Magari mengi hayana vifaa vya kustarehesha kama vile kiyoyozi na TV, hivyo kufanya safari kuwa za kero.
• Uvunjaji wa sheria za usalama barabarani na za usafirishaji kama vile kuendesha kasi, kupakia abiria kupita kiasi, kupakia abiria na mizigo, kuendesha magari bila leseni, kuweka sauti kubwa sana ya mziki na kukatisha njia (route). Haya huongeza uwezekano wa ajali na kusababishia usumbufu kwa wasafiri.

Utatuzi wa changamoto za usafiri kwa wafanyakazi
Kuwa na mabasi maalum kutaboresha usafiri kwa wafanyakazi kwa kutoa huduma zenye ufanisi, usalama na za kuaminika kama ifuatavyo;
• Kupunguza Msongamano wa magari: Kubeba wafanyakazi katika idadi ndogo ya mabasi maalum kutapunguza sana idadi ya magari binafsi barabarani. Hii itapunguza msongamano wa magari na kupelekea muda mfupi wa kusafiri kwa watumiaji wote wa barabara.
• Kuongeza Tija: Kuwa na usafiri bora na wa wakati, kutasaidia wafanyakazi kuongeza uzalishaji kazini, kwani wafanyakazi watatumia muda mdogo kuhangaikia safari za kila siku na muda mwingi kujikita katika kazi zao.
• Faida za Mazingira: Uwepo wa magari machache barabarani kutapunguza utoaji wa gesi chafuzi kwa mazingira hivyo kuendana na malengo ya maendeleo uendelevu (SDG) namba 11 na 13.
• Akiba ya Kiuchumi: Wafanyakazi watapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za kutumia usafiri binafsi kuendea kazini hivyo kuwa na akiba za kiuchumi watakazozitumia katika majukumu mengine ya kimaisha na maendeleo.
• Usalama na Faraja: Mabasi maalum yatawaongezea usalama wafanyakazi kwa kuwaepusha kuendesha vyombo vya moto wakiwa na uchovu na msongo wa mawazo.
Mikakati ya Utekelezaji
• Ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi (PPPs): Serikali kutoa vibali na usimamizi kwa sekta binfasi kumiliki mabasi na kutoa huduma hii kwa kuwafuata wafanyakazi katika vituo jirani na makazi yao na kuwapeleka makazini, kutahakikisha utoaji wa huduma kwa ufanisi na uendelevu.
• Programu za majaribio: Kuanza utekelezaji wa mradi huu katika maeneo yenye wafanyakazi wengi kama hospitali za kanda, mikoa kutasaidia kutathmini uwezekano na ufanisi wa mradi. Maoni kutoka kwa majaribio haya yatasaidia kuboresha ubora na kuongeza wigo wa utoaji huduma.
• Nauli za mabasi maalum: Ili kumudu gharama za uendeshaji, nauli inaweza kuwa mara mbili ya nauli ya daladala. Mfano kwa Mwanza, kutoka Kisesa hadi hospitali ya Bugando nauli ni tsh 1,300. Nauli ya basi maalum inaweza kuwa Tsh. 2,500 kwa safari moja na Tsh. 5,000 kwenda na kurudi. Nauli hii ni nafuu sana (1/3) kwa mfanyakazi anaetumia wastani wa Tsh. 15,000 kama gharama ya mafuta ya kwenda kazini na kurudi nyumbani kwa siku. Malipo yanaweza kufanyika kwa wiki au kwa mwezi kwa akaunti ya lipa namba au akaunti za benki ili kupunguza usumbufu wa kukusanya nauli.
• Muunganiko wa Teknolojia: Kuwa na mfumo wa kiteknolojia wa kufuatilia mahali basi lilipo (GPS) ili kupunguza muda wa kusubiria barabarani na kupokea taarifa kuhusu ratiba za usafiri na maoni ya wateja.

Mabasi maalum yatatatua kwa kiasi kikubwa changamoto za wafanyakazi za kutumia usafiri binafsi na usafiri wa umma uliopo sasa. Mafanikio ya mradi huu yatasaidia mradi huu kuongeza wigo wa kuhudumia makundi mengine.
 
