Kuna uhusiano gani kati ya choo na nauli ya basi? Nadhani mtoaji mada angefafanua hili.
Basi lina gharama zake za uendeshaji na ndio maana unalipa nauli. Na hivyo hivyo kwenye chakula na choo pia - kuna gharama za usafi na uendeshaji maliwato ki-ujumla na ndo maana unalipia.
Leo ukilipa 30,000/- ukapewa huduma ya choo bure, kesho utasema kwanini nalipa 30,000/- alafu chakula nanunua - utataka na chakula upewe bure kwa sababu tu mgahawa unamilikiwa na Dar express.
Ile ni biashara ya choo bwana, embu tuwe waelewa. Hata kama wewe si abiria unaweza pia ukatumia huduma hiyo pale unapohitaji. Na kama haukoradhi kulipia hiyo 200, unaweza tafuta jinsi nyingine ya kutimiza haja zako. Hakuna mtu anayekuchagulia.