Mabasi mapya ya Mwendokasi ya MOFAT yaanza kubeba Abiria Gerezani–Mbezi

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Mabasi Mapya yaendayo haraka ya Kampuni ya Mofat yameonekana asubuhi ya leo (2/10/2025) yakibeba abiria katika vituo vya mwendokasi yakitokea Gerezani kwenda Kimara-Mbezi.

Hii inakuja siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila kufika kituo cha mwendokasi Kimara na kushuhudia kadhia wanayopitia wananchi katika usafiri huo.

Jana usiku majira ya saa mbili pia mabasi ya mwendokasi na vituo ikiwemo cha Gerezani, Magomeni Mapipa, Magomeni Usalama na Magomeni Kagera kushambuliwa kwa mawe.

Magari ya Mofat yaliletwa nchini kwa ajiri ya 'route' ya Mbagala lakini leo yameonekana barabara ya Gerezani- Mbezi.

1759384961758.png

1759385004866.png

1759385038287.png
 
Hii nchi kumbe raia wakiamua ibadilike inawezekana, baada ya kuona mabasi mabovu yakipigwa mawe Serikali imesikia na kuchukua hatua chapchap ya kuleta mabasi mapaya chini ya saa 12.

Sasa yale mabasi mabovu yaliyobakia wayaondoe yote kwenye route.
 
Mabasi Mapya yaendayo haraka ya Kampuni ya Mofat yameonekana asubuhi ya leo (2/10/2025) yakibeba abiria katika vituo vya mwendokasi yakitokea Gerezani kwenda Kimara-Mbezi.

Hii inakuja siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila kufika kituo cha mwendokasi Kimara na kushuhudia kadhia wanayopitia wananchi katika usafiri huo.

Jana usiku majira ya saa mbili pia mabasi ya mwendokasi na vituo ikiwemo cha Gerezani, Magomeni Mapipa, Magomeni Usalama na Magomeni Kagera kushambuliwa kwa mawe.

Magari ya Mofat yaliletwa nchini kwa ajiri ya 'route' ya Mbagala lakini leo yameonekana barabara ya Gerezani- Mbezi.

View attachment 3482190
Sasa haya ni kupiga moto
 
Back
Top Bottom