Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Niseme tu very smart comment so far...umeandika nimekuelewa na umeeleweka. Shida ni baadhi ya viongozi kukosa uzalendo. China yupo kutafutia watoto wake na sisi tunatakiwa kuwa na fikra za aina hiyo..kwanini viongozi wetu wanakuwa rahisi sana kuuza watu wao hata kwa miaka 100? Mkataba ukiwa na maslahi kwa taifa sioni sababu ya kuupinga. Ila sio mradi unaouwa bandari zetu na kubeba mapato yote for decades, ujinga gani huo? Kisa umepewa billion 100 ndio uwauze watu wako for the next 50 or 100 years?
 
Umeweka andiko kiujumla jumla mno kiasi kwamba sipati pa kushikia.

Katika watu wote, achia kati ya marais pekee, sikuwahi hata siku moja kumwamini Magufuli kwa lolote asemalo mpaka nione ukweli ulipo. Kwa hiyo nikiandika hapa, siandiki kutokana na aliyosema Magufuli.

Kuhusu ujenzi wa bandari kama hii ya Bagamoyo, kuna vigezo vingi sana vizuri vinavyoipa sifa ya kuwa na sifa ya kufanya "biashara itakayolipa."

'
"connections na influences" zipi unazohitaji ili wafanya biashara wa eneo la ukanda wote huu waone kuwa biashara zao zitakuwa na faida kubwa kwao kwa kutumia bandari iliyo karibu zaidi, na hasa kama itaendeshwa kwa ufanisi!
 
Hakuna mtu anaebisha au kupinga mradi utakao leta manufaa kwa taifa. Kuwa reli inayohitaji mzigo ndio i justify mkataba wa bagamoyo kwa namna yoyote ile ? Kwa vyovyote vile mkataba ulivyo? Akili gani hizi? Kama mkataba upo vizuri unalinda maslahi ya nchi esp kwenye mapato nani huyo mwenye akili za kijinga anapinga huo mradi? Tunataka win win...china anatafutia watu wake na sisi tuna wajibu wa kutafutia watu wetu...thus win win.
 
Mimi niliona 12.6 USD. Kisasi hiki kitalipwa kwa wamiliki wa bomba hilo ambao ni Total, wachina,Uganda na Tanzania. Umiliki wa Tanzania kwenye bomba hilo ni 5%

Hiyo 12.6 USD ni gross. Unatoa gharama za uendeshaji wa bomba hilo,kinachobaki ndio wanahisa wa bomba hilo wanagawana.
 
Mkuu, siyo kuwa nausuport mradi hundred percent. We need more information. Point yangu ni kwamba kama benefits Zina overturn losses, why not taking it kwa kuwa at the end of the day it is ours unlike Machimbo ya madini yanayoondoa mali na kutuachia mashimo. Aridhi ambayo haina faida yeyote mchimbaji akiondoka

Kwenye point yangu kuhusu connection is simple. Ni kwamba mzigo hauongezeki tu kwa kuwa bandari imekuwa kubwa na efficient. Kuna a lot of other factors.
 
Tatizo marais wetu wanawaza kufanya vitu within 10 years ya utawala wao, angalau Mkapa alifanya vitu ambavyo vilikuwa havimpi ujiko wa haraka lakini kwa leo hii watu wenye kutambua, wanajua kuwa yule mzee alikuwa anasimika mifumo ya kusaidia nchi hata kwa miaka 50 mbele.

Sasa watawala wa leo wangeichukua kuwa hii bandari kuwa ni ajenda ya Kitaifa ya kuifanya kwa miaka 30 na ikatungwa sheria ya kulazimisha serikali itenge bajeti ya kiasi fulani kila mwaka kutekeleza mradi huu, nakuhakikishia hii kitu tunaweza kuifanya!
 
Ninakubaliana nawe kuhusu ushindani.

Ila sikubali kuhusu ubunifu, sio 'preserve' ya watu walioko skta binafsi pekee.

Serikali ikitaka watu wake wawe wabunifu na wafanye kazi ya kufanikisha mashirika, inaweza sana.

Viongozi serikalini ndio tatizo.
Na haohao viongozi serikalini baadhi ndio wanaopotosha na kupotoshwa...
 
Tanzania haiwezi kuwa kisiwa... mradi huohuo "mbaya" jirani zetu waliuhitaji uwe kwao .. ushawishi gani ulitumika ili uje kwetu tubaki kimya! Yaweza kuonekana ni hasara lakini faida za usafirishaji na uchangamkaji wa biashara ambao ungetokana na bandari hiyo.. kuna mengi hayatazamwi bali ubaya pekee...!!!
 
