Dunia ya leo hata kama hukanyagi Marekani lakini kama umejiunga kwenye jumuiya za kimataifa bhasi VETO power yao huwezi kuiepuka.
Ushawishi wa Marekani ni mkubwa na sisi kama sisi sidhani kama tunaweza survive kama wakiamua kweli kutukazia
Viwanda vyetu vyenyewe ndio hivi ambavyo hata kutengeneza sindano ni shida, Export zetu zenyewe nadhani unazielewa na chanzo kikubwa cha foreign reserve unakijua. Kukaziwa sisi ni rahisi sanaaaa ila tuombe tu mambo yasiharibike
Usihofu ndugu yangu, sababu zenyewe walizozitoa hao wapinzani na hao watu wa Amnesty International na ma NGOs ni sababu za kipuuzi sana ambazo haziwezi kuifanya serikali ya Marekani, UN au EU kuiwekea Tanzania vikwazo vya kiuchumi.
Kwenye report hii wamezungumzia mambo mengi sana kuhusu malalamiko ya wapinzani na hasa CHADEMA na ACT Wazalendo na kidogo CUF, lakini pia NGOs na watu wa haki za binadam ikiwemi majournalists uchwara.
Ukweli ambao usioweza kupingika ni kwamna hayo yaliyo andikwa humu ni kama maneno ya kijiweni yasiyo kuwa na uzito mkubwa wa kuyaamini. Ninporojo tu za kipashkuna pashkuna.
References zao nyingi ni za kutoka kwenye magazeti uchwara kama ya chama cha TWAWEZA ambacho duniani hakijurikani.
Kwa kifupi serikali ya Marekani haioni sababu yoyote ya kimsingi ya kuiwekea Tanzania vikwazo vya uchumi. Watanzania kwa ujumla wanaishi vizuri na hakuna mtu ananyanyasika au kunyanyaswa na serikali yake.
Magufuli anafanya kazi nzuri ya kuwaletea wananchi wake maendeleo. Sisi hatukuwanyang'anya mashamba watu wao kama Zimbabwe ilivyo fanya na wala serikali yetu haiwasulubu watu wake kwa hiyo ni porojo tu za vilabuni ambavyo havina mantik.
Off course NGOs na taasisi za kimataifa kama Amnesty International ambavyo vilitarajia kusikia su kuona vurugu zetu zijitokea, hazita jisikia vizuri kwa sababu hawawezi ku operate Tanzania kwa faida. Kama kujilisha tuna jilisha sisi wenyewe na hatutegemei sana misaada ya nje kwa vyakula.
Mahusiano ya kibiashara na nchi za nje yanaendelea kama kawaida na mikopo kutoka World Bank na IMF tutaendelea kupata vile vile tukiihitaji.
Kwa report hii mimi naona wapinzani ambao ni radicals, wanaharakati kama akina Maria Sarungi, Fatma Karume na wengineo ambao walitegemea sisi tuwekewe vikwazo vya uchumi wameshindwa vibaya sana na hawana hamu tena ya maisha. Ningewaomba watafute sttategy nyingine lakini sio ya haki za binadam.
Wao wanafikiri ulimwengu hauoni mambo yanayotendeka Tanzania. Ulimwengu unajua kila kitu kinachofanywa na serika ya magufuli. Kama magufuli angekuwa anafanya vitu vibaya wananchi wake vyombo vyao vya habari kama CNN International, BBC International na Al Jazeera wangekuwa wanareport kila siku mambo yanayo tokea huku. Lakini mambo ya kikekike na ya kishogashoga ya akina Zuhura Yunus, Salim Kikeke na Mary Mgawe wa VOA kwa kiswahili mnafikiri nani anayasikiriza, ni sisi tu na majiranibzetu wakenya wakongo na uganda kidogo.
Watu wakubwa wanao tuchafulia nje ni hawa Amnesty International walioko Kenya wakishirikiana na wapinzani wetu hasa CHADEMA, ACT na CUF.
na NGOs wachwara wa Europe hasa wa ujerumani.