Upvote 30
Matumizi ya magari binafsi mengi barabarani kila siku huongeza utoaji wa moshi hatarishi kwa mazingira hivyo kuchangia uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya tabianchi.
Magari binafsi mengine ni mazito sana kwa shughuli za mjini. Ni kama kutumia..... ngoja hii picha inajieleza vizuri.
Screenshot_20240509-110004_Chrome.jpg

Yaani inakuwa hasara kutumia nguvu kubwa kujaza nafasi kisa tu kusafirisha mtu mmoja.

Muunganiko wa Teknolojia: Kuwa na mfumo wa kiteknolojia wa kufuatilia mahali basi lilipo (GPS) ili kupunguza muda wa kusubiria barabarani na kupokea taarifa kuhusu ratiba za usafiri na maoni ya wateja.
Nzuri sana, unajua kabisa basi la saa tatu lipo pale, nikilikosa hili la saa tatu unusu bado liko mbali. Bora niwahi kituoni
Mabasi maalum yatatatua kwa kiasi kikubwa changamoto za wafanyakazi za kutumia usafiri binafsi na usafiri wa umma uliopo sasa
Umegusia kitu muhimu sana. Hili ni suluhisho la mambo mengi tu. Nimekosa picha ningeweka...... anyway ngoja niitafute maana inakazia maelezo uliyoyaweka.
Screenshot_20240524-175259_Chrome.jpg

Asee insha nzuri sana👏
 
Magari binafsi mengine ni mazito sana kwa shughuli za mjini. Ni kama kutumia..... ngoja hii picha inajieleza vizuri.
View attachment 2998280
Yaani inakuwa hasara kutumia nguvu kubwa kujaza nafasi kisa tu kusafirisha mtu mmoja.

Nzuri sana, unajua kabisa basi la saa tatu lipo pale, nikilikosa hili la saa tatu unusu bado liko mbali. Bora niwahi kituoni

Umegusia kitu muhimu sana. Hili ni suluhisho la mambo mengi tu. Nimekosa picha ningeweka...... anyway ngoja niitafute maana inakazia maelezo uliyoyaweka.
View attachment 2998284
Asee insha nzuri sana👏
Asante mkuu kwa kuniongezea ushahidi, 70 people in bus vs car
 
