Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Tukubali tusikubali, fursa ya Bandari ya Bagamoyo ikituponyoka tutakuja kuijutia pale Mchina atakapoamua kurejea tena Lamu, au popote pale kwenye ukanda huu wa Bahari ya Hindi!
Hakuna ushahidi popote, kwamba Mchina alishawahi kuwa na 'interest' na mradi wa Lamu. Hii ni sehemu ya upotoshaji na propaganda zinazotumika kupofusha watu ili wakubali mradi wenye masharti mabovu.

Ni sehemu mhimu ya ushahidi unaoonyesha maslahi ya watu katika mradi huo wa Bagamoyo.
 
Kwa hiyo , hiyo Bandari vitu vya nchi pinzani na china hazitapita, na nchi zingine haziruhusiwi kuweka viwanda vyao hapo Bagamoyo na sehemu zingine za Tanzania
 


Your browser is not able to display this video.
 
Hiyo ajira hapo bagamoyo atanufaika mzawa wa bagamoyo au mchina. Je unajua ni wachina wangapi watahamia bagamoyo kwa miaka hiyo 40. watoto wangapi wa kichina watazaliwa hapo bagamoyo na wao kudai viwanja vya kujenga na kufanya biashara kubwa?hii lease ya miaka 99 mbona huijadili na kuona faida yake. neno kuwa eti kutakuwa na fursa ya biashara na ajira ni la kitoto bila kujua hatima ya kuchukuliwa ardhi miaka 99
 
Duuh,Afrika tuna wazaelendo wa ajabu sana duniani.
Na sio wazalendo ila ni watu wenye roho mbaya wanaopenda kupata wao tu .

Mwacheni Yule bwana mkubwa apumzike mana wengi walimuelewa kibaguzi zaidi sio kiuchumi.

Serikali ya awamu ya sita inafanyia kazi miradi yote iliyoasisiwa na watangulizi ikiwemo mradi wa Bagamoyo. Mradi wenye tija kubwa sana Afrika nzima.
Ardhi ya Bagamoyo itakayotumika kujenga Bandari ni ndogo sana. Ni kama beach za watu wengi wanazaomiliki kule Kigamboni bila kuziendeleza. Wengi wamejigawia tu kwa manufaa na uroho wao bila tija kwa umma zaidi ya kamtandao kwa watu wachache waliotaka kuchukua kila kitu cha nchi hii kwa kigezo cha uzalendo feki.
Ardhi kwa wawekezaji wa kubwa wote zinamilikiwa kwa miaka 99 bila kujali kuwa ni wachina au wanyarwanda waishio Tanganyika au wanaChama wa chama Dume waliogawa Mali zote za umma kwa familia zao.Ni sheria iliyotungwa na bunge la CCM kuwamilikisha watu ardhi kwa miaka 99.
Kwa mtanzania yeyote asiyeona fursa ya Bandari ya Bagamoyo ni mzalendo feki kabisa.
Awamu ya tano ilikua inaendeshwa na kuongozwa na akina Sabaya na watu wa aina yake hivyo kutegemea kuwa kuna watu waliokua wana mtizamo wa miaka 100 ijayo ni kujidanganya na kujilisha upepo kwa umma. Ni awamu iliyokuwa sawa na Mkokoteni kutangulia Farasi . Yaani ni kama Farasi kukokotwa na Mkokoteni. Spika Job anaeleza vizuri sana kuhusu Mradi ule.

