- Thread starter
- #501
Pamoja sana....Nimesoma bandiko lako lenuvizuri sana...mmeeleza vizuri sana kiasi kwamba nimeafiki hili
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pamoja sana....Nimesoma bandiko lako lenuvizuri sana...mmeeleza vizuri sana kiasi kwamba nimeafiki hili
Pamoja...[emoji1317]
Hakuna ushahidi popote, kwamba Mchina alishawahi kuwa na 'interest' na mradi wa Lamu. Hii ni sehemu ya upotoshaji na propaganda zinazotumika kupofusha watu ili wakubali mradi wenye masharti mabovu.Tukubali tusikubali, fursa ya Bandari ya Bagamoyo ikituponyoka tutakuja kuijutia pale Mchina atakapoamua kurejea tena Lamu, au popote pale kwenye ukanda huu wa Bahari ya Hindi!
Kwa hiyo , hiyo Bandari vitu vya nchi pinzani na china hazitapita, na nchi zingine haziruhusiwi kuweka viwanda vyao hapo Bagamoyo na sehemu zingine za TanzaniaUTANGULIZI
Amini usiamini, wale wale ambao wamekuwa wakijivika uzalendo, linapokuja suala la Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ndiyo hao hao wanaotumikia Mabeberu bila wao kujijua!
Nitajadili mada hii katika sehemu mbili:-
Kwa bahati, binafsi mwaka 2016 nilikuwa “Mbeba Mikoba” wa Researcher mmoja wa Kimarekani (Beberu?) aliyekuwa anafanya utafiti kuhusu Belt and Road Initiative (BRI).
- Kwanini wale wanaoitwa Mabeberu hawawezi kuwa tayari kuona miradi kama ya Bandari ya Bagamoyo inafanikiwa, na
- Hoja zinazotolewa na Wazalendo Kupinga Mradi wa Bandari ya Bagamoyo.
Kazi yangu kubwa ilikuwa Literature Review!
Kwa wanaofahamu mambo ya Resech, ukifanya Literature Reviews, hususani ya wasomi kama huyu bwana, basi unapata fursa ya kufahamu mambo mengi zaidi yaliyopata kutokea hapo kabla kwenye eneo husika!
Kwa wasiofahamu, Mradi wa Bandari ya Bagamoyo ni matokeo ya (BRI) ambayo, Rais wa China, Xi, anailezea BRI kwamba:
Kwa lugha nyepesi, malengo ya China kupitia BRI ni kuiunganisha nchi hiyo na sehemu zingine duniani, hususani Asia, Afrika, na Ulaya! Uunganishaji huo ni kwa ujenzi wa miundombinu, hususani ya bandari, reli, na viwanja vya ndege.
Ndugu yangu MALCOM LUMUMBA alipata kuchambua kwa undani kabisa suala la Belt and Road Initiative!!
Na hapo sidhani kama mtu anahitaji kuwa na Shahada ya Diplomasia ya Uchumi na Ushikirikiano wa Kimataifa kunusa “threat” ya mpango huo wa China kwa mataifa makubwa, hususani Marekani!
Kutokana na ukweli huo, ndo maana haishangazi mara tu BRI ilipotangazwa, Waandishi na Watafiti mbalimbali kutoka nchi za magharibi wakaanza kulivalia njuga suala hilo.
Makala zikaandikwa, na tafiti zikafanywa kuhusu BRI, lakini makala nyingi kama sio zote zililenga kuyatisha mataifa mengine kuwa makini na BRI!
Watu hawa wakageuka kuwa “Wajomba Zetu” Afrika, huku wakituasa tusije tukaingia kwenye mtego huo hatari wa China!
Ni kupitia hizo tafiti ndipo nami nikajikuta nipo na huyo Mtafiti Msomi kweli kweli wa Kimarekani.
Huyu Bwana case studies zake zilikuwa Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, Bandari ya Hambantota (Sri-Lanka), pamoja na Bandari ya Piraeus (Ugiriki).
Ukweli ni kwamba, ilinichukua chini ya dakika 3 kugundua Mtafiti huyu ni kama tayari alishakuwa na “matokeo” ya utafiti wake hata kabla kazi haijaanza! Kwa kifupi, alionesha dalili zote za kutounga mkono Mradi wa Bandari ya Bagamoyo!