Kwanza, naomba msamaha kama nilisema literature review in proposal. Hapo nimechapia, nilichotaka kusema ni kuwa literature review ni sehemu ya prposal na ni sehemu muhimu ya proposal. Proposal inaandikwa na mtaalamu mwenyewe, kwa sababu yeye ndiyo anayeijuwa concet nzima ya utafiti anaotaka kufanya. Cha ajabu wewe ulikuwa recruited kama research assistant, lakini eti ukawa na jukumu la kuwa na sehemu kubwa katika hiyo proposal ya kuandika lietrature review. Mimi nilichokuuliza ni, je IRB ilikaa na kubariki huo utafiti ambao haukuwa na literature review. Ni mtafiti wa dunia gani atabeba mikoba yake kuja kufanya utafiti ambao proposal haijakamilika na kibali hajapewa cha kuja kufanya utafiti. Ndiyo maana nilikuambia siyo kweli wewe ndiyo mwandishi wa literature review. Kama wewe ni mtafiti huu ukweli unaujuwa. Mtu hawezi kwenda nchi ya kigeni kufanya utafiti ambao haujapitishwa. Ningeandika mengi, lakini huenda naongea na mtu ambaye hata concept ya statement on goals, objectives,utilization...research problem...research question(s), na hypothesis/hypotheses...methodology hajui nini. Ameparamia na kudanganya ameandika literature. Reseach assistants and or data collectors have no room in writing any section on a research proposal.
 
Sasa hapa unaonyesha mikogo isiyofaa.

Inaonekana unataka tu kujionyesha kuwa unajua maswala ya utafiti, jambo ambalo nina wasiwasi nalo.

Kwa mfano, hapo unaweka IRB (Investigational Review Board) kwa misingi na sababu zipi?

Kwani utafiti ni lazima uwe na investigational review board?

Wacha aisee, usijifanye mjuaji, kumbe hujui.
 
Aiseee!

Wewe ni mwanafunzi? Kwa hali hii, itabidi uweke juhudi sana, kwa sababu bado upo mbali sana.

Kwa andiko hili hapa pekee, linaonyesha wazi hukuelewa ulichofundishwa kuhusu taratibu za kufanya tafiti.

Kwa hakika, ungekuwa mwanafunzi wangu kwenye 'topic' ya utafiti (Research Methodology), ningekurudisha nyuma.
 
Gamba la Nyoka,

Kwenye notification naona umeni-quote, lakini niki-click, naishia kwenye post #439 uliyom-quote Gift mzalendo!! Sijui ulikosea nini wakati wa quoting, I don't know!

Lakini kwavile hoja zako zinaendana na kile ambacho nimesema hapo kabla, wacha ni-respond!!!

1. Kujenga bandari kwa target ya mzigo wa nchi moja tu nayo ni useless.

GLN, unapoanzisha biashara yoyote basi ukitaka kufanikiwa unatakiwa uwe na target market. Lakini kubwa zaidi, keyword hapa ni transshipment. Meli zinazofanya transshipment hazitoki China peke yake.

2. Je, uchumi (wa China ukiyumba), tukirofishana (na China)?

Tuache hilo la uchumi ukiyumba, manake ukweli mchungu ni kwamba, dunia ya leo ukiyumba uchumi wa China inakuwa umeyumba uchumi wa Dunia kutokana percentage export and import inayokuwa handled na China!

Je, tukikorofishana?

China hawana ujinga huo!! Kwa ukubwa wa China hivi sasa ana uwezo wa kuikea vikwazo nchi, na nchi husika ikawa inatoa makamasi! Je, unaweza kuniambia ni nchi ngapi zimewekewa vikwazo na China?

Hebu soma hii paragraph kutoka Bloomberg:-

Hiyo ni The Port of LA in California! Long Beach ndio bandari nyingine kubwa sana kwa CA! Soma hapa:
If you’re waiting on packages from China to be delivered to your doorstep, most likely they’re stuck at the Port of Long Beach (POLB). It’s the second-largest trade gateway in the country, after the Port of Los Angeles (POLA).

Unaona ni namna LA and LB Ports zinavyo-handle cargo kubwa to and from China licha ya hostilities kati ya hizo nchi mbili.

China na India hadi kutwangana, huwa wanatwangana, lakini bado kuna biashara kubwa sana kati ya nchi hizo mbili!!

Sasa hofu yako labda tuitengeneze sisi!!!

3. Bora tujenge wenyewe!!

Nimeshasema, well and good lakini amini usiamini, issue sio uwezo wako wa kujenga bandari bali uwezo wako wa ku-utilize bandari!

Kwamba, tupo strategically located, na tunazalisha landlocked countries! Nakubaliana na wewe kwa 100%! The question is: Unazilisha kwa mzigo kutoka wapi? US? EU? Japan? or China?

