Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Atautoa wapi mkuu!


Yeyekafanya research! Yani eti research ni sawa na mkataba,
Ndio hapo sasa

Aweke hapa hiyo research !

Mwongo mkubwa huyu mtu.

Sijui alidhani sote humu ni majuha ???

Kama ambavyo bunge with their naked King Ndugai wanavyotuchukulia wananchi ?
 
Sasa unazunguka tu mlemle kama umechanganyikiwa na kupoteza lengo.
Mara Ptriotism", wazalendo wa Magufuli - Magufuli atakuwaje na wazalendo? Hilo tu kuliweka kwenye heading ya mada yako ilifanya mada isiwe na uzito wake stahili.

Unaandika "Nyie hamna uzalendo wa kumzidi Mchina", kwani sisi ni wachina? Una maana gani hapa!

Ni nini hasa kinachokufanya ufikiri kwamba waTanzania, hata hao wanaopinga maandishi yako hapa hawataki au hawajui "umuhimu kama sio ulazima wa FDI"? Kuna sehemu yoyote umenisoma nikiandika sioni umuhimu wa FDI?..., nionyeshe maneno hayo ulipoyasoma wewe.

Hivi unafikiri mchina aje kujengewa kila kitu ndipo akaendelea? Dhana hii unaitoa wapi? Ni barabara zipi, reli gani, bandari zipi alizosubiri waje wajenge watu wengine ndipo china iendelee?

Hiyo quote ya maneno ya Mwalimu Nyerere huitendei haki kabisa kuiweka hapo, na hili ndilo linalodhihirisha kwamba wewe ni wakala tu wa hawa wanaohujumu jitihada zetu za kutaka kujikwamua kutoka kwenye hali duni ya maisha.

Halafu unajisikia raha kweli na kusema "uzalendo uliopitwa na wakati". Wewe uzalendo wako ni upi, kuuza kila kitu tulichonacho bila ya kuwafaidisha maskini wa nchi hii?

Nilijuwa toka mwanzo, na niliandika hivyo mwanzo kabisa. Mada hii umeileta hapa kwa madhumuni ya kipropaganda tu. Wewe ni wakala wa watu wasiokuwa na fikra za kuwainua maskini wa nchi hii. Hatimaye umejitoa mzima mzima mafichoni.

Magufuli alichokosea ni tabia zake mbaya na kuvuruga haki za watu, na ushamba au ulimbukeni wake wa kujenga vitu visivyostahili kijijini kwake na kutafuta sifa kusikokuwa na staha.
Vinginevyo, hata mimi ningemuunga mkono katika baadhi ya mambo aliyotaka kulifanyia taifa hili.
 
us inahangaika sasa kwa sababu master mind wa china ni wamarekani ambao wanalipwa vizuri na china
Nimeyasoma mengi kwenye andiko lako nilikotoa mstari nilio'quote' hapo juu. Nikacheka!

Lakini nilipofika kwenye mstari huu, nikashangaa!
 
Sasa kama Tanzania haitajali maslahi yake, wewe unadhani china ndio atayajali?

Hivi unaelewa unachoandika?
Ingekuwa watu hawajali maslahi mkataba ungesainiwa tangu wakati wa Mkwere! The problem, watu mnachanganya mambo, na kwavile mmemezeshwa propaganda, mnafanya judgement kupitia hizo propaganda!!!

Nadhani 2019 Kakoko aliongea na media, na hapo ndipo Merchant Group walijitokeza na kusema Kakoko ni mwongo! Na licha ya Kakoko kuitwa mwongo, akaufyata na hakutoka tena front kuji-defend kwa sababu haiwezekani DG wa taasisi kubwa kabisa uitwe muongo halafu ukae kimya!!

Lakini kubwa zaidi, tafuta clip ya Kakoko usikilize hoja zake...
 
Nimeyasoma mengi kwenye andiko lako nilikotoa mstari nilio'quote' hapo juu. Nikacheka!

Lakini nilipofika kwenye mstari huu, nikashangaa!
Kama huna access ya inner circle yao huwezi kujua ni sawa na unaona mtu kafanikiwa kweli kwenye Biashara ya Nguo, na wewe unachukua muda wa miaka 2 ukifanya uchunguzi wa hio biashara na unajua A-Z anavyofanya, unafungua hio biashara na wewe unaona haikupi faida, kumbe ana Biashara nyingine ambayo ndio inampa faida. Kwa wafanya Biashara nguli na Viongozi nguli wanajua namna ya kucheza na mifumo ya dunia
 
Wewe na mimi hatujui kwa nini mkataba haukusainiwa wakati wa Kikwete, na wala usigeuze unachopigania hapa kiwe ndio sababu ya kutugeuzia kibao.

Unasema "Merchant Group walijitokeza na kusema Kakoko ni mwongo." Huyo mchina alikwambia ukweli gani katika majibu yake. Mbona hujayaeleza hapa?

