Mabasi mapya 150 ya MOFAT yakwama kupata njia | kafulila aingilia kati

Mabasi mapya 150 ya MOFAT yakwama kupata njia | kafulila aingilia kati

YAY

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2024
Posts
879
Reaction score
873
IMG-20260507-WA0186.jpg

Dar es salaam, Zaidi ya mabasi ya Mofat 150 yamekwama kwa zaidi ya nusu mwaka bila kuanza kazi katika barabara ya Mbagala, jijini Dar es Salaam. Hali hii imeibua mjadala mpana kuhusu ufanisi wa mradi wa mwendokasi na athari zake kwa wananchi pamoja na mwekezaji.

Hata hivyo, Kampuni ya Mofat imefanya uwekezaji mkubwa kwa kuleta mabasi 200 mapya, kila moja likiwa na uwezo wa kubeba abiria 165. Mabasi haya yamekamilika nyaraka zote muhimu, yamepata bima na yamehakikiwa na mamlaka husika.

Pamoja na hayo ni mabasi 50 pekee ndiyo yanayotoa huduma kwa sasa, jambo linaloibua maswali kuhusu ufanisi wa mradi na Mapokeo ya PPP kwa mamlaka za Serikali.

Kukosa nafasi za kuanza kazi licha ya maandalizi kukamilika ni kiashiria cha hasara kwa mwekezaji kutokana na mabasi yaliyokwama bila kutumika yangeweza kubeba abiria 250,000 kwa siku na ikiwa amekopa basi huenda Uhusiano wa kifedha wa mteja na benki unaweza kuathirika iwapo mabasi hayataanza kazi mapema huku mwekezaji akihitajika kurejesha mkopo.

Hata hivyo Mkurugenzi wa PPPC na Mwenyekiti wa DART, Bwana David Kafulila, amesema kuwa serikali imeanza mchakato wa suluhu kupitia ripoti ya tathmini ya nusu mwaka. Kafulila amesisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha uwekezaji huu mkubwa unaleta tija na manufaa kwa wananchi wa kipato cha chini na kuondoa changamoto kabisa za usafiri zilizopo katika Jiji la Dar es salaam.

Wakati haya yakiendelea Wananchi wamependekeza mabasi haya yaelekezwe barabara ya Gongo la Mboto, ambayo imekamilika kwa 99%. Hatua hii inaweza kupunguza msongamano wa abiria na kuongeza ufanisi wa huduma ya mwendokasi katika Jiji la Dar es salaam.

===
 
Watu wenyewe kila siku domo blah blah matokeo sifuri
Huu mradi una legalega tu
Ujenzi wenyewe haujakamilika 100%

Ova
Hata kama hapajakamilika tuanze hivyo hivyo
 
Back
Top Bottom