Na hapa ipo hivi! Kuna one Super Megaship from China, ambayo inatakiwa kuja kutia nanga East Africa ambayo kuna bigger state owned port in Bagamoyo, and another bigger Chinese operated port in Lamu!

Huyu anajua kabisa kwamba akija Bagamoyo, of course, atashusha mzigo mkubwa kweli kweli kutoka Mashariki ya Mbali! Je, atatoka na mzigo mkubwa vile vile?

Mchina sio mjinga kujenga industrial complexes kwenye bandari "zake"! Hiyo ni kuhakikishia meli import and export handling!!!

That being said, hoja yako inawezekana kabisa but not as simple as ABCs!

Anyway, ngoja niishie hapa manake tukitoa hizi facts, wanakuja wengine "Oh, umelipwa na Mchina"!
 
Kama alivyosema Kalamu1, kweli we jamaa una mbwembwe!!!

Let's assume IRB hawaku-approve! Kwahiyo research findings zitakazopatikana hapo hazitakuwa za kweli kwa sababu tu IRB hawaku-approve?!

Hivi kwa uelewa wako utafiti on Belt and Road Initiative unaangukia kwenye mahitaji ya IRB?! Au kwa uelewa wako unaamini EVERY RESEARCH MUST BE APPROVED BY IRB?

Halafu mbona unaongea kama unanifahamu?! Nini kinakufanya uamini sina uwezo wa kuandika Literature Review?! Watu siku hizi proposals zinaandikwa

Kwamba mtu hawezi kwenda nchi ya kigeni kufanya utafiti ambao hujapitishwa... kupitishwa na nani?! Na host country au na hao IRB?

Kama ni IRB then am sorry to say kwamba huijui vizuri IRB au unaijua juu juu tu!!!

Leo hii, ukitoka US, kwenda Tanzania kufanya research on, for instance, Impact of AIDS at household level, hapo lazima upate IRB approval kwa sababu hiyo ni purely Human Research!!!

Lakini unaenda Tanzania, kwa mfano kufanya utafiti kujua impact of Chinese-Tanzania Trade Cooperation halafu ni lazima upate IRB Approval? Hilo kwangu ni geni!!!
Mimi sijui lakini sidhani kama ni WEWE PEKEE unaejua hizo nondo hapa jukwaani!

Andika hayo mengi kwa ajili ya Wajuvi wenzako kwa sababu JF post haiandikwi kwa ajili ya mtu bali kwa ajili ya wanajamvi!

Anything for specific person kinaandikwa PM, so mwagika hayo manondo though you sound more of a Research Student than a Research Expert!!!

My apologize kama nitakuwa nimekushusha daraja... kwamba, you're a Research Expert!
 
Unawapa China 'credits' kuzidi kiasi aisee.

China haiwezi kuwa kila kitu kwetu.

Wakienda Lamu na mmeli mkubwa, si bado meli ndogo zitaleta mizigo hapa na kuwasambazia wenyewe wanaotegemea bandari zetu?

Mameli makubwa yapo mangapi, yapo china pekee? Hilo lilokwama juzi hapo Suez ni la china?

Bidhaa zote zitakuwa zinatoka china pekee?

Mizigo yetu na ya wanaotegemea bandari zetu, ni lazima iende china?

Kadri ya huu mjadala unavyoendelea, ndivyo kadri inavyozidi kuvutia kujenga hiyo bandari sisi wenyewe.

Wachina ni wafanya biashara, waje wajenge viwanda vyao hapo Bagamoyo, wakitumia badari yetu.. Tutaijenga kwa miaka kumi, potelea mbali, lakini tunaweza kuijenga tusipotetereka.

Hivi tutaanza kujiamini lini kwamba nasi tunaweza kujenga kitu cha kujivunia?
 
Unawapa China 'credits' kuzidi kiasi aisee.

China haiwezi kuwa kila kitu kwetu.

Wakienda Lamu na mmeli mkubwa, si bado meli ndogo zitaleta mizigo hapa na kuwasambazia wenyewe wanaotegemea bandari zetu?
Na ndo maana nimesema tangu mwanzoni kwamba Mchina hawezi kuwa competitor wa Bandari ya Dar es salaam, kwa sababu kila mmoja ana soko lake!

Lakini hata hivyo, sio kwamba nawapa credit kupita kiasi... man, China owns global trade!!! Mimi sio shabiki wa China lakini hilo halinizuii kuzungumzia uhalisia!! China keshampiku US kwa global trade!

Hebu wasome Investopedia ambao ni Wamarekani:-
Hivi kwa hilo gap unaamini kabisa kwamba nawapa credits kuzidi kiasi?!

