Pale Moshi Dar Express wana stendi yao wenyewe hawashirikiani na mabasi mengine isipokuwa ya kwao. Pia wana mgahawa pale. Sasa nashangaa kwa nini wawatoze watu kutumia choo kwani migahawa ya mjini yote si inastahili kuwa na choo cha wateja?
Hivi naweza kukupeleka nyumbani kwangu, kwa gari langu mwenyewe amabalo nimekutoza nauli halafu nikuchaji kutumia choo. Tena baada ya wewe kununua chakula nilichopika mwenyewe? Kuna wengine humu nadhani hawaelewi
wakuu, mahali ambapo ipo stand ya Dar express moshi siyo stand kuu ya mabasi, sehemu hii yenye offisi za dar express iko adjacent na restaurant ambayo kimsingi hiyo restaurant ndiyo yenye choo ndani yake, restaurant hii siyo ya dar express hivyo basi nadhani kama wameanzisha huduma ya kulipia choo basi ni uamuzi wa hiyo restaurant na siyo dar express
basi wawe wanawapeleka abiria stendi. DAR EXPRESS mpk mzigo wako mwenyewe wanakulazimisha uulipie wakati nauli umewapa ........ mmiliki na wahudumu wake wote ni wase***
Jitahidini sana lakini hamutaweza kuwaharibia Dar Express. Anaewatuma mwambieni aingize magari yake na a-operate kwa ushindani. If he can that is.
Kwan lazma upande
hiyo gari?
Unadhani bila mchango wako wangekuwa hapo
walipo! Kapande ngorika osaka bufalo
ndo utatia akili! Kama vipi maliza haja zako home !au km waona jiti mbili zako dili baaas
ingia kichakani! Hakuna huduma ya bure
kwa nji hii kwa sasa
msimsakame dar exp
Kuna uhusiano gani kati ya choo na nauli ya basi? Nadhani mtoaji mada angefafanua hili.
Basi lina gharama zake za uendeshaji na ndio maana unalipa nauli. Na hivyo hivyo kwenye chakula na choo pia - kuna gharama za usafi na uendeshaji maliwato ki-ujumla na ndo maana unalipia.
Leo ukilipa 30,000/- ukapewa huduma ya choo bure, kesho utasema kwanini nalipa 30,000/- alafu chakula nanunua - utataka na chakula upewe bure kwa sababu tu mgahawa unamilikiwa na Dar express.
Ile ni biashara ya choo bwana, embu tuwe waelewa. Hata kama wewe si abiria unaweza pia ukatumia huduma hiyo pale unapohitaji. Na kama haukoradhi kulipia hiyo 200, unaweza tafuta jinsi nyingine ya kutimiza haja zako. Hakuna mtu anayekuchagulia.