Hata "beberu" niliyekuwa namtumikia, nae alikuwa pamoja na "Wazalendo" wetu!!
Binafsi, nilikuwa “in favor of” Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, kwahiyo tukaanzisha kimdaharo kisicho rasmi!
Baada ya kuona hoja zake nyingi nazipangua, akaishia kuuliza ikiwa nadhani ni busara kwa taifa maskini kama Tanzania kuwa na bandari kubwa kama ya Bagamoyo!!
Jibu langu kwake lilikuwa rahisi sana, kwamba: Bandari ya Bagamoyo itakuwa ni kubwa mno kwa Tanzania endapo tu unaamini Tanzania na majirani zake wataendelea kuwa maskini kwa miongo kadhaa ijayo, vinginevyo, huwezi kusema ni “kubwa mno”!
Kwa ufupi, Mheshimiwa huyu, kama walivyokuwa wenzake wengine, nyimbo zao zilikuwa ni agenda ya siri ya China kuitumia BRI kama Mtego wa Madeni kwa nchi maskini!
Lilipokuja suala la Bandari ya Hambantota kule Sri-Lanka, propaganda zikasambazwa kwamba China IMEITWAA bandari ya Sri Lanka ili kufidia deni lake!
Wazalendo wetu nao wakazidaka propaganda hizo, na bila kufanya utafiti, wakaanza kutueleza kwamba “tukishindwa kulipa deni, Wachina wataichukua Bandari ya Bagamoyo kama walivyofanya kule Sri-Lanka.”
Kuweka kumbukumbu sawa, habari za Wachina KUITWAA bandari hiyo zilipotoshwa. Nitaeleza hili kinaga ubaga hapo baada kwenye makala hii.
Pamoja na suala la “Debt Trap”, watu hawa tunaowaita Mabeberu ambao kwa hili tunawaona wanajali maslahi yetu, pia wakawa wanatuambia agenda nyingine ya siri ya China ya kuanzisha “military base” kupitia BRI.
Hapa wakawa wanalenga kutuambia, hata mradi kama wa Bandari ya Bagamoyo, lengo lake ni Wachina kutaka kuweka kambi za kijeshi eneo hili la Afrika Mashariki!
Hata hivyo, hawatuambii ukweli kwamba, ni wao wenyewe ndio wanaozihofia hizo “military bases” za China endapo zitawepo!
Kila mfuatiliaji wa mambo duniani, anafahamu Marekani ina kambi za kijeshi sehemu kadhaa duniani, lakini linapokuja suala la China au mataifa mengine kufanya yale yale ambayo yeye keshayafanya kwa miongo kadhaa, hapo inageuka kuwa nongwa!
Waingereza wana msemo “If you can’t beat them, join them.”
Guys, amini usiamini, juzi yule Mtafiti niliyekuwa nae ametoa makala kwenye moja ya majarida maarufu sana duniani! Baada ya kuisoma makala ile, hapo hapo nikajisikia uchungu, na kumhurumia!
Yaani yule yule aliyekuwa anaipinga BRI, kwenye hiyo makala anaulaumu wazi wazi Utawala wa Trump kwa kutumia kete ya Debt Trap kama njia ya kuidhoofisha BRI.
Kwenye makala hiyo, kuna sehemu anahoji “Kama kweli BRI ni kitu kibaya kiasi hicho, ni kwanini basi China inaendelea kutafuta Washirika walio tayari kujiunga na BRI.”
Mwishowe, Mtafiti huyu anaisemanga serikali yake kwamba ”USA haitaweza kumzuia Rais wa China kuwekeza kupitia BRI endapo US haitakuwa na mbadala kwa mataifa yanayoshirikiana na China!
Ufaransa, imeanza kuliona hilo kama ilivyowahi kuripotiwa na France24 kwamba:
Desperation ya Mtafiti huyu bila shaka inatokana na vile anavyoona jinsi ambavyo nchi mbalimbali duniani jzinavyojiunga na BRI, kinyume na matarajio ya USA ambayo ilikuwa ina-lobby nchi zingine, hususani Washirika wake kutojiunga na BRI.