Kutokana na ukuaji wa mjiji na majiji, wafanyakazi wengi wanaishi (kujenga makazi au kupanga) maeneo ya mbali kidogo (zaidi ya kilomita kumi) kutoka maeneo wanayofanyia kazi hali inayowalazimu uhitaji wa usafiri wa kwenda kazini na kurudi nyumbani. Kwa mfano katika jiji la Mwanza, wafanyakazi wengi wanaofanya kazi maeneo ya mjini kati (city center), wanaishi maeneo ya Buhongwa, Usagara, Igoma, Kisesa, Kiseke, Buswelu nk. ambapo ni takribani kilomita ishirini kutoka mjini kati. Baadhi ya wafanyakazi wanalazimika kununua magari ili waweze kuwahi kazini na kurudi majumbani kwao huku wengi wao wakitegemea usafiri wa umma (daladala, bajaji na bodaboda) katika safari za kwenda kazini kila siku.
Changamoto za usafiri binafsi
Usafiri binafsi wa kwenda kazini una changamoto zinazoathiri ustawi wa wafanyakazi, uzalishaji wao, na ubora wa maisha kama;
• Gharama kubwa za uendeshaji wa chombo cha usafiri zinazotokana na matumizi ya mafuta na gharama za matengenezo na huduma (service) za mara kwa mara kutokana na uchakavu wa haraka.
• Kuongezeka kwa msongamano wa magari barabarani kutokana na kila mfanyakazi kwenda kazini na gari lake binafsi katika barabara chache zilizopo, hali inayoongeza hatari ya kupata ajali, na husababisha kuchelewa kazini hivyo kuathiri uzalishaji na kuongeza msongo wa mawazo kwa wafanyakazi.
• Uchovu wa dereva kutokana na kuwahi kuamka alfajiri ili kuwahi foleni, kushinda kazini siku nzima na kuchelewa kutoka kazini ili kusubiri foleni ipungue husababisha dereva kupoteza umakini barabarani, hali inayoongeza uwezekano wa kupata ajali na kuathiri utendaji kazi wa mfanyakazi.​
View attachment 2998050
• Kupoteza muda wa familia na wa kushiriki matukio ya kijamii kutokana na kuamka mapema sana ili kuwahi foleni na kuchelewa kurudi nyumbani wakisubiri foleni ipungue.
• Uhaba wa muda wa burudani na kupumzika kutokana na muda mwingi unaotumika barabarani, hivyo kuathiri afya zao ya kiakili na ubora wa maisha.
• Matumizi ya magari binafsi mengi barabarani kila siku huongeza utoaji wa moshi hatarishi kwa mazingira hivyo kuchangia uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya tabianchi.
Changamoto za Usafiri wa Umma
Usafiri wa umma uliopo sasa katika miji mikubwa na majiji nchini una changamoto kama;
• Msongamano wa watu kutokana na daladala, bajaji na bodaboda kubeba watu wengi kupita uwezo wa chombo. Hali hii huwaweka wasafiri katika hatari ya kupata madhara makubwa endapo ikitokea ajali, huwaongezea wasafiri uwezekano wa kuambukizana magonjwa kama vile mafua na kupelekea wasafiri kuwa na msongo wa mawazo.
• Usalama mdogo wa mali za wasafiri kutokana na msongamano mkubwa katika vituo vya usafiri na kwenye vyombo vya usafiri. Wasafiri wengi hujikuta wakiibiwa na kupoteza mali zao kama simu, pochi na mizigo yao.​
View attachment 2998051
• Ratiba zisizo thabiti za huduma za usafiri wa umma kuwa usafiri unaanza saa ngapi na unaisha saa ngapi, hali inayosababisha wasafiri kukosa huduma ya usafiri hasa nyakati za usiku au kuchelewa sana kurudi nyumbani.
• Upotevu wa muda wa kusubiria usafiri na wakati wa safari huwasabibishia wasafiri msongo wa mawazo na kupelekea ugomvi mara kwa mara baina ya wasafiri, wasafiri na watoa huduma, na wasafiri na wanafamilia zao. Muda unaopotea pia huwachelewesha wasafiri katika shughuli za uzalishaji mali.
• Magari ya usafiri wa umma mara nyingi ni ya zamani na yamechakaa, na hivyo kuhatarisha usalama wa abiria. Magari mengi hayana vifaa vya kustarehesha kama vile kiyoyozi na TV, hivyo kufanya safari kuwa za kero.
• Uvunjaji wa sheria za usalama barabarani na za usafirishaji kama vile kuendesha kasi, kupakia abiria kupita kiasi, kupakia abiria na mizigo, kuendesha magari bila leseni, kuweka sauti kubwa sana ya mziki na kukatisha njia (route). Haya huongeza uwezekano wa ajali na kusababishia usumbufu kwa wasafiri.