Mwaka 2016 Rais yule wa awamu ya tano alifika pale kyamierwa Mpakani mwa Muleba na Chato. Wananchi wakiongozwa na Diwani wa CUF waliandamana na mabango wakidai kuwa Mh.Rais wa wakati huo wa awamu ile ya Tano ataifishe shamba lenye maelfu ya Ekari la Prof.Mama Tibaijuka kwa kuwa hajaliendeleza na linawakosesha fursa wakulima na wafugaji na pia lipo kando ya ziwa Victoria na ndilo lililpo kwenye eneo zuri. Jibu alilowapa yule Mh. Hayati JpM kuwa lile shamba ni la Mjane Prof. Anna aliloachiwa na Marehemu mume wake alilolinunua miaka mingi iliyopita akiwa balaozi Uingereza na alililipia kwa miaka 99. Alidai kuwa hata wangeandamana na mabango yao kamwe asingemnyanganya mjane ardhi yakeivyo . Hivyo walikua wanapoteza muda wao na mabango yao. Ukitegemea diwani alikua ni wa CUF na wanachama walioandamana wengi walikua ni wanachama wa CUF ya wakati huo. Lakini aliwashauri wasukuma waliokua wanafuga maeneo hayo kuwa ardhi ya Tanzania ni kubwa sana na yeye ndiye Rais mwenye ardhi yate wakitaka sehemu ya kufuga waombe kwani anauwezo wa kufuta ardhi ya hifadhi na kubadili matumizi na kuwagawia wananchi alimradi wafuate utaratibu lakini sio kutaka kupora ardhi ya mjane.


Ni mfano tu kwa watanzania wanaokaa na vichaka na mapori kwa karne lakini akitokea mwekezaje wanaandamana kwa roho zao mbaya kuwa ardhi yao inachukuliwa wakati hawana matumizi nayo huku vizazi vikiendelea kumiliki umaskini wa kutisha.

Bandari ikijengwa Bagamoyo eneo kubwa linakua baharini kwani meli kubwa zinashusha mzigo kwenye kina kirefu.
Patakua na ukuaji mkubwa sana wa shughuli za kiuchumi na wageni watakua ni wengi sana. Mfano. Kwa siku moja pakiwa na uwezekano wa kuingia Malori na magari zaidi ya Elfu mbili ni fursa kwa wauza Mafuta, magesti, mahoteli au migahawa, Maduka ya spea za magari mana mengine yatafanyiwa service humu nchini. Ajira kwa askari wa Suma JKT,Ajira kwa mama ntilie n.k. Bandari zetu bado zinachelewesha mizigo kwa makusudi mana watumishi wengi wa umma wanafanya kazi mchana na usiku wanalala nyumbani huku wateja wakiwa wanasubiri na mizigo inaendelea kuingia.

Bandari ya kisisa itafanya kazi Massa 24 na management yote inapatikana muda wote mchana na usiku kama wanavyojenga madaraja ,hawalali.
Kuna wizi mkubwa sana pale Bandari ya DSM ndio maana wafanyakazi wa pale ni mabilionea watupu na ndio wanaojitahidi kuishauri serikali iachane na mradi wa Bagamoyo kwa manufaa yao.
Wanajua bandari ikiongozwa na wawekezaji ubabaishaji wao utakoma mana watu watatafuta eneo lingine kupitishia mizigo yao. Nchi zetu maskini watu wanapata pesa za ufisadi kupitia usumbufu na urasimu wa kuchelewesha huduma . Na ndicho kinachofanyika kwenye ofisi za umma.

Bandari ya Bagamoyo itajengwa kama ilivyokuwa imekusudiwa na kufanyiwa utafiti na watu wenye nia njema na wenye roho njema kwa watanzania sio mihemko ya akina Sabaya na genge lake waliokua wanatumia madaraka yao kuamua mambo kwa matamko badala ya kuwaachia wachumi kufanya kazi yao. Awamu zilizopita zilikua zinachukua mpaka wataalam kutoka nje ambao ni wazalendo ili waishauri serikali kwa uwazi na sio kinafiki na kupamba pamba kwa hofu kubwa.
 
Mtu amewekeza tril.zaidi ya 30 halafu unahoji kuwa atanufaika yeye tu bila kuangalia kuwa mtaji huo ni fedha nyingi sana.