Kwa bahati mbaya sana, si Afrika, si Asia! Hadi baadhi ya nchi za Ulaya na Carribean zinaingia kwenye BRI. Mbaya zaidi, miradi ya BRI inaonekana kufanya vizuri sana!
Kwa mfano, mwaka 2016 Bandari ya Piraeus ilikuwa ndio ya kwanza barani Ulaya kubinafsishwa chini ya BRI. Bandari hii ndiyo bandari kubwa kuliko zote nchini Ugiriki, na ndio langu kuu la bahari linalounganisha nchi za EU na Asia!
Hapo kabla, bandari hii ilikuwa haifanyi vizuri, na ripoti za nyuma zilikuwa zinaiweka bandari hiyo kama bandari ya 17 barani Ulaya!
Baada ya Wachina kuchukua 51% ya hisa za bandari hiyo, na hatimae hisa hizo kufikia 67%; ripoti ya mwaka huu kupitia Port Economics inasema kwa sasa Bandari ya Piraeus ndiyo bandari kubwa zaidi (kwa kiwango cha makontena) kwenye ukanda wa Bahari ya Mediterranean, na ya 5 Barani Ulaya!!
Sasa haya ndo mambo ambayo watu hawakuyataka! Yaani bandari iliyo kwenye ardhi ya Mzungu, 67% imilikiwe na Mchina, na hapo hapo inaanza kutishia ushawishi wa bandari zingine zinazomilikiwa na Wazungu wenyewe!
JokaKuu
Tutasoma yote hayo huko baadae, lakini kwa sasa nina haya machache:
1. Hakuna nchi yoyote duniani isiyopigania maslahi yake; isipokuwa labda hizi zetu za 'Banana Republic' ambazo maslahi ya viongozi wake ndiyo yanayowekwa mbele zaidi ya yale ya nchi husika.
China wana maslahi, ndiyo maana ya hiyo BRI; kwa hiyo kama nchi inao viongozi wenye akili timamu hawawezi kusubiri mpaka waambiwe na "mabeberu" ni wapi maslahi ya nchi zao yalipo.
Kama wanajua maslahi ya nchi zao yako wapi, basi watafanya uamzi sahihi kuhusu mradi ulio na manufaa kwa nchi zao.
Tuna miaka zaidi ya sitini sasa tukijiamlia mambo yetu. Tunao watu waliosoma vizuri na kuelewa mambo vizuri karibu katika kila fani. Hatuna visingizio tena vya kusema hatuna raslimali watu. Iliyopo sasa ni kutojua tu jinsi ya kuitumia vyema raslimali hiyo.
Acha mchina aje na BRI yake atuonyeshe anataka kufanya nini, na sisi tumueleze mategemeo yetu ni nini, bila ya aibu au woga wowote.
Tujadiliane, tukikubaliana, ajenge kwa makubaliano tuliyofikia pamoja na yeye; kama hatukubaliani juu ya matakwa yake, aende zake, na wala isiwe tena hizi kelele za mabeberu hivi au mabeberu vile. Huu utakuwa ni uamzi wetu.
Na hii haituzuii kuingia kwenye mapatano mengine juu ya mradi huo, eti kwa kuogopa tu "mabeberu".
Tayari Biden na BoJo wanajadili uwezekano wa kuweka $65 Billion mezani kwa kazi hiyo ya kupambana na BRI. Hatuwezi kuwaogopa hawa wala mwingine yeyote, kama tunajua maslahi yetu ni yapi.Hizo enzi za kuyumbishwa na kugawanywa zimepitwa na wakati - ni maslahi yetu pekee ndiyo yaliyo muhimu.
Na si hawa pekee, yaani China na Mabeberu tunaoweza kushirikiana nao kujenga mradi huo, na sio lazima iwe mmoja, wawili au kundi lwa wawekezaji. Huu ni mradi mkubwa, kwa hiyo kila mtu anaweza kushiriki ankoona kunamfaa, na tutakaribisha aje tujadili, tukiafikiana anajiunga.
Tunaweza pia kuanza kujenga sisi wenyewe taratibu, kama Lamu inavyojengwa hivi sasa, baada ya kukosa mwekezaji wa kuuchukua kama huyo BRI na wengine.
2. Ukweli ni kwamba, Tanzania na pwani yake ipo pazuri mno. Wenzetu hapo juu wanahangaika kwelikweli kujiuza bila ya mafanikio yoyote.