Utatuzi wa changamoto za usafiri kwa wafanyakazi
Kuwa na mabasi maalum kutaboresha usafiri kwa wafanyakazi kwa kutoa huduma zenye ufanisi, usalama na za kuaminika kama ifuatavyo;
• Kupunguza Msongamano wa magari: Kubeba wafanyakazi katika idadi ndogo ya mabasi maalum kutapunguza sana idadi ya magari binafsi barabarani. Hii itapunguza msongamano wa magari na kupelekea muda mfupi wa kusafiri kwa watumiaji wote wa barabara.
• Kuongeza Tija: Kuwa na usafiri bora na wa wakati, kutasaidia wafanyakazi kuongeza uzalishaji kazini, kwani wafanyakazi watatumia muda mdogo kuhangaikia safari za kila siku na muda mwingi kujikita katika kazi zao.
• Faida za Mazingira: Uwepo wa magari machache barabarani kutapunguza utoaji wa gesi chafuzi kwa mazingira hivyo kuendana na malengo ya maendeleo uendelevu (SDG) namba 11 na 13.
• Akiba ya Kiuchumi: Wafanyakazi watapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za kutumia usafiri binafsi kuendea kazini hivyo kuwa na akiba za kiuchumi watakazozitumia katika majukumu mengine ya kimaisha na maendeleo.
• Usalama na Faraja: Mabasi maalum yatawaongezea usalama wafanyakazi kwa kuwaepusha kuendesha vyombo vya moto wakiwa na uchovu na msongo wa mawazo.
Mikakati ya Utekelezaji
• Ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi (PPPs): Serikali kutoa vibali na usimamizi kwa sekta binfasi kumiliki mabasi na kutoa huduma hii kwa kuwafuata wafanyakazi katika vituo jirani na makazi yao na kuwapeleka makazini, kutahakikisha utoaji wa huduma kwa ufanisi na uendelevu.
• Programu za majaribio: Kuanza utekelezaji wa mradi huu katika maeneo yenye wafanyakazi wengi kama hospitali za kanda, mikoa kutasaidia kutathmini uwezekano na ufanisi wa mradi. Maoni kutoka kwa majaribio haya yatasaidia kuboresha ubora na kuongeza wigo wa utoaji huduma.
• Nauli za mabasi maalum: Ili kumudu gharama za uendeshaji, nauli inaweza kuwa mara mbili ya nauli ya daladala. Mfano kwa Mwanza, kutoka Kisesa hadi hospitali ya Bugando nauli ni tsh 1,300. Nauli ya basi maalum inaweza kuwa Tsh. 2,500 kwa safari moja na Tsh. 5,000 kwenda na kurudi. Nauli hii ni nafuu sana (1/3) kwa mfanyakazi anaetumia wastani wa Tsh. 15,000 kama gharama ya mafuta ya kwenda kazini na kurudi nyumbani kwa siku. Malipo yanaweza kufanyika kwa wiki au kwa mwezi kwa akaunti ya lipa namba au akaunti za benki ili kupunguza usumbufu wa kukusanya nauli.
• Muunganiko wa Teknolojia: Kuwa na mfumo wa kiteknolojia wa kufuatilia mahali basi lilipo (GPS) ili kupunguza muda wa kusubiria barabarani na kupokea taarifa kuhusu ratiba za usafiri na maoni ya wateja.

Mabasi maalum yatatatua kwa kiasi kikubwa changamoto za wafanyakazi za kutumia usafiri binafsi na usafiri wa umma uliopo sasa. Mafanikio ya mradi huu yatasaidia mradi huu kuongeza wigo wa kuhudumia makundi mengine.
Hongera thread nzuri.
 
👍
 
Ni kwa vile tu nchi hii huwa tunakwenda mbele mita 50 kisha tunarudi nyuma mita 100 au 150. Nakumbuka zamani idara na mashirika mengi yalikuwa na mabasi maalumu kwa ajili ya wafanyakazi. Na kuna wakati mabasi hayo pia yalihudumia wanafunzi. Nini kilitusibu!?
 
Changamoto ya gharama za uendeshaji. Hapo nimependekeza wafanyakazi walipie nauli ili mradi uweze kujiendesha
 
