Mabeberu, Vibaraka wa Mabeberu, Wazalendo wa Hayati Magufuli, na Mradi wa Bandari ya Bagamoyo

Naomba nikupuuze basi endapo hutajali?!
 
Yes ni jamii ya ovyo nenda ambako hakuna jamii ya ovyo kwani umefungwa miguu.kuna free mobility.kuna mentality hii imejengeka miongoni mwa watu wasiojua asili ya binadamu ama mtu ambaye hajaishi na jamii zingine kuwa ya kwenu ni ovyo.mkuu tafuta nchi uhame hujakatazwa. Hata sayari unahama mbona Elon Musk ongea naye utahamia Mars unadhani Kuna mahala pakatifu duniani
 
Nita so ma tena na tena mpaka nifahamu ulichoandika na ulichokikusudia.....

Barikiwa sana
 
Again, jikite hapa>>> Taja hapa hayo masharti unayosema mabovu, na yamesainiwa lini!!
Mkuu 'Chige', mimi nasoma na kuelewa unachoandika humu. Nimesoma mabandiko yako karibu yote kuhusu mradi huu wa Bagamoyo.

Pia naomba uelewe kwamba mimi sipingi mahali popote, umhimu na mahitaji ya mradi huu kwa taifa letu. Nasisitiza hili ulielewe vizuri sana.

Ukinielewa hivyo, utaanza kuona kwa nini mimi natofautiana na wewe kabisa. Ndiyo maana imenibidi nirudi nyuma na kusoma maandishi yako tena ili nijiridhishe na niliyoyaelewa kutokana na maandiko yako hayo.

Unaposisitiza nitaje hayo masharti mabovu, wewe unayo yasiyokuwa mabovu ambayo una uhakika yamo kwenye mapatano? Kama huna ni kipi kinachokutofautisha mimi na wewe.

Ukiwa ni mtu mwenye fikra, utajaribu kutuliza akili yako na kujiuliza jinsi ulivyowasilisha maandishi yako kwenye mijadala hii. Utaona wazi wewe hupo huru, akili yako imetekwa kuhimiza hayo unayoyataka yatokee, hata kama huna uhakika nayo.

Sasa kama hupiganii tumbo lako na kusahau mahitaji ya nchi yako, ingekupa muda kufikiri na kujihoji kuhusu nilichoandika hapa.
 
Mimi ninazungumzia kwa minajili ya dhana yako ya hiyo BRI na hali ya Tanzania na points ulizoelezea za nchi za magharibi kupinga hiyo BRI .
 

Kama nimekuelewa vizuri tunamuwezesha mchina asogelee soko lake kwa ukaribu hizo comparative na competitive advantage hazituhusu sisi maana hatuzalishi wao ndio wazalishaji na sisi tunabaki kuwa watazamaji wa movie ya macranes ya kichina yanavyopakua mizigo katika ardhi yetu tutakachoambulia labda service charge kwa dawasco ya maji taka au sijakusoma vizuri mkuu
 
Nashindwa kutia neno kwa sababu umeshasema mapema kwamba hujasoma, manake ingekuwa umesoma, mengi uliyosema nimeshayajadili!
Kamtuhumu Kakoko kuwa anapindisha Ukweli lakini Kakoko huyohuyo katika ufafanuzi wake alimalizia kuwa waliwaandikia barua Wachina kutaka marekebisho sehemu ambazo wanaona hazijakaa sawa ili waje waweke mambo sawa ila hawakuwa wamejibu mpaka mda uo! Hatujui kwanini wachina kwao waliamua kupuuzia mapendekezo ya serikali!
 
Mkuu,mimi nilishaacha kuamini hawa "wataalamu - wanasiasa" wetu miaka 30 iliyopita. Kakoko haaminiki.
 
Mkuu,mimi nilishaacha kuamini hawa "wataalamu - wanasiasa" wetu miaka 30 iliyopita. Kakoko haaminiki.
Changamoto inakuja tumuamini nani? Maana Kakoko, Mkinga na Magufuli wote tunaamini waliona hiyo MOU na wote waliongea kitu kimoja, Wawili hawapo Duniani aliyebaki ni mmoja tu ambaye nae si muongeaji kwakweli Kakoko!!

Issue inakuja ata kipindi wanasaini IPTL, RICHMOND, DOWANCE, SYMBION ao wataalamu wa JK na JKhuyohuyo akiwepo sasa tumuamini nani?
 
Mada yako imeegemea upande mmoja.