Ni viongozi wetu tu watumie akili zao na uzalendo wao ili nchi yetu ifaidike na mahali ilipowekwa kijiografia.
Hakuna lazima ya kujisalimisha kwa mchina kama masharti yake hayana maslahi kwetu.
Hiyo ajira hapo bagamoyo atanufaika mzawa wa bagamoyo au mchina. Je unajua ni wachina wangapi watahamia bagamoyo kwa miaka hiyo 40. watoto wangapi wa kichina watazaliwa hapo bagamoyo na wao kudai viwanja vya kujenga na kufanya biashara kubwa?hii lease ya miaka 99 mbona huijadili na kuona faida yake. neno kuwa eti kutakuwa na fursa ya biashara na ajira ni la kitoto bila kujua hatima ya kuchukuliwa ardhi miaka 99Unajua ukubwa wa Ardhi ya kutoka Mtukula mpaka Tanga ina ukubwa gani?
Je,Hapo katikati kuna mradi wowote utakaofanyika kwenye hiyo ardhi ya bomba la mafuta la mabeberu ?
Je, huoni Bagamoyo utaibuka kuwa eneo kubwa la kubiashara na ajira ukilinganisha na maelfu ya Hekari za kutokea Mtukula mpaka Tanga yatakayo yamekufa bila shughuli yoyote ya kiuchumi?
Acheni Uzalendo wa Kikabila.
Mmeturudisha sana nyuma?
Duuh,Afrika tuna wazaelendo wa ajabu sana duniani.Hiyo ajira hapo bagamoyo atanufaika mzawa wa bagamoyo au mchina. Je unajua ni wachina wangapi watahamia bagamoyo kwa miaka hiyo 40. watoto wangapi wa kichina watazaliwa hapo bagamoyo na wao kudai viwanja vya kujenga na kufanya biashara kubwa?hii lease ya miaka 99 mbona huijadili na kuona faida yake. neno kuwa eti kutakuwa na fursa ya biashara na ajira ni la kitoto bila kujua hatima ya kuchukuliwa ardhi miaka 99
Mtu amewekeza tril.zaidi ya 30 halafu unahoji kuwa atanufaika yeye tu bila kuangalia kuwa mtaji huo ni fedha nyingi sana.Hiyo ajira hapo bagamoyo atanufaika mzawa wa bagamoyo au mchina. Je unajua ni wachina wangapi watahamia bagamoyo kwa miaka hiyo 40. watoto wangapi wa kichina watazaliwa hapo bagamoyo na wao kudai viwanja vya kujenga na kufanya biashara kubwa?hii lease ya miaka 99 mbona huijadili na kuona faida yake. neno kuwa eti kutakuwa na fursa ya biashara na ajira ni la kitoto bila kujua hatima ya kuchukuliwa ardhi miaka 99
Nina mashaka kama nimeelewa msingi wa swali lako, kwa sababu sidhani kama kuna nilipoashiria kusema investment itatumiwa exclusively na Wachina peke yao!Kwa hiyo , hiyo Bandari vitu vya nchi pinzani na china hazitapita, na nchi zingine haziruhusiwi kuweka viwanda vyao hapo Bagamoyo na sehemu zingine za Tanzania
It take a witch to know one, na kwahiyo inaonesha wazi kwamba we jamaa umezoea sana kutumika na ndo maana unaona kila mtu anaweza kutumika!!Hakuna ushahidi popote, kwamba Mchina alishawahi kuwa na 'interest' na mradi wa Lamu. Hii ni sehemu ya upotoshaji na propaganda zinazotumika kupofusha watu ili wakubali mradi wenye masharti mabovu.
Ni sehemu mhimu ya ushahidi unaoonyesha maslahi ya watu katika mradi huo wa Bagamoyo.
Kwani lazima hio bandari ajenge mchina hatuwezi kujenga wenyewe mdogo mdogo wakatusaidia pesa kidogo ni mpaka kummlikisha ardhi mchina...km mchina anatupenda sana na sisi ni ndugu zake atujengee apitishe mizigo yake tukatane kidogo kidogo sio aimiliki yeyeNina mashaka kama nimeelewa msingi wa swali lako, kwa sababu sidhani kama kuna nilipoashiria kusema investment itatumiwa exclusively na Wachina peke yao!