Kutokana na ukuaji wa miji na majiji, wafanyakazi wengi wanaishi (kujenga makazi au kupanga) maeneo ya mbali kidogo (zaidi ya kilomita kumi) kutoka maeneo wanayofanyia kazi hali inayowalazimu uhitaji wa usafiri wa kwenda kazini na kurudi nyumbani. Kwa mfano katika jiji la Mwanza, wafanyakazi wengi wanaofanya kazi maeneo ya mjini kati (city center), wanaishi maeneo ya Buhongwa, Usagara, Igoma, Kisesa, Kiseke, Buswelu nk. ambapo ni takribani kilomita ishirini kutoka mjini kati. Baadhi ya wafanyakazi wanalazimika kununua magari ili waweze kuwahi kazini na kurudi majumbani kwao huku wengi wao wakitegemea usafiri wa umma (daladala, bajaji na bodaboda) katika safari za kwenda kazini kila siku.
Changamoto za usafiri binafsi
Usafiri binafsi wa kwenda kazini una changamoto zinazoathiri ustawi wa wafanyakazi, uzalishaji wao, na ubora wa maisha kama;
• Gharama kubwa za uendeshaji wa chombo cha usafiri zinazotokana na matumizi ya mafuta na gharama za matengenezo na huduma (service) za mara kwa mara kutokana na uchakavu wa haraka.
• Kuongezeka kwa msongamano wa magari barabarani kutokana na kila mfanyakazi kwenda kazini na gari lake binafsi katika barabara chache zilizopo, hali inayoongeza hatari ya kupata ajali, na husababisha kuchelewa kazini hivyo kuathiri uzalishaji na kuongeza msongo wa mawazo kwa wafanyakazi.
• Uchovu wa dereva kutokana na kuwahi kuamka alfajiri ili kuwahi foleni, kushinda kazini siku nzima na kuchelewa kutoka kazini ili kusubiri foleni ipungue husababisha dereva kupoteza umakini barabarani, hali inayoongeza uwezekano wa kupata ajali na kuathiri utendaji kazi wa mfanyakazi.​
View attachment 2998050
• Kupoteza muda wa familia na wa kushiriki matukio ya kijamii kutokana na kuamka mapema sana ili kuwahi foleni na kuchelewa kurudi nyumbani wakisubiri foleni ipungue.
• Uhaba wa muda wa burudani na kupumzika kutokana na muda mwingi unaotumika barabarani, hivyo kuathiri afya zao ya kiakili na ubora wa maisha.
• Matumizi ya magari binafsi mengi barabarani kila siku huongeza utoaji wa moshi hatarishi kwa mazingira hivyo kuchangia uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya tabianchi.
Changamoto za Usafiri wa Umma
Usafiri wa umma uliopo sasa katika miji mikubwa na majiji nchini una changamoto kama;
• Msongamano wa watu kutokana na daladala, bajaji na bodaboda kubeba watu wengi kupita uwezo wa chombo. Hali hii huwaweka wasafiri katika hatari ya kupata madhara makubwa endapo ikitokea ajali, huwaongezea wasafiri uwezekano wa kuambukizana magonjwa kama vile mafua na kupelekea wasafiri kuwa na msongo wa mawazo.
• Usalama mdogo wa mali za wasafiri kutokana na msongamano mkubwa katika vituo vya usafiri na kwenye vyombo vya usafiri. Wasafiri wengi hujikuta wakiibiwa na kupoteza mali zao kama simu, pochi na mizigo yao.​
View attachment 2998051
• Ratiba zisizo thabiti za huduma za usafiri wa umma kuwa usafiri unaanza saa ngapi na unaisha saa ngapi, hali inayosababisha wasafiri kukosa huduma ya usafiri hasa nyakati za usiku au kuchelewa sana kurudi nyumbani.
• Upotevu wa muda wa kusubiria usafiri na wakati wa safari huwasabibishia wasafiri msongo wa mawazo na kupelekea ugomvi mara kwa mara baina ya wasafiri, wasafiri na watoa huduma, na wasafiri na wanafamilia zao. Muda unaopotea pia huwachelewesha wasafiri katika shughuli za uzalishaji mali.
• Magari ya usafiri wa umma mara nyingi ni ya zamani na yamechakaa, na hivyo kuhatarisha usalama wa abiria. Magari mengi hayana vifaa vya kustarehesha kama vile kiyoyozi na TV, hivyo kufanya safari kuwa za kero.
• Uvunjaji wa sheria za usalama barabarani na za usafirishaji kama vile kuendesha kasi, kupakia abiria kupita kiasi, kupakia abiria na mizigo, kuendesha magari bila leseni, kuweka sauti kubwa sana ya mziki na kukatisha njia (route). Haya huongeza uwezekano wa ajali na kusababishia usumbufu kwa wasafiri.

