Mabasi ya Hood yameishia wapi?

Mabasi ya Hood yameishia wapi?

Tawaqal
Zainabu
Masiah
M Sleeping Coach
Matema Beach
Scandinavia Express
Kiswele
Executive
Hood ltd
Safina
Embakassy
Lupelo
Sayuni

Wajana kiba Ngorika, Ndenjela, Mohammed Trans, Ilasi etc
Mengi Huwa ni Kodi zetu wakubwa wakistaafu na mabus nayo ustaafu kwa sababu mirija ya Kodi zetu ukata.
Lipo wapi buffalo, subiria wa ESTA akiwa nje ya system kama utayaona road.
 
Biashara ya mabus ni jini mla pesa niliifanya simshauri mtu watumishi wengi ndipo wanapopatia umasikini kwenye biashara hii.
Daladala nyingi ni za matrafic wakistaafu nazo ustaafu juu ya mawe.
Kange trans za Lugola sijui Kama zipo bado
 
Kweli ushindani ni mkubwa
Yaani leo niko jogging nakuta BM mbili zimeshatoka lakini Kilimanjaro limepigwa doro abiria wachache
Nani anapanda sufuria wakati Cha upepo kipo.
Full AC,good interior design, fully suspension spring, lather sofa seat, charging system, luxuries and comfortability
 
Biashara ya mabus ni jini mla pesa niliifanya simshauri mtu watumishi wengi ndipo wanapopatia umasikini kwenye biashara hii.
Daladala nyingi ni za matrafic wakistaafu nazo ustaafu juu ya mawe.
Kange trans za Lugola sijui Kama zipo bado
Hii biashara kwa mtu mwenye umri zaidi ya miaka 50 sidhani kama ni nzuri kwa afya 😄
 
Kukuta tajiri wa mabus ana maendeleo ni ngumu sana wengi ni wakurupukaji.
1.Channel ya kupiga Kodi zetu easy money kurupu kwenye mabus ofisi ikikata uzioni basi barabarani.
2.matajiri wa madini kurupu bi kadhaa hizi hapa kichwa kichwa biashara ya kwanza mabus manne mapya madini yakikata chali.
3.Washirikina Hela za manyoka wanapenda mabus kwa sababu ni rahisi kupata kafara.
 
Hii biashara kwa mtu mwenye umri zaidi ya miaka 50 sidhani kama ni nzuri kwa afya 😄
Si nzuri kwa afya ya akili inatakiwa under 40.
Pana Mzee alistaafu akanunua daladala mwanzoni safi baada ya mazoea analetewa kiswahili akawa anashinda stand ya daladala kuhesabu tripu ngapi imepiga kwa siku.
 
Biashara ya usafiri naona inalipa iwapo unapata tender ya kusafirisha bidhaa etc ila hii ya kusubiri abiria ukichanganya na akili za madereva aiseee ni balaa ila kuna watu wanaziweza na zimewatoa
 
Baadhi ya yale mabasi yalikuwaga na shape ya mkate nakumbuka
... TTBS - Tanganyika Transport Bus Service; mlango wa abiria uko katikati ya bus na carriers ziko juu ngazi za kupandia huko ziko karibu na siti ya mlangoni.

Leyland na Bedford hizo! Scania by then bado sana; Marco Polo ndio ndoto za alinacha; Yutong hajatungwa mimba. Sina hakika kama kata-K wanaelewa.

Kipindi kile mwanamke kuvaa suruali ilikuwa ni aibu ya mwaka leo wako na skin tight maofisini na masokoni!
 
Back
Top Bottom