Mabasi mapya 70 ya Mwendokasi yamehifadhiwa eneo la hatari sana

Mabasi mapya 70 ya Mwendokasi yamehifadhiwa eneo la hatari sana

LICHADI

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2015
Posts
4,491
Reaction score
12,560
Serikali inaleta gari 70 baada ya kuziingiza kwenye mzunguko watu wapate nafuu ya mateso wanayoyapata kwa sasa matokeo yake gari wameenda kuzimwaga pale Jangwani, hata kama ni swala la usajili na vibali serikali ikiamua lake haiwezi zidi wiki moja lakini mwezi unaenda kukata wameyabwaga pale.

Kumbukeni lile eneo kupaki magari mapya pale ni kutafuta hasara, ikipiga mvua kubwa panajaa maji, na ndio maana waziri mkuu alikuta magari pale yamekufa sababu ya kujaa maji na matope hadi ndani, eneo ambalo yamewekwa yake magari mapya ikipiga mvua ya kushtukiza pale mtakuta yanaelea.

Huwezi uka-risk kuweka gari mpya 70 eneo lile kama sio kutafuta hasara nyingine, ikipiga mvua kubwa ya kushtukiza pale itakuwa ni hasara nyingine, ni suala la muda tu.
 
Yaani hawa maCEO sijui huwa wana pumba gani kichwani

Yaani wakuu wa idara za serikali ndio waamuzi utadhani anaamulia ya familia yake

Prof Assad alisema hatuna taasisi strong tuna watu strong,
 
Yaani hawa maCEO sijui huwa wana pumba gani kichwani

Yaani wakuu wa idara za serikali ndio waamuzi utadhani anaamulia ya familia yake

Prof Assad alisema hatuna taasisi strong tuna watu strong
Yaani wamuite mtu kama baaresa wampe hii tenda serikali kufanya biashara ni kutafuta hasara tu.
 
Akina nani wanapata shida?

Kwani si yanasubiri route zile za Mbagala wacha iishe kwanza ile project then watayaruhusu kufanya kazi kutoka Gerezani kwenda Mbagala.

Nyie wa Mbezi/ Kimara/ Morocco mtaendelea kutumia yale yanayofanya kazi kwa sasa.
 
Akina nani wanapata shida
Kwani si yanasubiri route zile za Mbagala wacha iishe kwanza ile project then watayaruhusu kufanya mazi kutoka Gerezani kwenda Mbagala.
Kulikua na haja gani kuyaleta sasa hivi?

Huoni yataanza chakaa kabla ya wakati
 
Akina nani wanapata shida
Kwani si yanasubiri route zile za Mbagala wacha iishe kwanza ile project then watayaruhusu kufanya mazi kutoka Gerezani kwenda Mbagala...
Wewe itakuwa ni mwenyeji wa tabora huko dar unapaskia tu, route ya kimara gari ni chache watu wanapata shida , gari zinahitajika pale alafu unasema zinasubiria route ya mbagala unaakili kweli wewe
 
Back
Top Bottom