Je, umewahi kukopa pesa ukafungua biashara halafu ukamwajiri mtanzania ukaona jinsi anavyofundishwa kuiba bila kujali kuwa wewe unadaiwa na benki?
Hujui Tanzania inawasomi wezi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki kutokana na mfumo na staili ya maisha tuliyonayo?

Umewahi kuona jinsi wafanyakazi wa viwanda vya Tanzania wanavyoiba bidhaa kwa maelfu wakati wa kusafirishaji mizigo. Dereva anaingaza semi ili apakie mifuko 500 ya sementi lakini mchongo unapigwa inazishwa 10 kila siku. Matokeo yake Tanzania bidha zote ni ghali hata Sukari inayotokana na miwa inayolimwa humu nchini zote ni kwa sababu ya wizi.
Ukienda bandari ya umma wizi ,ukienda ofisi za umma wizi,ukienda ghala la madawa ya binadamu wizi,ukienda kwenye mabomba ya mafuta wanafunga bomba na kupeleka majumbani mwao matokeo yake mafuta yanauzwa Rahisi Zambia kuliko Tanzania. Tunafudia gharama zinazofanywa na wasomi wezi badala ya kuwanyonga gerezani. Tunakaa nao mezani na kubageini badala ya kuwapiga risasi hadharani yote ni kwa sababu ni mtandao wa wasomi na wanasiasa.
Tunabaki kudanganywa kuwa wawekezaji ni mabebebru na wezi huku wanaotudanganya wakiwa wameshajilimbikizia Mali mpaka wajukuu zao hivyo urithi wao utafaa kwa kuwa taifa lina wajinga wengi na maskini wengi hivyo hao watakua ni watumwa wao na vizazi vyao.
 
Kwa hiyo , hiyo Bandari vitu vya nchi pinzani na china hazitapita, na nchi zingine haziruhusiwi kuweka viwanda vyao hapo Bagamoyo na sehemu zingine za Tanzania
Nina mashaka kama nimeelewa msingi wa swali lako, kwa sababu sidhani kama kuna nilipoashiria kusema investment itatumiwa exclusively na Wachina peke yao!

Anyway, ngoja nijaribu kukuelewa!

Nilichosema ni kwamba, kupitia Belt & Road Initiative, target ya Mchina ni kuliunganisha taifa lake na maeneo mbalimbalu duniani through infrastructure development. kutokana na hilo, amewekeza kwenye reli, bandari na viwanja vya ndege sehemu mbalimbali.

Na lengo la Mchina kufanya hivyo ni kurahisisha trade flow to and from China, kwa sababu anajua kwa mfano, kukiwa na mega port pale Bagamoyo or anywhere kwenye ukanda huu, basi few megaships from China zinaweza kubeba shehena kubwa inayoweza kuwa supplied Afrika mzima!!

Hatimae, badala ya meli kutoka West Africa kwa mfanona kufunga safari hadi Singapore (transshipment port), watakuwa wanaenda kufuata mzigo Bagamoyo, na hivyo kupunguza gharama za usafiri pamoja na risks zingine za kibiashara!!

Kuna shipping lanes from South America ambazo zinaanzia South America through Atlantic Ocean to Cape of Good Hope in South Africa, kisha zinakuja kutokea Indian Ocean on way to China (or to the nearest transshipment port)!

Hii route ni ndefu sana, sasa kama Bagamoyo inakuwa successful, hizo meli zinaweza kuchukulia mizigo Bandari ya Bagamoyo ambayo ilitarajiwa iwe transshpment port.

Maelezo hayo hayamaanishi kwamba bandari itatumiwa exclusively na Wachina peke yao!!

Hata hiyo Industrial City ambayo ilikuwa iwe funded na Oman, anyone can invest. Lakini kwavile hakuna shaka yoyote kwamba ni China ndie amehodhi biashara kubwa Afrika, basi kuna dalili zote kwamba Wachina ndio watachangamkia zaidi fursa ya hiyo industrial city!