Another major economy in the world ni European Union, na wenyewe kwenye tovuti yao wanasema:-
Wenyewe hapo wanakuambia largest export share ya EU inatoka China, na biashara yao ni USD 1.2 Billion kwa siku!! Bado unaamini naikweza China kupita kiasi?
Mameli makubwa yapo mangapi, yapo china pekee? Hilo lilokwama juzi hapo Suez ni la china?
Sio ya China peke yake lakini it's all about shipping lanes and destination! Kwa mfano, meli kutoka US West Coast haziweza kupita huku... zije kufanya nini?! US East Coast shipping lanes hazipiti huku, ingawaje inawezekana!

Meli zinazotoka Europe kwenda Asia or Far East Asia pia haziwezi kuja huku unless tuwe na biashara kubwa kati ya Europe na Africa ya Indian ocean, vinginevyo mizigo itaenda kufaulishwa to any transshipment port, na hatimae kuletwa Bongo na meli tunazoziona sasa!!!

! Kama kuna mzigo kwenye mega ship unaokuja Africa's Indian ocean kutoka Ulaya, hiyo meli itaenda kufaulisha mzigo
Bidhaa zote zitakuwa zinatoka china pekee?
Issue sio mizigo yote au hapana bali share ya mzigo!!! Sina shaka unafahamu maduka ya Afrika yame-flood bidhaa kutoka China, na mashariki ya mbali kuliko bidhaa kutoka Europe and elsewhere!
Mizigo yetu na ya wanaotegemea bandari zetu, ni lazima iende china?
Mizigo ipi?! Korosho na kahawa ya msimu, au?! Manufactured goods tunazozalisha sisi zinaweza kubebwa hata na jahazi... inakera lakini ndo ukweli wenyewe!!
Kadri ya huu mjadala unavyoendelea, ndivyo kadri inavyozidi kuvutia kujenga hiyo bandari sisi wenyewe.
Ndo maana nikasema itakuwa vizuri lakini usifanye hivyo kwa kusukumwa na uzalendo wa kijamaa bali usukumwe na sababu za kibiashara na uchumi!
Wachina ni wafanya biashara, waje wajenge viwanda vyao hapo Bagamoyo, wakitumia badari yetu.. Tutaijenga kwa miaka kumi, potelea mbali, lakini tunaweza kuijenga tusipotetereka.
hapo unatakiwa umshawishi kwa sababu mkakati wao sio huo!!
Hivi tutaanza kujiamini lini kwamba nasi tunaweza kujenga kitu cha kujivunia?
Nimeshasema, kujenga tunaweza kabisa haidhuru hata kama kujenga gati tu hadi tupate mkopo wa wazungu!!! Lakini kubwa kabisa sio kujenga bali to handle the investment profitably!

This's business, na hatutakiwi kuongozwa na patriotisms bali with commercial and economic conscious!
 
China ndiye mwenye kujua thamani ya ujenzi wa hiyo bandari na ndiye aliyeweza kuja na kutaka kuwekeza, hivyo mtoa mada ndiye alivyoweza kuchangia katika yale anayoyajua kutokana na yanayoendelea kuhusu bandari ya Bagamoyo, na waliyopondwa kuwa ni wanyonyaji ni hao wachina hivyo kila mwenye kujua nini kifanyike katika kutoa mchango wa mawazo yake yupo huru. Tushukuru hapa JF watu mbalimbali wanapata fursa ya kutoa mawazo yao kutokana na hali zetu za maisha hivyo tutumie uwanja huu wa kusoma, kuelewa na kuhabarishana kwa mambo muhimu kama haya.
Haya maproject makubwa yanataka akili kubwa kuyaendea, tusiangalie mambo ya leo na kesho bali tuangalie mambo ya miaka mingi ijayo. Tunahitaji watu kama Chige at least amethubutu kushare yale anayoyaona yamepotoshwa katika mradi huu, na uzalendo si kukubali kila linalosemwa na wakuu wetu au kukataa kila linalopingwa na wakuu wetu bali ni kuweka hoja za ukweli na mashiko kwa maslahi ya nchi yetu.
 
Uko sahihi, ila moja iangalie kwa jicho la tano, wazungu walioajiriwa ndio ilikua kivutio na kuunganisha pande 2 ili zifanye biashara tz wanasubiri nini kutumia hata advantage moja tu waliyonayo
 
Eti kama benefit zina overturn losses. Aisee ivi tutaacha lini kutumia notes za form four ku argue practical matters
 
Kwa jinsi ninavyoufahamu huu mradi umeutendea haki kwa 99%. Sina cha kuongezea. Kudos
Wasomi mnatuchanganya, mwenye guess ya kukaa madarakani muda husika ndiye atakula 10 percent. Sisi tunangojea nani mwenye nguvu ,atapewa mwali(BAGAMOYO).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…