Clip ya Kakoko nimekwishaisikilza mara nyingi humu JF. Kama anasema uongo hilo sijui na wala siwezi kumtetea; lakini bado sijasikia lolote toka kwa mchina ambalo linakanusha uongo huo. Kusema tu "hiyo ni 'FEKI'", sio kueleza ukweli ni upi.
 
Mkuu 'Lob', ninakuelewa barabara kwa hayo uliyoandika hapa.

Kwa mktadha wa mada hii, tunazungumzia serikali na biashara ya mashirika yake kadhaa, na sio kila biashara.

Hapo ulivyoeleza, maana yake ni kwamba kila aina ya njia zinatumika, hata zile chafu, au sio?

Na huku katika upande wa serikali na mashirika yake machache iliyoyaanzisha kwa mikakati mahsusi ya biashara hiyo, ninachosema ni kwamba hakuna sababu yoyote inayozuia serikali isiifanye biashara hiyo kwa ufanisi. Kama ni uzembe wa wafanya kazi wake, hiyo nayo tuiite kuwa ni sababu ya serikali kutoweza kufanya biashara yake kwa ufanisi?. Watu waende maofisini kwao kuzubaazubaa tu, na biashara inakufa, hapo tuseme serikali haiwezi kufanya biashara?

AU, hao jamaa zako unaowasemea hapa na mbinu zao, wahujumu mashirika ya serikali kama mbinu za kufanikisha biashara zao, hiyo nayo tuseme ni sababu kwa nini serikali haiwezi kufanya biashara ya faida?
 
Naunga mkono hoja!
 
Hii Hoja iko vice versa!!
 
Wewe na mimi hatujui kwa nini mkataba haukusainiwa wakati wa Kikwete, na wala usigeuze unachopigania hapa kiwe ndio sababu ya kutugeuzia kibao.
Sijui vipi wakati nimekuambia?! Sijui au umeshaji-tune kukiamini kile ulichoambiwa na akina Kakoko, ambao hata hivyo sijawahi kusikia wakisema kwamba mkataba ulishasainiwa!

Okay, mimi na wewe hatujui... ina maana unashindwa hata kutumia common sense?!

Ni kauli ipi kati ya hizi umewahi kuisikia kati ya:-
1. "...majadiliano bado yanaendelea, kwa sababu kuna mambo hatujakubaliana" na,
2. "... tumevunja mkataba wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo"
Unasema "Merchant Group walijitokeza na kusema Kakoko ni mwongo." Huyo mchina alikwambia ukweli gani katika majibu yake. Mbona hujayaeleza hapa?
Hivi mtu anaposema kwa mfano: "Habari kwamba TRA hawatakusanya kodi ni uzushi", hivi hapo unatakiwa tena ufafanuliwe kwamba ukweli ni upi?
Clip ya Kakoko nimekwishaisikilza mara nyingi humu JF. Kama anasema uongo hilo sijui na wala siwezi kumtetea; lakini bado sijasikia lolote toka kwa mchina ambalo linakanusha uongo huo. Kusema tu "hiyo ni 'FEKI'", sio kueleza ukweli ni upi.
Umemsikia akisema nini kuhusu:-
1. Kodi,
2. Uendelezaji wa Bandari zingine, na
3. Muda ambao Mchina ata-operate bandari?
 
Ndio hapo sasa

Aweke hapa hiyo research !

Mwongo mkubwa huyu mtu.

Sijui alidhani sote humu ni majuha ???

Kama ambavyo bunge with their naked King Ndugai wanavyotuchukulia wananchi ?
Yaani nikuwekee Research hapa?! Na sio mkataba tena?! Btw, mimi ni muongo, unaweza kumtaja huyo mkweli? Kakoko, au?

Hapo peke yake umeshathibitisha kwamba ni Juha, kwa sababu huwezi kukurupuka na kumuita mtu usiyemjua mwongo badala ya kujadili hoja zake!
 
Mimi kama mtaalamu wa kodi naku zoom tu. Nahitaji kusoma andiko lako zaidi.
 
Wakati huu tunaganga yaliyopo. Hili kwa sasa ni kiporo au lilikwishachacha.

Nadhani ni vyema kurudia hitimisho: wewe ni wakala tu. Wewe na mimi sote hatujui usahihi wa jambo hili.

Hata tukitumia 'common sense', hiyo haitufanyi tujue lililo kweli.

Bandari ya Bagamoyo ni muhimu sana kwetu, lakini kama masharti ya ujenzi wake hayana maslahi tunayoyatafuta, haitulazimu kuingia makubaliano na huyo aliyejitokeza kuutekeleza. Tutafute njia nyingine za kuutekeleza. Na zipo njia nyingi tu za kufanya hivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…