REMEMBER... hata hivyo viwanda vilivyopo China na vinavyo-supply bidhaa duniani kote, sio kwamba vyote ni vya Wachina! Wanachofanya China ni kuwekeza miundombinu na kuvutia wawekezaji wa aina mbalimbali!!

Na kwavile Bagamoyo alikusudia kujenga megaport basi anajua industrial city ikishakuwa more succesful, bandari sio tu itapokea mizigo kutoka China na sehemu zingine duniani bali pia itasafirisha mizigo kutoka Bagamoyo kwenda sehemu mbalimbali duniani!
 
It take a witch to know one, na kwahiyo inaonesha wazi kwamba we jamaa umezoea sana kutumika na ndo maana unaona kila mtu anaweza kutumika!!

We jamaa mbona una mawazo ya hovyo sana wewe?! Yaani mtu asipokubaliana na wewe ndo ana maslahi binafsi?! Btw, hivi tangu tuanze huu mjadala, kuna hoja ipi ya maana zaidi ya kung'ang'ania kwamba:-

1. Nina maslahi binafsi,
2. Mradi una masharti mabovu!!

Sasa tukate mzizi wa fitina.

Taja hapa hayo masharti unayosema mabovu, na yamesainiwa lini!!

Nakuomba ujikite kwenye hilo suala hapa juu il hatimae nifahamu kwamba najadiliana na mtu anayeelewa anachokijadili. Kwa hofu ya kukutoa kwenye reli, sitazungumzia suala la Bandari ya Lamu BUT in your own free time, tafuta habari kuhusu the so-called LAPSSET DEVELOPMENT CORRIDOR kisha i-study kwa makini halafu oanisha na Belt & Road Initiative.

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa, LAPSSET Development Corridor ni USD 25 Billion project!! Sasa kama unaamini Kenya watakuwa na uwezo wa ku-finance such capital intensive project kwa pesa yao wenyewe, basi itoshe tu kusema kwamba, una safari ndefu sana kuelewa kinachozungumzwa!!

Na kukukumbusha tu, one of the project through LAPSEET ni ujenzi wa SGR! Mwanzoni Kenya walitoa tenda kwa Italy lakini China aka-offer some incetives kwa Kenya, na matokeo yake Kenya wakawanyang'anya Waitaliano ile tenda na kuwapa Wachina!!!

Again, jikite hapa>>> Taja hapa hayo masharti unayosema mabovu, na yamesainiwa lini!!
 
Kwani lazima hio bandari ajenge mchina hatuwezi kujenga wenyewe mdogo mdogo wakatusaidia pesa kidogo ni mpaka kummlikisha ardhi mchina...km mchina anatupenda sana na sisi ni ndugu zake atujengee apitishe mizigo yake tukatane kidogo kidogo sio aimiliki yeye
 


Tunataka wazalendo wengi wa aina yako.
Mungu akubariki sana.
Tanzania bila unafiki inawezekana .
Kazi njema iendelee.
 
Argument yako ya hiyo belt ya kibiashara ambayo western countries wanaipinga na wewe umeiweka kama kigezo cha kuimarisha hiyo dhima yako ya kupinga hiyo project
 
Cha kushangaza yeye amemponda huyo jamaa aliyembebea mikoba kuwa yeye alikuja kufanya tafiti za BRI za china.huyo beberu tayari eti alikuwa na majibu yake huyo jamaa kisa ametoka USA anapingana na Sera za uchina.
Mbona yeye ametoa makala yake lakini tayari akiwa na majibu yake kuwa anakubaliana na ujenzi wa bandari.
Kama vipi weka mkataba hapa wazi tuuchambue tuuone mbivu na mbichi.
Pia utakuwa una maslahi na msoga genge bila Shaka.
Na huu mradi ukifantika kweli nitajua jk anaingiza nchi maza ni remote tu Ila mbonyeza remote amekaa msoga pale
 