Anyway, ngoja nijaribu kukuelewa!
Nilichosema ni kwamba, kupitia Belt & Road Initiative, target ya Mchina ni kuliunganisha taifa lake na maeneo mbalimbalu duniani through infrastructure development. kutokana na hilo, amewekeza kwenye reli, bandari na viwanja vya ndege sehemu mbalimbali.
Na lengo la Mchina kufanya hivyo ni kurahisisha trade flow to and from China, kwa sababu anajua, kwa mfano, kukiwa na megaport pale Bagamoyo or anywhere kwenye ukanda huu, basi few megaships from China zinaweza kubeba shehena kubwa inayoweza kuwa supplied Afrika mzima, ambapo badala ya meli kutoka West Africa kwa mfano kufunga safari hadi Singapore (transshipment port), watakuwa wanaenda kufuata mzigo Bagamoyo!
Kuna shipping lanes from South America ambazo zinaanzia South America through Atlantic Ocean to Cape of Good Hope in South Africa, kisha zinakuja kutokea Indian Ocean on way to China (or to nearest transshipment port)!
Hii route ni ndefu sana, sasa kama Bagamoyo inakuwa successful, hizo meli zinaweza kuchukulia mizigo Bandari ya Bagamoyo ambayo ilitarajiwa iwe transshpment port.
Maelezo hayo hayamaanishi kwamba bandari itatumiwa exclusively na Wachina peke yao!! Hata hiyo Industrial City ambayo ilikuwa iwe funded na Oman, anyone can invest. Lakini kwavile hakuna shaka yoyote kwamba ni China ndie amehodhi biashara kubwa Afrika, basi kuna dalili zote kwamba Wachina ndio watachangamkia zaidi fursa ya hiyo industrial city!
REMEMBER... hata hivyo viwanda vilivyopo China na vinavyo-supply bidhaa duniani kote, sio kwamba vyote ni vya Wachina! Wanachofanya China ni kuwekeza miundombinu na kuvutia wawekezaji wa aina Qqitmbalimbali!!
Na kwavile Bagamoyo alikusudia kujenga megaport basi anajua industrial city ikishakuwa more succesful, bandari sio tu itapokea mizigo kutoka China na sehemu zingine duniani bali pia itasafirisha mizigo kutoka Bagamoyo kwenda sehemu mbalimbali duniani!
Nina mashaka kama nimeelewa msingi wa swali lako, kwa sababu sidhani kama kuna nilipoashiria kusema investment itatumiwa exclusively na Wachina peke yao!
Anyway, ngoja nijaribu kukuelewa!
Nilichosema ni kwamba, kupitia Belt & Road Initiative, target ya Mchina ni kuliunganisha taifa lake na maeneo mbalimbalu duniani through infrastructure development. kutokana na hilo, amewekeza kwenye reli, bandari na viwanja vya ndege sehemu mbalimbali.
Na lengo la Mchina kufanya hivyo ni kurahisisha trade flow to and from China, kwa sababu anajua, kwa mfano, kukiwa na megaport pale Bagamoyo or anywhere kwenye ukanda huu, basi few megaships from China zinaweza kubeba shehena kubwa inayoweza kuwa supplied Afrika mzima, ambapo badala ya meli kutoka West Africa kwa mfano kufunga safari hadi Singapore (transshipment port), watakuwa wanaenda kufuata mzigo Bagamoyo!
Kuna shipping lanes from South America ambazo zinaanzia South America through Atlantic Ocean to Cape of Good Hope in South Africa, kisha zinakuja kutokea Indian Ocean on way to China (or to nearest transshipment port)!
Hii route ni ndefu sana, sasa kama Bagamoyo inakuwa successful, hizo meli zinaweza kuchukulia mizigo Bandari ya Bagamoyo ambayo ilitarajiwa iwe transshpment port.
Maelezo hayo hayamaanishi kwamba bandari itatumiwa exclusively na Wachina peke yao!! Hata hiyo Industrial City ambayo ilikuwa iwe funded na Oman, anyone can invest. Lakini kwavile hakuna shaka yoyote kwamba ni China ndie amehodhi biashara kubwa Afrika, basi kuna dalili zote kwamba Wachina ndio watachangamkia zaidi fursa ya hiyo industrial city!