Utatuzi wa changamoto za usafiri kwa wafanyakazi
Kuwa na mabasi maalum kutaboresha usafiri kwa wafanyakazi kwa kutoa huduma zenye ufanisi, usalama na za kuaminika kama ifuatavyo;
• Kupunguza Msongamano wa magari: Kubeba wafanyakazi katika idadi ndogo ya mabasi maalum kutapunguza sana idadi ya magari binafsi barabarani. Hii itapunguza msongamano wa magari na kupelekea muda mfupi wa kusafiri kwa watumiaji wote wa barabara.
• Kuongeza Tija: Kuwa na usafiri bora na wa wakati, kutasaidia wafanyakazi kuongeza uzalishaji kazini, kwani wafanyakazi watatumia muda mdogo kuhangaikia safari za kila siku na muda mwingi kujikita katika kazi zao.
• Faida za Mazingira: Uwepo wa magari machache barabarani kutapunguza utoaji wa gesi chafuzi kwa mazingira hivyo kuendana na malengo ya maendeleo uendelevu (SDG) namba 11 na 13.
• Akiba ya Kiuchumi: Wafanyakazi watapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za kutumia usafiri binafsi kuendea kazini hivyo kuwa na akiba za kiuchumi watakazozitumia katika majukumu mengine ya kimaisha na maendeleo.
• Usalama na Faraja: Mabasi maalum yatawaongezea usalama wafanyakazi kwa kuwaepusha kuendesha vyombo vya moto wakiwa na uchovu na msongo wa mawazo.
Mikakati ya Utekelezaji
• Ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi (PPPs): Serikali kutoa vibali na usimamizi kwa sekta binfasi kumiliki mabasi na kutoa huduma hii kwa kuwafuata wafanyakazi katika vituo jirani na makazi yao na kuwapeleka makazini, kutahakikisha utoaji wa huduma kwa ufanisi na uendelevu.
• Programu za majaribio: Kuanza utekelezaji wa mradi huu katika maeneo yenye wafanyakazi wengi kama hospitali za kanda, mikoa kutasaidia kutathmini uwezekano na ufanisi wa mradi. Maoni kutoka kwa majaribio haya yatasaidia kuboresha ubora na kuongeza wigo wa utoaji huduma.
• Nauli za mabasi maalum: Ili kumudu gharama za uendeshaji, nauli inaweza kuwa mara mbili ya nauli ya daladala. Mfano kwa Mwanza, kutoka Kisesa hadi hospitali ya Bugando nauli ni tsh 1,300. Nauli ya basi maalum inaweza kuwa Tsh. 2,500 kwa safari moja na Tsh. 5,000 kwenda na kurudi. Nauli hii ni nafuu sana (1/3) kwa mfanyakazi anaetumia wastani wa Tsh. 15,000 kama gharama ya mafuta ya kwenda kazini na kurudi nyumbani kwa siku. Malipo yanaweza kufanyika kwa wiki au kwa mwezi kwa akaunti ya lipa namba au akaunti za benki ili kupunguza usumbufu wa kukusanya nauli.
• Muunganiko wa Teknolojia: Kuwa na mfumo wa kiteknolojia wa kufuatilia mahali basi lilipo (GPS) ili kupunguza muda wa kusubiria barabarani na kupokea taarifa kuhusu ratiba za usafiri na maoni ya wateja.

Mabasi maalum yatatatua kwa kiasi kikubwa changamoto za wafanyakazi za kutumia usafiri binafsi na usafiri wa umma uliopo sasa. Mafanikio ya mradi huu yatasaidia mradi huu kuongeza wigo wa kuhudumia makundi mengine.
Wazo zuri na sahihi sana katika kutatua changamoto za usafiri Kwa watumishi
 
Andiko zuri saana.

Wazo zuri, Lakini changamoto itakayotokea huenda gharama zikaielemea serikali kutokana na magari hayo kubeba watu wachache. Na hii ni kutokana na ratiba binafsi za wafanyakazi, kuna wanaowahi zaidi, kuna wanapitia maeneo mengine kabla ya kufika nyumbani/kazini kwaajili ya mambo mengine, nikimaanisha safari zao sio za moja kwa moja mpaka nyumbani/kazini. Kitu ambacho kitawafanya washindwe kutumia usafiri huo.

Kwa hili ni mikakati gani itawekwa ili kuepusha serikali kuambulia hasara kutokana na mabasi hayo kukosa wateja.
 
Jukumu la serikali katika mradi huu ni kutoa vibali vya njia kwa wafanyabiashara (sekta binafsi) ili waweze kuutekeleza, kwahiyo hakuna hasara kwa serikali. Mfanyakazi ni mtu yoyote anayetoka nyumbani kwenda kazini kwake sio muajiriwa tuu wa serikali. Generally, huwa kuna watu walio tayari kugharamia huduma bora na yenye uhakika ndio maana hotel za bei kubwa, usafiri wa VIP vinapata wateja, kwahiyo ubora wa huduma katika mradi huu utavutia wateja hivyo uendelevu wa mradi
 