Unataka tusiiamini selikali ambayo ndio yenye mkataba, ila unataka tukuamini wewe unae watetea wachina ambae huna mkataba na umeandika kwa kudhani.

Sasa ili mada yako ionekane ya maana weka mkataba hapa.
Mkuu na wewe upo biased; Serikali ni nani ? Serikali ni Magufuli pekee ambaye sio mara moja amedanganya on Camera ?, Au Serikali ni Samia, Ndugai, JK na wengine wengi ambao kwa sasa wanasema Mradi ni mzuri na uendelee?

Kwahio mkuu sababu hatuna mkataba yet, hivyo hatuwezi kujua.., ila kukosa kwetu mkataba sio kwamba tunakosa logic ya kuona kwamba some things do not add up... Na wala hatuwezi kuamini kauli tu za mtu/watu ambayo kudanganya kwao ni desturi (wanasiasa)
 
Mimi ninazungumzia kwa minajili ya dhana yako ya hiyo BRI na hali ya Tanzania na points ulizoelezea za nchi za magharibi kupinga hiyo BRI .
Nahisi nashindwa kukuelewa kwa sababu swali lako hufafanui vizuri!! Na kama ni kwa mazingira ya Tanzania, nchi za Magharibi, hususani US wamekuwa wakii-discredit BRI kwa kutumia hoja zifuatazo:-

1. BRI ni Debt Trap... kwamba, Mchina anataka kutumia mipesa yake kuzikopesha nchi mbalimbali duniani ili zikishindwa kulipa, Mchina azi-own hizo nchi; ikiwa ni pamoja na kutaka kuhodhi raslimali za nchi husika ili kufidia deni lao!

Ni kutokana na hilo, ndo maana Sri Lanka waliposhindwa kuiendesha Hambantota Port commercially, na hivyo kulazimika kuuza 70% ya hisa za Hambantota, kilichofuata hapo kutoka kwa nchi za magharibi ilikuwa "...si mnaona! Tuliwaambia"

Sasa kwa mazingira ya Tanzania kama unavyosema, unaweza kuhusisha mfano wa Hambantota Port na Bagamoyo Port endapo Bagamoyo Port itajengwa kwa mkopo, na kuiendesha sisi wenyewe!!

Sasa kama tutashindwa kuiendesha bandari kibiashara na hivyo kushindwa kulipa, si tunaweza kulazimika kumtafuta mwekezaji anayeweza kuiendesha profitably?! Hapo ndipo anapoweza kuingia Mchina, na kuamua kuiendesha Bagamoyo Port!

2. Military Bases... hii ndo hoja nyingine inayotumia na USA kwamba, lengo la Mchina kuwekeza kwenye bandari, na kuita hatua hiyo ni strictly business ni janja janja tu ya Mchina lakini lengo lake hasa ni kuweka military bases kwenye nchi husika at security risk!!

Kwa maana nyingine, anatuambia Mchina akijenga bandari pale Bagamoyo, halafu akawa anaiendesha yeye, hiyo ni one step ahead toward establishing military bases!!!

Sasa basi, kwangu hizo naziita propaganda tu kwa sababu, kimsingi wanachohofia US ni Mchina kusambaza ushawishi wake duniani! Ni kichekesho kusema Mchina anataka kuweka military bases wakati US wenyewe ndo wanaongoza kwa kuwa na military bases outside the United States!!

Si kwamba Mchina HANA nia ya kuweka hizo military bases... HELL NO!! Pale Djboouti kaweka military base pua na mdomo na military bases za US na France... sasa hiki ndicho wasichokitaka US na Washirika wake!!

Sasa njia pekee wanayoitumia US ni kutumia lugha itakayopendeza masikioni mwetu.... lugha kama "...hiyo mikopo ni debt trap" au "be careful, hiyo mikopo itahatarisha usalama wa nchi zenu" wakati US hao hao ndio wanaoongoza kudukua mawasiliano ya mataifa mengine, including mataifa ambayo ni washirika wake!

HOWEVER, hivi sasa ukifuatilia tayari wamegundua "threat card" imeshindwa kusaidia kwa sababu mataifa mengi zaidi yanaingia kwenye BRI. Ni kutokana na hilo, ndo maana nchi kama Ufaransa imeamua kutaka kurudisha mpira kwa kipa kama ilivyoandikwa kwenye website ya TV Station inayomilikiwa na serikali, yaani France24 kwamba:-


Hiyo ni kauli ya serikali, iliyoandikwa na media ya serikali husika; serikali hiyo hiyo "inayotutetea" dhidi ya Mchina!!!