REMEMBER... hata hivyo viwanda vilivyopo China na vinavyo-supply bidhaa duniani kote, sio kwamba vyote ni vya Wachina! Wanachofanya China ni kuwekeza miundombinu na kuvutia wawekezaji wa aina mbalimbali!!
Na kwavile Bagamoyo alikusudia kujenga megaport basi anajua industrial city ikishakuwa more succesful, bandari sio tu itapokea mizigo kutoka China na sehemu zingine duniani bali pia itasafirisha mizigo kutoka Bagamoyo kwenda sehemu mbalimbali duniani!
Argument yako ya hiyo belt ya kibiashara ambayo western countries wanaipinga na wewe umeiweka kama kigezo cha kuimarisha hiyo dhima yako ya kupinga hiyo projectNina mashaka kama nimeelewa msingi wa swali lako, kwa sababu sidhani kama kuna nilipoashiria kusema investment itatumiwa exclusively na Wachina peke yao!
Anyway, ngoja nijaribu kukuelewa!
Nilichosema ni kwamba, kupitia Belt & Road Initiative, target ya Mchina ni kuliunganisha taifa lake na maeneo mbalimbalu duniani through infrastructure development. kutokana na hilo, amewekeza kwenye reli, bandari na viwanja vya ndege sehemu mbalimbali.
Na lengo la Mchina kufanya hivyo ni kurahisisha trade flow to and from China, kwa sababu anajua, kwa mfano, kukiwa na megaport pale Bagamoyo or anywhere kwenye ukanda huu, basi few megaships from China zinaweza kubeba shehena kubwa inayoweza kuwa supplied Afrika mzima, ambapo badala ya meli kutoka West Africa kwa mfano kufunga safari hadi Singapore (transshipment port), watakuwa wanaenda kufuata mzigo Bagamoyo!
Kuna shipping lanes from South America ambazo zinaanzia South America through Atlantic Ocean to Cape of Good Hope in South Africa, kisha zinakuja kutokea Indian Ocean on way to China (or to nearest transshipment port)!
Hii route ni ndefu sana, sasa kama Bagamoyo inakuwa successful, hizo meli zinaweza kuchukulia mizigo Bandari ya Bagamoyo ambayo ilitarajiwa iwe transshpment port.
Maelezo hayo hayamaanishi kwamba bandari itatumiwa exclusively na Wachina peke yao!! Hata hiyo Industrial City ambayo ilikuwa iwe funded na Oman, anyone can invest. Lakini kwavile hakuna shaka yoyote kwamba ni China ndie amehodhi biashara kubwa Afrika, basi kuna dalili zote kwamba Wachina ndio watachangamkia zaidi fursa ya hiyo industrial city!
REMEMBER... hata hivyo viwanda vilivyopo China na vinavyo-supply bidhaa duniani kote, sio kwamba vyote ni vya Wachina! Wanachofanya China ni kuwekeza miundombinu na kuvutia wawekezaji wa aina mbalimbali!!
Na kwavile Bagamoyo alikusudia kujenga megaport basi anajua industrial city ikishakuwa more succesful, bandari sio tu itapokea mizigo kutoka China na sehemu zingine duniani bali pia itasafirisha mizigo kutoka Bagamoyo kwenda sehemu mbalimbali duniani!
Cha kushangaza yeye amemponda huyo jamaa aliyembebea mikoba kuwa yeye alikuja kufanya tafiti za BRI za china.huyo beberu tayari eti alikuwa na majibu yake huyo jamaa kisa ametoka USA anapingana na Sera za uchina.Hivi nyie watu huwa hamsikii mpaka damu iwatoke masikioni eeh? Tumeshasema miradi ya wizi wizi na ujanja ujanja iliishia wakati wa Kikwete, kuanzia Magu na kuendelea tunataka kila kitu wazi wazi. Wakati wa kutuchezea akili ulienda na kikwete. Tunataka miradi ya win win situation.
Btw, ardhi yetu ya bagamoyo na uhuru wetu vina thamani zaidi kuliko maisha ya huyo mtoto aliyekamatwa na sembe.