Kutokana na ukuaji wa miji na majiji, wafanyakazi wengi wanaishi (kujenga makazi au kupanga) maeneo ya mbali kidogo (zaidi ya kilomita kumi) kutoka maeneo wanayofanyia kazi hali inayowalazimu uhitaji wa usafiri wa kwenda kazini na kurudi nyumbani. Kwa mfano katika jiji la Mwanza, wafanyakazi wengi wanaofanya kazi maeneo ya mjini kati (city center), wanaishi maeneo ya Buhongwa, Usagara, Igoma, Kisesa, Kiseke, Buswelu nk. ambapo ni takribani kilomita ishirini kutoka mjini kati. Baadhi ya wafanyakazi wanalazimika kununua magari ili waweze kuwahi kazini na kurudi majumbani kwao huku wengi wao wakitegemea usafiri wa umma (daladala, bajaji na bodaboda) katika safari za kwenda kazini kila siku.
Changamoto za usafiri binafsi
Usafiri binafsi wa kwenda kazini una changamoto zinazoathiri ustawi wa wafanyakazi, uzalishaji wao, na ubora wa maisha kama;
• Gharama kubwa za uendeshaji wa chombo cha usafiri zinazotokana na matumizi ya mafuta na gharama za matengenezo na huduma (service) za mara kwa mara kutokana na uchakavu wa haraka.
• Kuongezeka kwa msongamano wa magari barabarani kutokana na kila mfanyakazi kwenda kazini na gari lake binafsi katika barabara chache zilizopo, hali inayoongeza hatari ya kupata ajali, na husababisha kuchelewa kazini hivyo kuathiri uzalishaji na kuongeza msongo wa mawazo kwa wafanyakazi.
• Uchovu wa dereva kutokana na kuwahi kuamka alfajiri ili kuwahi foleni, kushinda kazini siku nzima na kuchelewa kutoka kazini ili kusubiri foleni ipungue husababisha dereva kupoteza umakini barabarani, hali inayoongeza uwezekano wa kupata ajali na kuathiri utendaji kazi wa mfanyakazi.​
View attachment 2998050
• Kupoteza muda wa familia na wa kushiriki matukio ya kijamii kutokana na kuamka mapema sana ili kuwahi foleni na kuchelewa kurudi nyumbani wakisubiri foleni ipungue.
• Uhaba wa muda wa burudani na kupumzika kutokana na muda mwingi unaotumika barabarani, hivyo kuathiri afya zao ya kiakili na ubora wa maisha.
• Matumizi ya magari binafsi mengi barabarani kila siku huongeza utoaji wa moshi hatarishi kwa mazingira hivyo kuchangia uchafuzi wa hewa na mabadiliko ya tabianchi.
Changamoto za Usafiri wa Umma
Usafiri wa umma uliopo sasa katika miji mikubwa na majiji nchini una changamoto kama;
• Msongamano wa watu kutokana na daladala, bajaji na bodaboda kubeba watu wengi kupita uwezo wa chombo. Hali hii huwaweka wasafiri katika hatari ya kupata madhara makubwa endapo ikitokea ajali, huwaongezea wasafiri uwezekano wa kuambukizana magonjwa kama vile mafua na kupelekea wasafiri kuwa na msongo wa mawazo.
• Usalama mdogo wa mali za wasafiri kutokana na msongamano mkubwa katika vituo vya usafiri na kwenye vyombo vya usafiri. Wasafiri wengi hujikuta wakiibiwa na kupoteza mali zao kama simu, pochi na mizigo yao.​
View attachment 2998051
• Ratiba zisizo thabiti za huduma za usafiri wa umma kuwa usafiri unaanza saa ngapi na unaisha saa ngapi, hali inayosababisha wasafiri kukosa huduma ya usafiri hasa nyakati za usiku au kuchelewa sana kurudi nyumbani.
• Upotevu wa muda wa kusubiria usafiri na wakati wa safari huwasabibishia wasafiri msongo wa mawazo na kupelekea ugomvi mara kwa mara baina ya wasafiri, wasafiri na watoa huduma, na wasafiri na wanafamilia zao. Muda unaopotea pia huwachelewesha wasafiri katika shughuli za uzalishaji mali.
• Magari ya usafiri wa umma mara nyingi ni ya zamani na yamechakaa, na hivyo kuhatarisha usalama wa abiria. Magari mengi hayana vifaa vya kustarehesha kama vile kiyoyozi na TV, hivyo kufanya safari kuwa za kero.
• Uvunjaji wa sheria za usalama barabarani na za usafirishaji kama vile kuendesha kasi, kupakia abiria kupita kiasi, kupakia abiria na mizigo, kuendesha magari bila leseni, kuweka sauti kubwa sana ya mziki na kukatisha njia (route). Haya huongeza uwezekano wa ajali na kusababishia usumbufu kwa wasafiri.