Sasa, ni kweli wanatutahadhalisha dhidi ya China, au wanatutahadhalisha ili tutekeleze ajenda yao ya kupambana na na influence ya Mchina?

What about the United States?

Mchambuzi mmoja wa Kimarekani anaandika kwenye Jarida la Fortune kwamba:-

The U.S. can’t keep waiting for China’s Belt and Road Initiative to fail​

Kisha anaendelea:-

Nimemfuatilia huyo Mchambuzi, ana makala kwenye magazeti yote makubwa ya ughaibuni unayoyafahamu, lakini hapo kwenye RED anazungumza wazi ni namna gani Trump Administration imetumia miaka 4 kututahadhalisha ni namna BRI ilivyo Zimwi kwenye ngozi ya kondoo... na hapo ametumia neno SULLY!

Mchambuzi huyo anaendelea:-
Kisha anakumbusha kauli mbalimbali za viongozi wa Marekani katika kampeni yao ya ku-discredit BRI, kwamba:-
Nadhani jana niligusia suala la mataifa ya magharibi kuanza kuisaliti US kwenye kampeni zake dhidi ya BRI, na hapo juu Italy unaiona!! And it's a matter of time kabla washirika wake wengine hawajamsaliti kwa sababu ukweli mchungu ni kwamba, katika dunia ya leo unaweza kumkwepa Mmarekani lakini sio Mchina!!

Hapa chini jamaa anapigilia msumari:-
Sasa unaweza kuhoji tena in relation to Bandari ya Bagamoyo!!! Jibu la hilo lipo kwenye ufunguzi wa thread yangu kwamba:-
Amini usiamini, wale wale ambao wamekuwa wakijivika uzalendo, linapokuja suala la Mradi wa Bandari ya Bagamoyo, ndiyo hao hao wanaotumikia Mabeberu bila wao kujijua!
Kwamba, kwavile USA wanaiona BRI Threat kwa upande wao, basi tutarajie mengi mabaya yatasemwa yatakayotokana na miradi ya BRI!! Mengine ni ya kweli na mengine ni proganda!!

Wapiga propaganda wa magharibi wataandika hili na lile, na kisha miongoni mwetu tutayadaka bila kuyafanyia uchunguzi na kudadisi undani wake!!!

Na ukweli mchungu ni kwamba, ukaribu wa Tanzania na Uchina unaweza kuitisha zaidi US pengine kuliko possible investment ya nchi yoyote!!!

So, the question is: Kama kuna wapuuzi wanaosema watu aina yangu tumenunuliwa na Mchina, au tuna maslahu binafsi; what kama ni wao wenyewe ndio wamenunuliwa na hao Mabeberu ili kutishia watu wauogope mradi?!

And REMEMBER... hapa wala simaanishi kwamba ile framework agreement (sio MKATABA, ingawaje watu wanazugumzia mkataba) ni bora... LA HASHA, na ndo maana kwenye thread yangu nimeacha sehemu kwa ajili ya RECOMMENDATION!!

Binafsi, nina mengi ya kueleza kwenye financial aspects ya mradi kama vile jinsi ya ku-handle masuala ya kodi, na mambo mengine yenye maslahi kwetu, including muda wa ku-operate (from Build Operate Transfer Scheme)!!!

Hivi sasa naifanyia personal research Islamic Build Operate Transfer Scheme!!!
 
Sijaelewa hapo uliposema "kamtuhumu", ambapo inaonesha someone else kamtuhumu huyo Kakoko! If so, huyo someone else ni nani?!

Au ulitaka kuandika "kumtuhumu", ukiwa na maana kwamba mimi namtuhumu Kakoko ambae kwa mujibu wa maelezo yako aliwaandikia Wachina?!

Kama NDIYO unavyomaanisha, hivi kabisa bado unaendelea kuamini yaliyokuwa yanasemwa na utawala uliopita?! Utawala ule ule ambao tuliambiwa hakuna corona, uchumi unapaa, pamoja na corona bado watalii wanaendelea kumiminika, n.k!!

Anyway, Mwakilishi wa kampuni iliyotaka kujenga hiyo bandari walikanusha vikali madai hayo ya Kakoko, na akasema wazi kwamba Kakoko anasambaza Fake News!!

Jinsi Mchina alivyokuwa ameongea lugha kali, ungemtarajia Kakoko atoke tena mbele kutoa ushahidi wa aliyosema ili kulinda image yake binafsi, na image ya TPA, lakini Kakoko akaufyata!!