So wewe ni mpiga magufuli afu ni mkubali Sera za msoga ama.just declare your interest tukuelewe kabisa.mana inaonekana kabisa una mahaba.
Umemuelezea beberu kuwa alikuja kufanya tafiti lakini tayari alikuwa na majibu yake ya kupinga huo mradi. Na wewe umendika ugoro mwingi Ila ishu kubwa iko kwenye mradi utekelezwe basi Ila wewe umejaza ugoro mwingi ili kupoteza maboya eti unafanya tafiti na wewe.
Kubali kuwa unautaka mradi twende sawa na ukishaweka mind yako ivyo Ina Mana hautoona ubaya hata Kama upo.
Bro wewe ni particle moja within a universe huwezi amulia viumbe wengine.you are just very minor i.e very very very minor kama una maslahi na nchi weka hapa huo mktaba uangaliwe na nchi.huu mradi unapigiwa chapuo na msoga gang
 
Argument yako ya hiyo belt ya kibiashara ambayo western countries wanaipinga na wewe umeiweka kama kigezo cha kuimarisha hiyo dhima yako ya kupinga hiyo project
Nimesema, nchi za Magharibi, hususani Marekani wanaipinga BRI kwa hofu ya China kusambaza ushawishi wake sehemu mbalimbali duniani!!!

Aidha, meli hazimilikiwi na serikali bali na wafanya biashara!!!

Viwanda havijengwi na serikali bali na wafanyabiashara!

Ni kutokana na ukweli huo ndo maana pamoja na migogoro ya biashara isiyoisha kati ya US na China, bado one of the busiest port in the United States ni Bandari ya Long Beach, California ambao wenyewe wanakuambia shehena kubwa bandarini hapo inatokea China!!

Na hali ipo hivyo hata kwa Bandari ya Los Angeles!!

Na ndo maana, hata serikali ya US wenyewe wanakuambia:-
Kwamba, kumbe pamoja na migogoro yao ya kibiashara isiyoisha bado US wanaagiza zaidi bidhaa kutoka China, na kwahiyo bado US-China Shipping Lane ipo busy!!!
 
o na staili ya maisha tuliyonayo?
Aisee... hilo suala linauma sana!!! Mtanzania ni mwizi from family to a national level!! Watu wengi wanakwamishwa kwenye biashara na ndugu zao wenyewe!!

Wakati wa vuguvugu la katiba mpya (during JK's time) niliongea sana hili kuhusu ni namna gani jamii ya Kitanzania ilivyo jamii ya hovyo! NI namna jamii yetu ilivyokosa maadili!

INAUMIZA SANA!! Ajabu ya taifa hili, hata wale wachache miongoni mwetu wakiamua kuwa tofauti na wengine na hivyo kuzingatia maadili yao, basi wanakuwa maadui hata wa wafanyakazi wenzao!!
 
Kwanza kabisa wala sio kwamba Mchina anatupenda!!!

Mchina atupende kwani alianza kuzaliwa nani, akaja nani, akafuatia nani hadi akafikia Mao Zedong na Nyerere, kabla ya JK, Xi, na JPM?!

It's STRICTLY business, and one's own interest, kwahiyo suala la kutujengea ndugu zake halipo lakini anaweza kutukopesha kama anavyowakopesha wengine wote!!

Kwamba, kwani ni "lazima bandari ijengwe na Mchina"? Jibu, SIO LAZIMA... tunaweza kujenga hata sisi wenyewe, ama kwa pesa zetu za ndani, mikopo au financing plan ya aina yoyote ile!!

Hata hivyo, hoja hapa sio uwezo wa kujenga bandari bali uwezo wa kuiendesha bandari kibiashara na hatimae kutengeneza faida!! Hoja hapa ni uwezo wa kuvutia meli nyingi zaidi kutumia bandari yetu na sio bandari nyingine yoyote kwenye ukanda huu!!!

Hoja hapa ni kufahamu comparative and competitive advantages tulizonazo kulinganisha na washindani wetu waliopo na wale watakaokuja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…