Utatuzi wa changamoto za usafiri kwa wafanyakazi
Kuwa na mabasi maalum kutaboresha usafiri kwa wafanyakazi kwa kutoa huduma zenye ufanisi, usalama na za kuaminika kama ifuatavyo;
• Kupunguza Msongamano wa magari: Kubeba wafanyakazi katika idadi ndogo ya mabasi maalum kutapunguza sana idadi ya magari binafsi barabarani. Hii itapunguza msongamano wa magari na kupelekea muda mfupi wa kusafiri kwa watumiaji wote wa barabara.
• Kuongeza Tija: Kuwa na usafiri bora na wa wakati, kutasaidia wafanyakazi kuongeza uzalishaji kazini, kwani wafanyakazi watatumia muda mdogo kuhangaikia safari za kila siku na muda mwingi kujikita katika kazi zao.
• Faida za Mazingira: Uwepo wa magari machache barabarani kutapunguza utoaji wa gesi chafuzi kwa mazingira hivyo kuendana na malengo ya maendeleo uendelevu (SDG) namba 11 na 13.
• Akiba ya Kiuchumi: Wafanyakazi watapunguza kwa kiasi kikubwa gharama za kutumia usafiri binafsi kuendea kazini hivyo kuwa na akiba za kiuchumi watakazozitumia katika majukumu mengine ya kimaisha na maendeleo.
• Usalama na Faraja: Mabasi maalum yatawaongezea usalama wafanyakazi kwa kuwaepusha kuendesha vyombo vya moto wakiwa na uchovu na msongo wa mawazo.
Mikakati ya Utekelezaji
• Ushirikiano wa Serikali na sekta binafsi (PPPs): Serikali kutoa vibali na usimamizi kwa sekta binfasi kumiliki mabasi na kutoa huduma hii kwa kuwafuata wafanyakazi katika vituo jirani na makazi yao na kuwapeleka makazini, kutahakikisha utoaji wa huduma kwa ufanisi na uendelevu.
• Programu za majaribio: Kuanza utekelezaji wa mradi huu katika maeneo yenye wafanyakazi wengi kama hospitali za kanda, mikoa kutasaidia kutathmini uwezekano na ufanisi wa mradi. Maoni kutoka kwa majaribio haya yatasaidia kuboresha ubora na kuongeza wigo wa utoaji huduma.
• Nauli za mabasi maalum: Ili kumudu gharama za uendeshaji, nauli inaweza kuwa mara mbili ya nauli ya daladala. Mfano kwa Mwanza, kutoka Kisesa hadi hospitali ya Bugando nauli ni tsh 1,300. Nauli ya basi maalum inaweza kuwa Tsh. 2,500 kwa safari moja na Tsh. 5,000 kwenda na kurudi. Nauli hii ni nafuu sana (1/3) kwa mfanyakazi anaetumia wastani wa Tsh. 15,000 kama gharama ya mafuta ya kwenda kazini na kurudi nyumbani kwa siku. Malipo yanaweza kufanyika kwa wiki au kwa mwezi kwa akaunti ya lipa namba au akaunti za benki ili kupunguza usumbufu wa kukusanya nauli.
• Muunganiko wa Teknolojia: Kuwa na mfumo wa kiteknolojia wa kufuatilia mahali basi lilipo (GPS) ili kupunguza muda wa kusubiria barabarani na kupokea taarifa kuhusu ratiba za usafiri na maoni ya wateja.

Mabasi maalum yatatatua kwa kiasi kikubwa changamoto za wafanyakazi za kutumia usafiri binafsi na usafiri wa umma uliopo sasa. Mafanikio ya mradi huu yatasaidia mradi huu kuongeza wigo wa kuhudumia makundi mengine.
Akili kubwa Sana imetumika hapa mtu kazi, congratulations Kwa wazo bunifu
 
Back
Top Bottom