The Citizen waliandika habari hiyo kwamba:-
Mr Mao said they have received no contract terms or an ultimatum from authorities regarding Bagamoyo Port, noting that they never dealt with Mr Kakoko to whom the reports were attributed.
Kisha wanamnukuu Mr. Mao
Ilikuwaje Kakoko akakaa kimya pamoja na tuhuma mzito kama hizo?!
 
Ok Brother all the Best, kutokana na Elimu yako Mradi wa Bagamoyo port upo sawa au haupo sawa.


Na kwanini tusifanye on phases ili kupunguza risk cost
 
Unajua ni heri ungeandika kile kilichopo kwenye mkataba ulichokiona kuliko maneno ya Mchina kasema mchina kasema!! Embu tumia ubongo wako unafikiri ye anaweza kujisema vibaya? Weka ulichokiona kwenye mkataba habari za Mr. Mao alisema na aliandika kwa hasira achananazo hazina maana.
 
Duh! Nyie watu bhana... sijui huwa mnamsoma mtu na kumwelewa kabla hamjatoa hoja zenu, au huwa mnakurupuka tu! Hoja yako ilikuwa ni hii hapa:-
Kwamba, ingawaje namtuhumu Kakoko lakini yeye alifafanua kwamba alimwandikia Mchina lakini Mchina hakujibu!!!

Now tell me: Kwahiyo unaamini hoja yako hiyo inaweza kujibiwa na mkataba na sio Mchina aliyeandikiwa na Kakoko, ambae nimekuonesha hapo kwamba Mchina kakanunusha na kumuita Kakoko ni mzushi?!

Hivi kuna ubaya hapo zaidi ya ule wa Kakoko kuitwa muongo na mwenyewe akakaa kimya?!

Sasa kama unaamini Mchina hawezi kujisema vibaya, how come Kakoko akakaa kimya pamoja na kusemwa vibaya?!

Halafu acheni hizi hoja nyepesi za kudai mikataba wakati tangu mzaliwe serikali haijawahi kuwaonesha hata mkataba wa ujenzi wa vyoo, lakini leo mnanidai mimi mkataba!! Huyo Kakoko mliwahi kumdai mkataba ili kujiridhisha ikiwa aliyowaambia yana ukweli, au mnatumia hoja ya mkataba kama defensive mechanism ya kukwepakujadili hoja!

Na hivi nilichokisema mimi kuhusu mradi ni maelezo ya Mchina, au ni maelezo yaliyotokana na matokeo ya utafiti?!
 
Ok Brother all the Best, kutokana na Elimu yako Mradi wa Bagamoyo port upo sawa au haupo sawa.
Kama hiyo "mradi upo sawa au hapana" unamaanisha "framework agreement(ambayo watu wanaita mkataba) ipo perfect, jibu ni VERY SIMPLE, katu haiwezi kuwa perfect, na kwahiyo majadiliano bado yanahitajika!!

Watu wanasaini framework agreement badala ya mkataba kwa sababu ya kutoa room ya majadiliano zaidi kabla ya mkataba kusainiwa rasmi!!

More often than not, hata huo mkataba hauwezi kuwa perfect, seuze framework agreement!!! Uzuri wa framework ndo huo, inakuwa hamjafikia tamati ya makubaliano!!

That having been said, ni LAZIMA framework agreement idadavulie kwa undani zaidi ili kabla hatujasaini mkataba, tuwe tayari tumezingatia maslahi mapana ya taifa! Lazima tuwe tumejua tupo tayari kuachia nini, na kutoachia nini; na ndo maana kwenye thread yangu hii, Post #8 nimeacha nafasi kwa kuandika "MAPENDEKEZO... Reserved For Later"!

Hapo nilikusudia niandike yale ninayoamini tukiya-demand kwenye mkataba basi mradi utakuwa na manufaa kwetu! Hapa panahitaji kujadili hadi unforeseen situations!!
Na kwanini tusifanye on phases ili kupunguza risk cost
Hata kwa sasa sio kwamba mradi utajengwa kwa mara moja... la hasha lakini hapo unaposema "...kwanini tusifanye" unamaanisha kwanini kwa ujumla wake tusijenge wenyewe kwa awamu, jibu ni kwamba inawezekana lakini ni suala linalohitaji mjadala!!

Kama kujenga wenyewe bandari ya kawaida tu, it's okay, lakini kama kujenga kama ile aliyokusudia Mchina, it's TOO RISKY coz' hatuna competitive and comparative advantages za kuweza kuendesha bandari kubwa kama hiyo!!
 
PLAIN BRAIN
 
Uko very deep, informed and authoritative. Also your art of presentation is scholarly
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…