So wewe ni mpiga magufuli afu ni mkubali Sera za msoga ama.just declare your interest tukuelewe kabisa.mana inaonekana kabisa una mahaba.Porojo at work!
Kila mwenye akili timamu anafahamu Jiwe nae ni miongoni mwa wezi wakubwa waliopata kutokea nchi hii.
Katumia billions of TZS kununua ndege, hata nikikuuliza wewe na ukoo wako wote ni wapi tenda ilitangazwa, hamuwezi kuwa na majibu! Ili asikaguliwe, akaamua kuhamishia Wakala wa Ndege za Serikali Ikulu, huku akiacha misukule yake ikiimba nyimbo za mapambio!!
Halafu hivi hujishtukii unavyosema "tunataka kila kitu wazi wazi" wakati utawala wa JPM ndio uliongoza kuficha yale yanayofanyika huko serikalini?!
Nimesema, nchi za Magharibi, hususani Marekani wanaipinga BRI kwa hofu ya China kusambaza ushawishi wake sehemu mbalimbali duniani!!!Argument yako ya hiyo belt ya kibiashara ambayo western countries wanaipinga na wewe umeiweka kama kigezo cha kuimarisha hiyo dhima yako ya kupinga hiyo project
Kwamba, kumbe pamoja na migogoro yao ya kibiashara isiyoisha bado US wanaagiza zaidi bidhaa kutoka China, na kwahiyo bado US-China Shipping Lane ipo busy!!!China is currently the United States’ 3rd largest goods trading partner with $558.1 billion in total (two-way) goods trade during 2019. Goods exports totaled $106.4 billion; goods imports totaled $451.7 billion. The U.S. goods trade deficit with China was $345.2 billion in 2019.
Mtu amewekeza tril.zaidi ya 30 halafu unahoji kuwa atanufaika yeye tu bila kuangalia kuwa mtaji huo ni fedha nyingi sana.
Je, umewahi kukopa pesa ukafungua biashara halafu ukamwajiri mtanzania ukaona jinsi anavyofundishwa kuiba bila kujali kuwa wewe unadaiwa na benki?
Hujui Tanzania inawasomi wezi kuliko nchi zote za Afrika Mashariki kutokana na mfumo na staili ya maisha tuliyonayo?
Umewahi kuona jinsi wafanyakazi wa viwanda vya Tanzania wanavyoiba bidhaa kwa maelfu wakati wa kusafirishaji mizigo. Dereva anaingaza semi ili apakie mifuko 500 ya sementi lakini mchongo unapigwa inazishwa 10 kila siku. Matokeo yake Tanzania bidha zote ni ghali hata Sukari inayotokana na miwa inayolimwa humu nchini zote ni kwa sababu ya wizi.
Ukienda bandari ya umma wizi ,ukienda ofisi za umma wizi,ukienda ghala la madawa ya binadamu wizi,ukienda kwenye mabomba ya mafuta wanafunga bomba na kupeleka majumbani mwao matokeo yake mafuta yanauzwa Rahisi Zambia kuliko Tanzania. Tunafudia gharama zinazofanywa na wasomi wezi badala ya kuwanyonga gerezani. Tunakaa nao mezani na kubageini badala ya kuwapiga risasi hadharani yote ni kwa sababu ni mtandao wa wasomi na wanasiasa.
Tunabaki kudanganywa kuwa wawekezaji ni mabebebru na wezi huku wanaotudanganya wakiwa wameshajilimbikizia Mali mpaka wajukuu zao hivyo urithi wao utafaa kwa kuwa taifa lina wajinga wengi na maskini wengi hivyo hao watakua ni watumwa wao na vizazi vyao.
Aisee... hilo suala linauma sana!!! Mtanzania ni mwizi from family to a national level!! Watu wengi wanakwamishwa kwenye biashara na ndugu zao wenyewe!!o na staili ya maisha tuliyonayo?
Kwanza kabisa wala sio kwamba Mchina anatupenda!!!Kwani lazima hio bandari ajenge mchina hatuwezi kujenga wenyewe mdogo mdogo wakatusaidia pesa kidogo ni mpaka kummlikisha ardhi mchina...km mchina anatupenda sana na sisi ni ndugu zake atujengee apitishe mizigo yake tukatane kidogo kidogo sio aimiliki yeye